Majambazi wameingia kwa staili Mpya Jijini Dar.

2 views
Skip to first unread message

Fusha

unread,
Feb 2, 2007, 5:58:43 AM2/2/07
to Mtaa Kwa Mtaa
Mwanaripoti wetu anaripoti

Kamanda Masindoki Masindoki alisema hivi sasa kuna ujambazi
unaoendeshwa na baadhi ya watu wanaokwenda katika nyumba za watu
wakidai ni mafundi wa umeme, simu au wanadai kutumwa na wenye nyumba
na wanapofunguliwa mlango huwavamia watu wanaowakuta na kupora vitu.

Alisema Januari 12 polisi walipata taarifa kuwa kuna majambazi
waliokuwa wamepanga kwenda kupora katika nyumba moja iliyopo mtaa wa
Sofia, Ilala. Waliwavamia watu hao na kuwakamata watuhumiwa sita.
Kamanda aliwataja watuhumiwa kuwa ni Kombo Abdallah, Mgonza Ally,
Bekini Mganga, Athumani Mtete, Said Jemedari na Amir Hussein, ambao
wanaendelea kuhojiwa.

Wakati huo huo, Msindoki alisema watu sita wanashikiliwa na polisi kwa
tuhuma za kuvunja na kuiba kasiki lililokuwa na Sh milioni 3.6, mali
ya Grace Mathias. Alisema Januari 12 katika mtaa wa Sikukuu,
watuhumiwa hao walitoboa duka la Grace na kuiba kasiki na kuondoka na
teksi aina ya Toyota Chaser. Wakiwa njiani polisi waliwatilia shaka,
wakawasimamisha na kuwakamata.

Masindoki alisema walipohojiwa walikiri kuvunja duka hilo na polisi
walipofungua kasiki hiyo walikuta Sh milioni 3.6. Grace alipofika
polisi na kuhojiwa alikubali kuibiwa na kukiri kuwa hizo ni fedha
zake.

Watuhumiwa wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo ni Abdallah Said, Issa
Shabani, Seif Abushiri, Rashid Khatibu ambaye ni dereva teksi, Jackson
Elias na Wilbert Nguku.

Hivyo ndugu zangu tuwe macho na dizaini ya wizi kama huu.

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages