Majambazi wasalitiwa na Raia wema Dar!

6 views
Skip to first unread message

Fusha

unread,
Feb 2, 2007, 5:53:39 AM2/2/07
to Mtaa Kwa Mtaa
JESHI la Polisi limemkamata mtu anayetuhumiwa kukodisha silaha kwa
majambazi Dar es Salaam, imefahamika. Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ilala, Masindoki Masindoki alisema jana kwamba jeshi hilo pia
linawashikilia watu 20 kwa tuhuma za ujambazi.

Masindoki aliwaambia waandishi wa habari kuwa Januari 10, polisi
kupitia wasiri na raia wema walipokea taarifa ya mkutano wa majambazi
katika baa ya Airport, Kipawa wakipanga kwenda kufanya uhalifu
Magomeni.

Alisema polisi walikwenda katika baa hiyo na kuwakamata watu watatu
aliowataja kuwa ni Abdu Amiri maarufu kama Subo, Ramadhani Kondo -
maarufu Mzee Pilipili na Elias Asukule -maarufu kama Shanti na
walipohojiwa walikiri kumsubiri mtu anayeaminika kukodisha silaha,
waliyemtaja kwa jina la Babu.

Watuhumiwa hao pia walisema wamekuwa wakikodi silaha kutoka kwa Babu
na wanapomaliza shughuli zao hurudisha silaha hizo na kumgawia kiasi
fulani cha fedha. Kutokana na taarifa hiyo polisi waliamua kufuatilia
Babu na kumkamata akiwa Magomeni Kagera, alisema Masindaki.

Kamanda alilitaja jina halisi la Babu kuwa ni David Kasambala maarufu
pia kwa jina la 'Father'. Alisema alipohojiwa alikiri kumiliki shotgun
na kueleza alipoificha. Polisi walipofanya upekuzi nyumbani kwake
waliikuta bunduki hiyo, risasi tisa aina ya banku, risasi nane za
bastola, magazine moja ya SMG. Mtuhumiwa huyo alikiri kuzikodisha kwa
majambazi, alisema Masindaki.

Alisema polisi pia walimkamata mtuhumiwa mwingine aliyejulikana kwa
jina Mark Masoya -maarufu kwa jina la Kofii au Isaluche, mkazi wa
Vituka aliyetuma ujumbe wa simu kwa Kasambala akitaka kukodishwa
silaha. Aliutuma ujumbe huo, 'Babu' alipokuwa akiendelea kuhojiwa na
polisi.

Kwa mujibu wa Kamanda Masindoki, Masoya alipohojiwa aliwataja
watuhumiwa wengine, Masona Marwa, Marwa Chacha maarufu kama Nyawicho
na Daniel Kihungi maarufu kama Mwita. Masindoki alisema watuhumiwa hao
wote wanaendelea kuhojiwa kubaini makundi mengine ya majambazi.

Riport
Na Mpekuzi wetu
Mtaa kwa Mtaa

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages