---------- Forwarded message ----------
From: Mobhare Matinyi <
mat...@hotmail.com>
Date: Sun, 31 Mar 2013 05:31:52 +0000
Subject: [Mabadiliko] Watanzania makini jazeni nafasi hizi .........
To: Mabadiliko <
mabadilik...@googlegroups.com>, Wanabidii
googlegroups <
wana...@googlegroups.com>
Serikali yatangaza nafasi za kazi 1,134. Serikali kupitia Ofisi ya
Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia
Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza nafasi wazi za kazi kama zilivyo
katika Tangazo la Lugha ya Kiingereza na Kiswahili.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti
ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni
www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya
Waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.
Daudi alifafanua kuwa Waajiri hao ni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wizaraya Mambo
ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Afisa Mtendaji Mkuu Wakala
wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu
Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na
Ajira, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara.
Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Katibu Mkuu Wizara ya
Maji, Katibu Ofisi ya Rais Maadili,
Wengine ni Katibu Tawala wa Mkoa Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya,
Mwanza, Shinyanga, Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani,
Mara, Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora, Tanga, Katavi na Arusha,
Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mkurugenzi Halmashauri
Manispaa Iringa, Songea, Shinyanga,
Morogoro, Singida, Kigoma/Ujiji na Temeke.
Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya
Mufindi, Kyela, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba,
Namtumbo, Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru,
Ukerewe, Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa, Meatu, Shinyanga, Kishapu,
Kilosa, Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda,
Monduli, Ngorongoro,Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo,
Tabora, Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto, Handeni, Pangani, Kibondo,
Chamwino, Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa naTandahimba. Mkurugenzi
Halmashauri ya Mji Njombe, Kibaha, Baraza la Kiswahili la Taifa
(BAKITA) na TEMESA.
Katibu huyo amesema kuwa nafasi hizo zilizotangazwa zimegawanyika
katika kada zifuatazo; Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta daraja la II –
(Nafasi 10), Afisa Vipimo II – Nafasi 6, Mpima Ardhi daraja la II
(Nafasi 26), Mhandisi daraja la II – Ufundi Umeme – Nafasi 9, Afisa
Mipango Miji daraja la II– Nafasi 13, Mhandisi daraja la II - Ujenzi
(Nafasi 16), Mhandisi daraja la II - Maji (Nafasi 13), Afisa Misitu
daraja la II (Nafasi 7), Afisa wa Sheria daraja la II – nafasi 3,
Mtakwimu Daraja la II – nafasi 8, Mthamini daraja la II – Nafasi 7,
Mkadiriaji Ujenzi daraja la II – nafasi 4, Afisa Ufugaji Nyuki Daraja
la II – nafasi 1, Mhandisi Daraja la II – Nishati (Nafasi 3), Msanifu
Majengo Daraja la II– (nafasi 3) na Mjiolojia Daraja la II – Nafasi 7,
Fundi Sanifu daraja la II (Ujenzi) -Nafasi
26, Mvuvi Msaidizi Daraja la II – nafasi 8 na Fundi Sanifu Msaidizi
(Maji) -nafasi 19.
Nafasi nyingine zilitotangazwa na Serikali ni Nahodha Daraja la II –
Nafasi 6, Fundi Sanifu daraja la II - Haidrolojia -Nafasi 6 ,Fundi
Sanifu Daraja la II -Nafasi 6, Msaidizi Misitu Daraja la II – nafasi
7, Fundi Sanifu Daraja II – Ramani – Nafasi 6, Fundi Sanifu Daraja la
II –Maendeleo ya Jamii– Nafasi 3, Dereva Mitambo Daraja la II– nafasi
1, Mpiga chapa msaidizi- Nafasi 5, Operata wa kompyuta msaidizi -
nafasi 3, Fundi Sanifu Daraja la II - Migodi – nafasi 9, Polisi
Msaidizi– Nafasi 5, Mpokezi–Nafasi 1, Katibu Mahsusi daraja la
III-nafasi 10, Mlinzi –Nafasi 100, Dereva Daraja la II – nafasi 178,
Msaidizi wa Ofisi– Nafasi 30, Afisa Kumbukumbu daraja la II– nafasi 1,
Mwenyekiti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya – nafasi 5, Afisa
Mtendaji wa Kata Daraja la III– nafasi 10, Afisa Mtendaji wa Kijiji
Daraja la II– nafasi 6.
Aidha, kada nyingine ni Afisa Mtendaji wa Kijiji daraja la III) –
nafasi 232, Afisa Mtendaji Mtaa daraja la III– nafasi 3, Afisa Lishe
daraja la II– nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II - Ufundi na Umeme,
Afisa Biashara msaidizi– Nafasi 1, Mchapa Hati daraja la II – Nafasi
1, Mhandisi Daraja la II –Baharini-(nafasi 1), Dereva Mitambo Daraja
la II – (nafasi 1), Dereva wa Vivuko daraja la II – Nafasi 3, Mkufunzi
Mwandamizi Daraja II - Nafasi 1, Mkufunzi Daraja ii - Nafasi 2, Fundi
Sanifu Msaidizi (bomba)–nafasi 3, Fundi Sanifu Msaidizi (Umeme)
–Nafasi 4, Mkufunzi Daraja II– nafasi 3, Mkufunzi daraja la II
-Jiolojia – nafasi 1, Mkufunzi Msaidizi– Jiolojia – nafasi 1, Fundi
Sanifu daraja II -Ubunifu Mipango Miji – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja
II- Urasimu Ramani – Nafasi 5, Fundi Sanifu daraja II- Uchapaji Ramani
–Nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II -Maabara– nafasi 13, Fundi Sanifu
Msaidizi (Ujenzi– nafasi 1), Fundi Sanifu daraja la II -Nafasi 4,
Wakufunzi wasaidizi – nafasi 54 na Mhasibu Mkuu daraja II.
Katibu alifafanua kuwa nafasi 949 zilizoko katika tangazo la Kiswahili
ni kwa ajili ya Waajiri walioainishwa hapo juu na kwa Tangazo la
nafasi wazi 185 zilizoko katika tangazo la lugha ya Kiingereza ni kwa
ajili ya Taasisi na Wakala mbalimbali za Serikali.
Daudi amesema mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 9
Aprili, 2013.
Aidha, amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kufungua matangazo
yote mawili ya kazi na kuzingatia masharti ya Matangazo yote kama
yalivyo katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili kabla ya kutuma maombi
yao.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 27 Machi, 2013
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
kwa Barua pepe;
g...@ajira.go.tz
This e-mail address is being protected from spambots, you need
JavaScript enabled to view it
au Simu; 255-687624975
http://www.ajira.go.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=129:taarifa&catid=1:latest-news
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la ‘Mabadiliko’.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii:
mabadilik...@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda;
mabadilikotanza...@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google
Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send
an email to
mabadilikotanza...@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
"For hope is but the DREAM of those that wake"
LOVE, HOPE AND FAITH!