Udaku Specially |
TID ASEMA "YES AM SMOKING MARIJUANA(BANGI) ILA MADAWA YA KULEVYA NO Posted: 06 Jul 2013 10:51 AM PDT Mtangazaji wa kipindi cha The Sporah Show, Sporah Njau hivi karibuni alijikuta katika wakati mgumu alipofanya interview na muimbaji mahiri nchini, Khalid Mohamed aka TID kwenye show hiyo kutokana na maswali yake yaliyogusa mambo ya ndani ya mkali huyo. Sporah alimuuliza maswali yaliyogusa masuala mazito katika maisha ya msanii huyo ikiwa ni pamoja na shutuma kuwa anatumia madawa ya kulevya, tabia yake inayotafsiriwa kama ya dharau, kuwa na hasira, kupungua kwa afya yake na suala la kifo cha aliyekuwa rafiki yake, Albert Mangweha. TID alikuwa akijieleza zaidi kwa lugha ya Kiingereza huku akitumia Kiswahili kidogo. Haya ni baadhi ya masuala aliyoulizwa na kujibu: Kuhusu sababu ya kifo cha Ngwair I don’t have a crew kwasababu he was away, he was in South Africam actually in Johannesburg. He was on tour it was actually a proper time we wanted him to go that big baada ya ile nyimbo tuliyofanya ‘No Beef’ and it was getting a lot of airplay, so we thought that could be the right time for him. We gave him a concert abroad ili apate exposure so when he comes back he is gonna be on the right time. Lakini ndio hivyo bahati mbaya we just heard like he was unconscious then he stopped breathing, they took him to hospital and he was lastly pronounced dead. Sasa mimi hata sijui, I am in Tanzania and I haven’t slept for the past two months kwahiyo sasa sielewi ni nini tatizo limeenda. Wao wamesema it’s a sudden death hivyo ndivyo wameandika kwenye certificate yake ya death. I am gonna miss this guy, damn only God knows how much. Kuhusu lini ataacha kuwa mtu wa sifa This is whom I am, sometimes it’s hard for people to understand, me I am not like them, I am different, I am the other guy they see me on TV so when they think I have Misifa, maybe that’s the attitude that I was born with. It’s very hard to explain, it’s very hard to make everybody like you while you are on the spotlight, it’s impossible. And sometimes I have to get it along, all my tweets are everywhere, it’s crazy. When I’m saying am taking a shower right now, people say ‘why are taking shower right now’ they have to comment about me. Kuhusu shutuma kuwa anatumia madawa ua kulevya People say a lot of things about me, they were just trying to exaggerate my life. Yes I’m smoking marijuana, that’s my sensitive thing. Hata kama promoter amenikuta nimelala, I had too much to drink., I am tired of the show, nimesafiri siku nzima, nimetoka zangu Dar es Salaam kwenye msiba, I have to be tired, I am a human being, I don’t have any access to drugs in the UK, how can I get drugs here? That’s impossible but to me it’s because I am on the spotlight and everybody is tryna get the advantage of it. And I really don’t know who are they, do they like me? Do they fancy my fortune? Do they wanna be like me? Do they appreciate the talent I have been giving for all these years? Au do they want to come around and make a point? So I am gonna do what I do best, give them right tunes, connecting my music to the world like what I am doing right now. These is more like a third time me and you (Sporah) we are talking right here, people with drugs don’t have a capability of making music. Some of them do, but I am not the one, I am very focused I have a family, I have a band, I need my future, I need to fulfil my dream. So whatever they say, it’s not gonna stop me from doing, being the best. Kuhusu kupungua kwa afya yake (hapa TID alikasirika kiasi cha kubadilika na kutaka kutoendelea na show) I’m fit, I am healthy, I don’t care about what people say about me, it’s my weight, it’s my life, it’s my health. If am good, am good. Do you think you have good healthy at the moment? Yeah I am fine, I am healthy I don’t think you are healthy though Are you my doctor? Are you tryina be my doctor? I mean you don’t look healthy You think so but I look healthy. You haven’t taken me to hospital how do you prove such a thing? So you have a point, you brought me here today to tell me unhealthy, you wanna have an interview with an unhealthy person? I really don’t appreciate what you are saying if you are coming to the point like telling me straight I am unhealthy. I am healthy, you are not a doctor, you haven’t checked me yet so don’t tryna be.. (tusi) Kwenye interview hiyo pia, TID alidai kuwa anatarajia kuja na filamu ya Girlfriend Part 2. Source:Bongo 5 |
CRDB YASHUTUMIWA KUWA NA UBAGUZI KATIKA UTOAJI WA KAZI KWA WANAFUNZI WA VYUO Posted: 06 Jul 2013 10:44 AM PDT UBAGUZI wa bank ya CRDB katika utoaji wa ajira kwa wasomi wetu hapa nchini...Ukisoma hilo tangazo lao hapo chini utaona wamesema upendeleo ni kwa chuo cha UDSM..Swali ambalo watu wengi wanalojiuliza je Tanzania kuna vyuo vingapi ?
------------------------------------------------------------------------ HILO NDIO TANGAZO LAO LA KAZI Internship opportunities with CRDB Bank PLC. These opportunities cover different regions/branches all over the country as indicated below. |
BAADA YA JOYCE KIRIA KUSHAURIWA AMWAMBIE MUMEWE AACHANE NA SIASA NA HII NDIO KAULI NA MSIMAMO WAKE Posted: 06 Jul 2013 08:51 AM PDT Hapa kuna swala nahitaji kuliweka sawa, naamini tutaelewana fans zangu wote
My Hubby Henry Kilewo. My Hubby Henry Kilewo akiwa katika shughuli zake za kisiasa. Nimeolewa na mwanasiasa, mume wangu Henry Kilewo ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Kinondoni, Ila mimi si mwanasiasa(nahudumia watu wote wenye vyama na wasio na vyama) Our Wedding Day, Nikila kiapo, "KWA TABU NA RAHA" Muda nakubali kuolewa naye nilifahamu fika kuwa yeye ni mwanasiasa, Ila nitamsupport mume wangu kwa kazi yake aliyoichagua, siwezi kumwambia AACHE SIASA, Hilo kwa kweli HALIWEZEKANI, Hata yeye hajawahi hata siku moja kuniingilia katika kazi yangu ya kutetea haki za wanawake na maendeleo ya wanawake kwa ujumla(WANAWAKELIVE) na kuniambia niiache. Ila nina swali la kuuliza hapa "KILA MTU ANAPOPATA TATIZO KATIKA KAZI YAKE ANATAKIWA KUIACHA???" Mfano Daktari akipata tatizo katika kazi yake aache? Ama Mwalimu ama mtu yoyote yule kwa kazi anayoifanya akipata changamoto anatakiwa kuacha???? Fans Wangu wote naamini mtakuwa mmenielewa na mtaendelea kuwa nami all the way, Msimamo wangu ni huu, Nitasimama upande wake na kuendelea kumsupport mume wangu Henry, SIASA ni kitu anachokipenda SIWEZI KUMWAMBIA AACHE |
PHOTOS:BEAUTY OF THE DAY-ELIZABETH LULU MICHAEL Posted: 06 Jul 2013 08:44 AM PDT |
UKWELI MCHUNGU:WASOMI WETU HAWANA SOKO KIMATAIFA Posted: 06 Jul 2013 08:41 AM PDT Najua kauli yangu hii itawakera wengi hususan hao wanaojiita wasomi, lakini najua kwamba ukweli mara nyingi huwa unauma sana.
Katika orodha ya nchi za Afrika ambazo wasomi wake wanaibwa na kusombwa na kupelekwa huko Ulaya na Marekani kufanya kazi , Tanzania haitajwi kabisa. Watanzania wengi wanaokwenda nje kufanya kazi, ni vibarua zaidi, wenyewe wanajiita wabeba mabox, na hata kama ni wasomi, basi utawakuta wanafanya kazi ambazo huwezi kusema zitaweza kuisaidia nchi. Hata hivyo wapo Watanzania wachache sana ambao wamenunuliwa nje na kufanya kazi huko kwa sababu ya uwezo wao kiufahamu katika taaluma zao. Lakini hii yote ni kutokana na mfumo wetu wa elimu ambao kwa miaka mingi umekuwa ukidumaza akili zetu. Mara nyingi wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipiga kelele kuhusu haja ya Serikali kubadili mfumo wa elimu ili kuweza kuwashindanisha wasomi wake na wasomi wa nchi nyingine duniani lakini jambo hilo limeonekana kama vile halina maana. Najua serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi imeshawahi kubadili mitaala ya elimu mara kdhaa, lakini ninachojaribu kusema hapa ni je tabia ya wanafunzi kukariri ili wafaulu mitihani badala ya kuelewa imekomeshwa kwa kutafuta chanzo chake? Ukweli ni kwamba, ni vigumu kwa wasomi wengi wa Tanzania kushindana kwenye soko la dunia kitaaluma kwa sababu, hawakuandaliwa kuwa watu wanaofahamu, bali wameandaliwa kuwa watu wanaokariri… |
HUYU NDIYE MTANZANIA ALIYEUWAWA NA VIBAKA JUZI ALHAMISI NCHINI MAREKANI Posted: 06 Jul 2013 08:28 AM PDT POLISI wametambua mwili wa mwanafunzi wa Howard University aliyeuawa kwenye jaribio la uhalifu Alhamisi usiku.
Omar Sykes, 22, na mwanafunzi mwenzake walikuwa wanatembea maeneo ya 700 block of Fairmont Street NW kabla ya saa 5.30 usiku walipofuatwa na watu wawili. Polisi wanaamini kulikuwa na jaribio la uhalifu ila yalitokea mabishano kabla mmoja ya wale watu kutoa bastola na kumuua Sykes. Alifikia mauti kwenye hospitali ya maeneo ya jirani. “Tunadhani ilikuwa jambo la ghafla na hatuna uhakika kama wanafunzi hao waliibiwa mali yoyote” alisema Kapteni Bob Alder wa kituo cha polisi DC alipohojiwa na News4. Mwanafunzi mwingine alipigwa na kitako cha bastola na kujeruhiwa kichwani ingawa hana majeraha makubwa. “Wanafunzi wengi wamepatwa na hofu ya kutoka na kutembea usiku kwani hali hii inaogopesha sana,” alisema mwanafunzi mmoja alipohojiwa na Megan McGrath kutoka News4. Maelezo kamili kuhusu watuhumiwa bado hayajapatikana. Kulikuwa na matukio mengi ya kujumuisha watu wakati wa tukio hivyo polisi wanatumaini kuwa haitawia vigumu kwa wahalifu hao kujulikana. Sykes alipenda uandishi na mara ya mwisho aliandika makala kwenye mtandao unaoitwa Our Black Pages mnamo tarehe 11 Juni. Wasifa wake unaonesha kwamba alikuwa anasomea Marketing na Public Relations. Mkesha wa sala kwa ajili ya marehemu utafanyika shuleni kwao Jumamosi kuanzia saa 1 usiku. Howard University imetoa maelezo yafuatayo kuhusiana na kifo cha Alhamisi: “Tuna huzuni kubwa kufuatia kifo cha mmoja wa wanafunzi wetu kilichotokea nje ya shule. Mwanafunzi mwingine alijeruhiwa kwenye tukio hilo na anaendelea na matibabu…. Polisi wa Howard University wanashirikiana polisi wa mji ili kupeleleza tukio hili hatari. Tunawapa pole familia, shule na wale wote walioguswa na tukio hili kwa namna moja au nyingine. Huduma ya ushauri nasaha itapatikana masaa 24 kwa wanafunzi wote watakaohitaji msaada katika kipindi hiki kigumu.” |
MASKINI:BASI LA SUMMRY LAUA WATU 9 NA KUJERUHI 53 Posted: 06 Jul 2013 08:23 AM PDT Basi la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni na kuua watu tisa na kujeruhi wengine hamsini na tatu. Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa wametoka Mbeya. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu kwa jina la Ntungu Alisema basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko, dereva wake alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza kutoka na kukimbilia kusikojulikana ... Mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole wahanga wa ajali hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo uanze. Source:Mpekuzi |
WAKAZI AMJIBU TID"BAADA YA KUMDISS ATAIMBA WIMBO GANI BBA"SOMA HAPA ALICHOSEMA Posted: 06 Jul 2013 08:19 AM PDT Rapper Webiro Wassira aka Wakazi amefunguka kupitia Bongo5 kuwa kitendo cha TID kumdiss kuwa haoni wimbo atakoutumbuiza kesho kwenye eviction show ya Big Brother Africa The Chase kinaonesha kuwa staa huyo wa ‘Kiuno’ hajui anachokiongea.
Jana kupitia Twitter, TID aliandika: Wakazi ataimba wimbo gani, anaenda kuonyesha kofia zake za marekani#mzee kasema#radarworththisshit#watuwabaya#msiwemaf**a. Akijibu kuhusu kile anachoweza kujibu baada ya tweet hiyo ya TID, Wakazi amesema: Sasa ntamjibu nini, anaongea vitu asivyovifahamu, yeye hapo akimuona Wakazi anaona kofia za Marekani sasa mtu kama huyo utaongea naye!!” “The greatest ignorance ya mtu ni pale anapoamua kudiss kitu ambacho hakijui au hajakifahamu bado vizuri , mtu kama huyo huwezi kuanza kubishana naye, na yeye ananiona mimi Mmarekani, wakati mimi ni Mtanzania, angekaa miaka mitatu Ulaya au Marekani angejiona na yeye ni mtu wa huko kwa jinsi upeo wake ulivyo.” |
MJUKUU WA MANDELA AFICHUA 'UCHAFU' WA FAMILIA YAO Posted: 06 Jul 2013 01:28 AM PDT Mjukuu wa mzee Mandela...Mandla Mandela alipokuwa akiongea na vyombo vya habari kijijini Mvezo jana. Chuki miongoni mwa familia ya Nelson Mandela imeongezeka na kuchukua sura mpya jana pale mjukuu wa kiume na mrithi Mandla kuwatuhumu ndugu zake kwa uzinzi na kuukamua umaarufu wa kiongozi huyo anayeheshimika wa kupinga ubaguzi wa rangi. Maoni yake hayo yamekuja wakati mabaki ya miili ya watoto watatu wa kiongozi huyo mwenye miaka 94 ikizikwa upya kwenye eneo la makaburi ya awali kufuatia amri ya mahakama kuirejesha baada ya Mandla kuwa amehamisha miili hiyo. Katika mkutano na vyombo vya habari uliorushwa moja kwa moja kwenye televisheni ambao umewafadhaisha wananchi wa Afrika Kusini, Mandla alithibitisha tetesi kwamba mtoto wake mdogo wa kiume, Zanethemba, alikuwa ni mtoto wa uhusiano haramu kati ya kaka yake Mbuso na mke wa Mandla ambaye sasa wametengana, Anais Grimaud. Huku Mandela akiwa kwenye mashine ya kupumulia hospitalini mjini Pretoria, chuki hiyo inayoongezeka imeiduwaza na kuishitua Afrika Kusini kwa uwiano sawa. "Mbuso alimpa ujauzito mke wangu," alisema Mandla huko Mvezo, kijiji kilichoko Eastern Cape kilomita 700 (maili 450) kusini mwa Johannesburg ambako Mandela alizaliwa na mahali ambako Mandla anatumikia akiwa kama chifu rasmi wa ukoo huo. Mandla, mwenye miaka 39, kwanza aliibua maswali kuhusu ubaba wa mtoto wake mwaka jana wakati alipotengana na Grimaud anayezungumza Kifaransa, ambaye tangu wakati huo alirejea kwao katika kisiwa cha Reunion kilichoko kwenye Bahari ya Hindi. Pia alibainisha wakati huo kwamba hakuwa na uwezo wa kupata watoto. Juhudi zake kuipata familia hiyo kujibu maswali hayo ya ubaba wa Zanethemba yaligonga mwamba kwa lengo la kuhifadhi mfanano wa umoja katika familia hiyo maarufu kabisa nchini Afrika Kusini," alisema Mandla. "Jambo hili halikuwahi kabisa kujadiliwa na wanaoitwa ndugu wa familia hiyo ambao wanasema kwamba wanataka kuhakikisha kwamba kuna utulivu katika familia hii," alisema, akiwapa changamoto waandishi wa habari kufanya vipimo vya DNA kuthibitisha madai yake hayo. "Ukweli uko pale. Unaweza kwenda na kubaini, fanya vipimo vya muhimu vinavyohitajika," alisema. Kaka yake Mbuso amekana kuwa baba wa mtoto huyo. Vyombo vya habari vimepachika vichwa vya habari 'Mandela vs Mandela' kwenye kurasa zao za mbele na tahariri zimesikitikia ukatili wa mgawanyiko wa chuki ndani ya familia hiyo ya mtu aliyetikisa dunia nzima kama mfano wa mapatano kati ya pande zinazopingana. |
PICHA:DIAMOND PLATNUMZ AKIPIMA OIL KWA SHABIKI WAKE Posted: 06 Jul 2013 01:22 AM PDT |
TID "WAKAZI ATAIMBA NYIMBO GANI BIG BROTHER AU ANAENDA KUONYESHA SWAGA ZA MAREKANI Posted: 06 Jul 2013 01:10 AM PDT Week hii kwenye show ya Big Brother Eviction Amechaguliwa Mtanzania anayejulikana kwa jina la Wakazi kubarudisha jumapili hii, wengi hawamjui jamaa huyu , pia hana single ambayo watanzania wanaijua ..amekuwa akiishi Marekani muda mrefu na nyimbo zake nyingi zile za mix tapes...Sasa TID kaibuka na kusema haya hapa chini .....
|
WAZAZI WAUA MTOTO WAKIGOMBANIA CD YA MSANII "DIAMOND" Posted: 06 Jul 2013 01:01 AM PDT Vilio na simanzi vilitanda Jumatano iliyopita Mwananyamala Kisiwani, jijini Dar kufuatia mtoto wa mwaka mmoja, Rahim Rajab kufariki dunia kwa kuangukiwa na watu watatu, akiwemo baba yake mzazi, Rajab Said..Tukio la watu hao kumwangukia mtoto huyo lilitokea Jumatatu iliyopita na lilisababishwa na ugomvi mkubwa wa CD yenye nyimbo za mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ulioibuka ndani ya chumba cha kulala kati ya mama wa marehemu na mpangaji mwenzake aitwaye Aisha. Akizungumza kwa machungu kuelezea tukio hilo, mama mzazi wa marehemu Rahim, Habiba Ally alikiri kuwa kisa cha kifo cha mwanaye ni CD tu.Akasema: " Kwa kweli hakuna kingine zaidi ya CD, naamini hivyo kwa kuwa mimi sikuwa na ugomvi wowote na Aisha. Tulikuwa tunaishi kawaida tu ukiacha mikwaruzo ya hapa na pale.” Akaongeza: Jumamosi iliyopita, Aisha alikuja ndani kwangu na CD zake tatu, ya Diamond, Kingwendu na ya Coast Modern Taarab. Alipomaliza kuangalia aliziacha, akaondoka zake. “Jumapili mimi nikaenda nazo kwa mama zote tatu kwa ajili ya kuziangalia, tulipomaliza na mimi niliziacha huko. “Jumatatu usiku Aisha akaja kunidai, nikamwambia zipo kwa mama. Kwa kuwa anapajua anapoishi mama, si mbali akaenda kuzichukua zote tatu. Ajabu aliporudi tu, akaja tena kwangu na kusema hajapewa CD ya Diamond kitu ambacho si kweli na ndipo ulipozuka ugomvi wote huo hadi kusababisha kifo cha mwanangu.” Akizungumza msibani juzi, bibi wa marehemu, Jamima Hassan alisema siku ya tukio alipigiwa simu na mkwe wake (baba wa marehemu) akamwambia kuna ugomvi nyumbani kwake unaohusu CD kati ya mkewe na mpangaji mwenzake ambapo bibi huyo aliamua kwenda kutatua ugomvi huo. “Niliondoka muda huohuo kwani huyo Aisha alitoka kwangu kuchukua CD zake muda mfupi tu, sasa nilijiuliza ni CD gani wanazogombania? “Nilipofika nilikuta ugomvi umepamba moto, baba wa mtoto na mume wa Aisha aitwaye Shaban Sangali walikuwa wameungana kumtoa nje ya chumba Aisha bila mafanikio. “Wakati naingia, Aisha alikuwa akitukana matusi mazito na tulipojitahidi kumtoa nje alitusukuma kwa nguvu. Ndipo yeye, mume wake na baba wa mtoto waliwaangukia watoto waliokuwa wamelala kitandani,” alisema bibi huyo. Akaendelea: Tulipowaangalia watoto ambao ni mapacha, hali zao zilikuwa mbaya, tukaamua kwenda kwa mjumbe wa mtaa kuripoti, akatupa barua, tukaenda Kituo cha Polisi Mwinyijuma, pale wakatupa PF3 ya kuwapeleka Hospitali ya Mwananyamala ambako walilazwa kwa matibabu. Bibi huyo alisema siku iliyofuata, Rahim alifariki dunia, ikabidi waende Polisi Oysterbay ambapo walifungua shitaka lenye faili kwa kumbukumbu No. OB/RB/1150/2013 MAUAJI. Watuhumiwa katika RB hiyo ni Aisha na mumewe, Sangali ambao walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi. Majirani waliozungumza na mwandishi wetu walisema wakati ugomvi kati ya Aisha na Habiba unatookea, mume wa Habiba alikuwa anarudi kutoka kazini, akakutana na kimbembe hicho. Walisema aliingilia kati kuamua bila mafanikio. Wakati huo mume wa Aisha alikuwa chumbani kwake na amefungulia muziki wa redio kwa sauti ya juu hivyo hakujua nini kinaendelea kwenye chumba cha mpangaji mwenzake. Ikaelezwa kuwa, kuna watu walikwenda kumgongea na kumwambia mkewe anapigwa na mume wa Habiba kwa kushirikiana na mkewe. Ilibidi mwanaume huyo atoke mbio hadi chumbani kwenye ugomvi ambako alikuta baba wa marehemu akijitahidi kuwaamulia wawili hao bila mafanikio. Habari zinasema mwanaume huyo aliingilia kati kuongeza nguvu lakini katika hali ya kuwalemea, Aisha aliwasukuma wote na kisha wao kuwaangukia watoto hao mapacha waliokuwa wamelala kwenye kitanda kimoja. Katika hali ya kusikitisha, marehemu amemuacha pacha mwenzake aitwaye Rahima Rajab ambaye ni kulwa. Wengi wanaamini kuwa maisha ya Rahima yangekuwa ya furaha zaidi kama Rahimu angekuwepo na kwamba itamsononesha sana akikua na kusikia mwenzake alifariki dunia kwa ugomvi wa mama yake na mpangaji mwenzao kisa ni CD ya nyimbo za mwanamuziki. GPL |
USHAURI KWA MABINTI AMBAO HAWAJAOLEWA BADO Posted: 05 Jul 2013 09:33 PM PDT Ndoto ya wasichana wengi ni siku moja kuja kuolewa. Mungu ametuahidi baraka zake nyingi ikiwamo baraka ya ndoa hivyo haupaswi kukaa na kusubiri hadi upate mchumba ndio uanze maandalizi yakupasa kuanza kujiandaa kuwa mke. Mungu amekuandalia mume mwema hivyo unapaswa kujiandaa mapema ili ndoa yako iwe bora.
1. Omba kwa ajili ya mume wako Wasichana wengi wanaomba ili waweze kuolewa, hiyo ni sawa kabisa lakini jambo la kwanza kabisa inabidi uombe kwa ajili ya mume wako ambaye Mungu anaenda kukupatia. Anza mapema kuomba kwa ajili ya mume ambaye Mungu anaenda kukupatia. Omba kwa ajili ya maisha yake ya kiroho, uwezo wake kusimamia na kuitunza familia na maisha yake kwa ujumla. Usisubiri hadi uolewe ndipo uanze kuombea umoja katika ndoa yenu, anza sasa na pia kumbuka kuomba kwa ajili yako ili uwe mke mwema. 2. Jiandae Familia yako unayoishi nayo ndio hasa sehemu yako ya kujiandaa kuishi na mume wako. Unapaswa kujifunza kuanzia sasa kuishi vizuri na watu wa familia yako, hutaweza kuishi vizuri na mume wako kama sasa unashindwa kuishi vizuri na ndugu na jamaa zako. Waonyeshe upendo, huruma na kujali na kwa kufanya hivi utakuwa umejijengea tabia ambayo utakuwa nayo kwa watu wote na mumeo pia. Unaposhindwa kukaa vizuri na watu wako wa karibu kama familia vivyo hivyo hautaweza kukaa vizuri na mume wako, ndoa haimbadilishi mtu bali inakuonyesha uhalisia wako. Jinsi ulivyo unapokuwa nyumbani kwenu ndivyo ulivyo. 3. Omba uweze kutambua hila za shetani Sababu ya uhitaji wa kuolewa ulionao inaweza kuwa ngumu kugundua kama mtu anayetaka kukuoa hajatoka kwa Mungu. Sio kila nayesema Bwana asifiwe ni kweli ameokoka maana wengine wapo ili wapate wake wazuri, ndio maana ni muhimu sana kuomba uongozi wa Mungu ili uweze kujua nani hasa ametoka kwa Mungu. Pia inawezekana akawa ameokoka lakini akawa sio mume ambaye Mungu amekuandalia hivyo ni muhimu sana kuomba kwa ajili ya uongozi wa Mungu katika muda huu wa muhimu katika maisha yako. 4. Tulia mbele za Mungu Filipi 4:6 Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru Mungu analifahamu hitaji lako na muhimu zaidi anakujua na kukupenda, hajakusahau maana hawezi kukusahau na anakuwazia yaliyo mema. Ebrania 13:5b kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, “Sita kupungukia kamwe wala sitakuacha” Yeremia 29:11 Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,’’ asema BWANA. “Ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru,ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo”. Usikate tamaa, mume wako yupo na atakuja kwa wakati wa Bwana. Endelea kumwamini Mungu. Ubarikiwe! Source:Jamii forums |
RAIS KIKWETE KUWA REFA MECHI YA WABUNGE WA SIMBA NA YANGA Posted: 05 Jul 2013 09:25 PM PDT Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amekubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalo fanyika Jumapili hii, Julai 7 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Aidha, Rais atahutubia katika tamasha na pia atakuwa refa wa mechi za wabunge wa Yanga na Simba.
|
You are subscribed to email updates from Udaku Specially
To stop receiving these emails, you may unsubscribe now. |
Email delivery powered by Google |
Google Inc., 20 West Kinzie, Chicago IL USA 60610 |
Udaku Specially |
MBOWE AFANYA MAZUNGUMZO NA MAAFISA WA IKULU YA MAREKANI Posted: 07 Jul 2013 07:48 AM PDT Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye alialikwa kushiriki dhifa ya Kitaifa Ikulu wakati wa ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani alifanya jambo kubwa muhimu kwa mustakabali wa Demokrasia hapa nchini.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Kiongozi Rasmi wa upinzani bungeni alipata fursa adhimu ya kufanya mazungumzo ya Faragha na maafisa wa Ikulu ya Marekani walioambatana na Rais Barack Obama. Mpaka sasa kilichozungumzwa na Kiongozi huyo anayeongoza chama kinachopendwa na watanzania wengi zaidi hakijawekwa bayana ingawa wachunguzi wa mambo wanasema yalikuwa mazungumzo nyeti na muhimu kwa mustakabali wa demokrasia na amani ya Tanzania. Taarifa zaidi zinasema Kiongozi huyo wa Upinzani nchini alialikwa na Ikulu kwa shinikizo kubwa kutoka ubalozi wa Marekani kutokana na Taifa hilo kutambua kazi kubwa inayofanywa na wabunge wa CHADEMA ndani ya bunge la Tanzania. |
UWOYA, LUCY KOMBA NDANI YA BIFU ZITO Posted: 06 Jul 2013 10:36 PM PDT MWANAFUNZI na mwalimu wake katika sanaa, Irene Uwoya na Lucy Komba wameingia katika bifu zito chanzo kikidaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumzunguka mwanafunzi wake kwa mumewe, Hamad Ndikumana ‘Katauti’. Lucy ambaye ndiye mwalimu wa Uwoya kisanaa, imedaiwa kuwa amemzunguka Uwoya kwa mumewe, Ndiku kwa kisingizio cha kucheza naye filamu iliyofahamika kwa jina la Kwa nini Nisimuoe? “Kimenuka! Lucy Komba amemhadaa Ndiku, akazuga kuigiza naye filamu moja ndipo walipozama kwenye ukaribu kwelikweli. “Mbaya zaidi filamu yenyewe wameigiza wahusika wawili tu (Lucy na Ndiku) mwanzo mwisho kule Tegeta. Sasa wewe unafikiri kuna nini hapo kama siyo mapenzi?’’ kilihoji chanzo hicho makini. Baada ya paparazi wetu kuyanasa madai hayo, Jumatano iliyopita alimtafuta Uwoya kwa njia ya simu ambapo alipopewa taarifa hizo, alionesha kushtuka na kuchanganyikiwa mumewe kuigiza filamu moja na Lucy, alikata simu kisha baadaye akampigia paparazi yeye. “Kuna wakati nilikuwa namtafuta Ndiku sijui alipo kumbe alikuwa na Lucy, sawa lakini kama Lucy ameamua kunifundisha mimi na sasa amemfundisha mume wangu sawa, tupo hapa!” Paparazi wetu alihamishia majeshi kwa kumtwangia ‘mtuhumiwa’, Lucy ambaye alitiririka kama ifuatavyo: “Nilijua Uwoya akisikia itakuwa ni balaa maana siku za nyuma niliwahi kumshutumu kutoka na mzazi mwenzangu (Patrick Mbasha) lakini mimi nipo tayari kwa lolote!” Lucy Komba ndiye aliyemuingiza Uwoya kwenye sanaa baada ya kumchezesha Filamu ya Yolanda ambayo ndiyo iliyomtambulisha vyema staa huyo kisha kuliteka soko la sinema Bongo. |
NISAIDIENI JAMANI MUME WANGU ANANITESA NAONA AIBU HATA KUTOKA NJE YA NYUMBA YANGU Posted: 06 Jul 2013 10:01 PM PDT ... Dada yangu anauzunika sana!
"Nisaidieni mwenzenu jamani, nina watoto wawili, miaka 6 na miaka 4, wote wanasoma. siku hizi mume wangu amebadilika sana, kiasi kwamba hata ada za watoto wake hatoi, hadi tugombane sana ndio anatoa ada. Mapenzi pia yamekwisha, anafanya mambo ya aibu hadharani huku watu wakiona. Kuna siku moja alikuwa na wanawake bar, amewanunulia pombe, huku wanamshikashika, dada mmoja akiwa pale bar ananifahamu akanipigia simu niende nikamuone, nikaenda nikajionea, wanavyofanya, (walikuwa wanamtomasatomasa na kunyonyana), wanamshikashika sana kila sehemu za miili yao (na kisses nyingi). Ndipo nikapata fahamu' "ndiyo maana akirudi nyumbani anakuwa hana hamu na mimi" Basi siku hiyo nilipata ujasiri nikamfuata pale pale, nikawambia jamani, tafuteni nyumba ya wageni, msitie aibu hapa, wale wadada walikimbia, mume wangu nae akaanza kunikimbiza ili anipige huku kashika chupa ya bia mkononi, nikajificha mahali, nilipoona amerudi bar, nikarudi nyumbani nikachukuwa nguo nikaondoka, nikakaa kwetu mwezi mzima, badaye akaja kuomba msamaha, nilikubali nikarudi nyumbani kwa huyo mme wangu!. Kwa sasa ujinga na upuuzi ule umeanza tena, nikimweleza atulie, anakuwa mkali na kunifokea, wakati mwingine ananitukana mbele ya watoto wangu, "mimi naumia sana moyoni ndugu zanguni" Mimi sina kazi, nikiondoka tu hata watoto hatawasomeshwa tena, sasa nifanyaje jamani. Niliwahi kufungua biashara ya kutengeneza nyele (salon), akanifanyia fujo na kunifanya nifunge, hataki nifanye chochote kile, Naomba ushauri mwenzenu, sijielewi kabisa nifanye nini, ukizingatia mtaa mzima tunakoishi wameishajua tabia yake mme wangu, naona hata aibu kutoka ndani ya nyumba." "by Happy' she is unhappy" *Ndugu wanaJF tumsaidieni ndugu yetu Furaha hanaraha kwa sasa. *Yamkini kuna wadau wako kwenye mazingira kama haya ya Happy. " Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku, kwa watu wanaoteseka kama ndugu yetu alivyosimulia tatizo linalomkabili, ili tuweza kukidhi mahitajio yake na watu wenye matatizo kama haya." "SOMA , CHANGIA KWA KUTOA HOJA ZA KUSAIDIA NDUGU YETU NA JAMII KWA UJUMLA." Karibu wote... Source:Jamii forums |
MOYO WA MANDELA ULISMAMA KWA DAKIKA 40 Posted: 06 Jul 2013 09:45 PM PDT Johannesburg. Kuharibika kwa gari la wagonjwa lililombeba Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, kulisababisha moyo wa shujaa huyo kusimama kwa dakika 40.
Hayo yalibainishwa na daktari wa moyo anayemtibu shujaa huyo wa Afrika Kusini, kwamba Juni 8, mwaka huu, wakati akipelekwa hospitali gari lililombeba lilipata hitilafu njiani na kukwama kwa muda. Daktari huyo wa moyo anayeheshimika nchini Afrika Kusini, (jina linahifadhiwa) alisema jana kuwa gari la wagonjwa lililokuwa likimpeleka Mandela hospitali liliharibika katika njiapanda ya Gauteng na kusababisha wasubiri gari lingine kwa zaidi ya dakika 45. “Moyo wake ulisimama kabisa tukiwa ndani ya gari, ikatubidi tumfufue kwa mashine (resuscitate),” alithibitisha daktari huyo bingwa. Ripoti inaeleza kuwa gari hilo la wagonjwa linalomilikiwa na jeshi, liliharibika wiki tatu zilizopita kati ya Pretoria na Johanersburg. Chombo cha habari cha Marekani, CBS kiliripoti jana kuwa moyo wa Mandela ulisimama kwa dakika kadhaa kabla gari lingine halijaletwa na kumpeleka Mandela katika hospitali ya Medi-Clinic. Wakati moyo wa Mandela uliposimama, nje kulikuwa na baridi kali kiasi cha nyuzi joto sita tu, hali ambayo inaelezwa kuwa ilichangia kuharibu zaidi mapafu ya Baba wa Taifa la Afrika Kusini. “Mke wa Mandela, Graca Machel, alikuwa amechanganyikiwa kwa dakika hizo 40, ambazo tulikuwa tukisubiri gari lingine,” kilisema chanzo hicho. Ingawa msemaji wa Rais Jacob Zuma, Mac Maharaj alisema kuwa madaktari wamethibitisha kuwa Mandela hakupata madhara makubwa kutokana na baridi hiyo, madaktari wengi wameonyesha kupingana naye. Daktari wa moyo, David Janekelow alisema, kutokana na hali yake, ucheleweshaji wa aina yeyote ile lazima ulisababisha madhara. “Unahitaji kupata matibabu ya dharura haraka iwezekanavyo. Kama mtu tayari alikuwa anafufuliwa, ucheleweshaji wa kumpeleka hospitali lazima ulete madhara,” alisema Janekelow. Daktari mwingine wa moyo, Richard Nethonde alisema, Mandela angekufa pale barabarani wakati wanasubiri gari la wagonjwa liletwe, imekuwa ni kama bahati hakufa. Wakati huohuo, gazeti la the Sunday Times limeeleza kuwa Graca, mke wake analala katika chumba kilicho pembeni ya chumba anacholala Mandela, kwa siku zote, tangu Mandela alazwe. Wakati huohuo, wakili wa mjukuu wa Mandela, Mandla Mandela, amesema atafungua mashtaka kwa baadhi ya wanafamilia ya Mandela kwa kuidanganya mahakama kuhusu hali ya shujaa huyo. Wakili huyo, Gary Jansen alisema kuwa wanafamilia hao walipeleka hati yenye maneno ya uongo mahakamani wakieleza kuwa Mandela yu mahututi, jambo ambalo limekanushwa na Rais, Jacob Zuma aliyemtembelea juzi. “Tutapeleka malalamiko ambayo yatatokana na hati ya kiapo iliyopelekwa mahakamani na wanafamilia 15 wa Mandela, kwa ajili ya kufukua miili ya watoto wa Mandela,” alisema Jansen. Wakili huyo alisema kuwa, wanafamilia hao walipeleka hati hiyo wakiitaka mahakama ichukue uamuzi wa haraka kwani afya ya Mandela ni mbaya, jambo ambalo ni la uzushi. “Lazima tufanye uchunguzi wa kutosha kwa sababu mwanasheria wa familia hiyo, ametumia hati ya kiapo vibaya” alisema Jansen. Wakati hayo yakiendelea, wananchi wengi Afrika Kusini wanaendelea kukusanyika katika viwanja vilivyopo karibu na Hospitali alikolazwa Rais Mandela kumuombea ili apate nafuu mapema. Habari kutoka ndani ya familia ya Mandela zinaeleza kuwa huenda mgogoro mkubwa zaidi ukaibuka endapo Mandla atatimiza azima yake ya kufungua kesi nyingine |
SURUALI ZA KUBANA KWA MWANAUME NI HATARI Posted: 06 Jul 2013 09:39 PM PDT Dk Vincent Kafuuza wa Kituo cha Friends Polyclinic & Ambulance Service alisema siyo tu kuhusu suruali za kubana, lakini nguo zozote za kubana siyo nzuri kuwa mavazi ya kila siku. Alieleza kuwa mwili unahitaji kupumua, hali ambayo hufanyika kupitia kutoka jasho kwenye vinyweleo kwenye ngozi na jasho linatakiwa kukauka lenyewe taratibu. Dk Kafuuza alisema ikiwa mtu amevaa jinzi ya kubana au nguo ya ndani ya kubana, jasho litagandana kwenye vinyweleo vya ngozi na wakati mwingine inaweza kusababisha magonjwa ya ngozi kama vile ‘fangasi’, maumivu ya mwili na vipele katika mapaja na sehemu zingine za siri. “Wanaume ambao wanavaa suruali za kubana wana hatari ya kupunguza kiwango cha mbegu za uzazi. Na wakati mwingine zinaweza kupungua kwa kiwango kikubwa na kumfanya mwanamume ashindwe kumpa ujauzito mwanamke,” alisema Dk Kafuuza. Dk Kafuuza alisema suruali za kubana zina kawaida ya kusukuma ndani sehemu zinazotunza mbegu za uzazi za mwanamume, hali inayosababisha matatizo kama vile uvimbe na ngozi kubabuka. Nguo za ndani za kubana zinazuia kukuwa kwa mbegu za uzazi. Wakati joto la kawaida la mwili ni sentigredi 37, mfuko wa mbegu za uzazi wa mwanamume unahitaji kiwango cha joto kati ya sentigredi 35.5 na 36 ili kufanya kazi katika hali ya kawaida. Dk Charles Kiggundu ambaye ni Mshauri wa Hospitali ya Mulago na Chuo Kikuu cha Afya cha Makerere, alisema joto la mbegu za uzazi za mwanamume linaweza kuongezeka ikiwa mfuko unaozishika utafifia ndani ya mwili kwa muda mrefu, kwa mfano kama mwanamume amevaa nguo ya ndani ya kubana. Kwa mujibu wa Dk Lawrence Kazibwe wa Hospitali ya Mulago, alisema mbegu za uzazi za mwanamume ziko kwenye mfuko maalumu kwa sababu zinahitaji kuwa zimepoa zaidi ya maeneo mengine ya mwili, ili ziwe kwenye mazingira tulivu. Alisema lengo hilo linaweza kuvurugika iwapo mwanamume atavaa suruali ya kubana ambayo itazifanya mbegu za uzazi zikose mawasiliano ya kawaida na sehemu nyingine ya mwili, ambayo ni kupata joto linalotakiwa. “Baadhi ya wanaume wanafikiri kusafirisha mbegu za uzazi pekee kwa mwanamke ndiko kunawezesha mwanamke kupata ujauzito, lakini urutubishaji hauwezi kutokea katika sehemu za kikeni, kwa kuwa mbegu za uzazi lazima zipite kwenye mrija unaotakiwa kukutana na mayai mengine. Hivyo basi mbegu za uzazi zinahitaji kuwa na nguvu na nyingi ili ziweze kuyafikia mayai ya kikeni na kuwezesha kupata ujauzito,” alifafanua Kiggundu. Kiggundu alisema; “Hebu fikiria katika hali ambayo mbegu za uzazi ni chache na dhaifu! Hii ina maana hazitaweza kurutubisha mayai ya kike. Hivyo unaweza kutoa mbegu za uzazi wakati wa tendo la ndoa, lakini hakuna ubebaji mimba utakaofanyika.” Mbegu za uzazi ambazo ni dhaifu, kama vile zile ambazo hazina mkia, zenye mkia mkubwa, zenye mkia mdogo, zilizopinda kichwani na zile zenye mikia miwili, haziwezi kupenye kwenye mrija wa kwenda kwenye mayai ya uzazi ya kike. Imeandikwa na Noor Shija kwa msaada wa mtandao. « Previous Page |
Udaku Specially |
Posted: 08 Jul 2013 04:49 AM PDT MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, amelowa mvua ya matusi baada ya kumfananisha mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na aliyekuwa mwanamuziki mkubwa duniani, marehemu Michael Jackson.
Wikiendi iliyopita, Uwoya aliandika kwenye ukurasa wake katika mtandao wa Instagram kuwa msanii huyo anayefanya vizuri katika Bongo Fleva ndiye staa atakayemrithi mkali huyo wa Pop, maandishi ambayo yalizua matusi hayo ya nguoni. Baadhi ya mashabiki wa mastaa hao walitoa maoni kuwa jambo hilo ni sawa na kufananisha vitu ambavyo havina uwiano hasa ukizingatia Michael Jackson alishafariki dunia Juni 25, 2009. “Sasa hiyo ni akili gani ya ki…(tusi) kumfananisha mtu aliyeko hai na marehemu?” alihoji Mishish, mmoja wa mashabiki wa Uwoya katika mtandao wa Facebook baada ya ishu hiyo kuwa gumzo mitandaoni. “Kweli wewe Irene (Uwoya) ni …(tusi) au kwa sababu Diamond amesha…(tusi) ndiyo maana unamsifia kiasi hicho,” aliandika shabiki mwingine kwenye Twitter na kupisha wengine kuendelea kumporomoshea Uwoya matusi ya nguoni |
PREZZO NI MTUNDU SANA TUKIWA WOTE.....HATA AKINIUDHI SIWEZI KUKASIRIKA "DIVA" Posted: 08 Jul 2013 04:46 AM PDT Muda mfupi uliopita mtangazaji wa ‘Ala za Roho’ ya Clouds FM Diva Loveness Love ambaye sasa anatumia “divathebawse” katika akaunti yake ya Instagram, ameweka picha mpya akiwa na Rapcellency Jackson makini aka Prezzo kutoka Kenya waliyopiga jana (July 7).
Picha hiyo ambayo inawaonesha wawili hao wakiwa “0 distance” ilikuwa na caption inayosomeka hivi, “Nothing Than Happiness… Prez is such a Nice guy. Hata Akiniudhi Sihesabu makosa yake. May you Live Long Pleaseeee……… Good hearted, My hero, My Mentor… A Person I can count to when I need to be happy… No one is Perfect yes but I love his flaws and All…. Bless you always’ . I Pray you live Long… I Pray for you Always” Picha nyingine iliwaonesha Prezzo na Diva wakikumbatiana na kusindikizwa na caption “Last Night at escape1… I was nothing than happy. With Prezzo”. |
WAPENZI WANASWA AIRPORT DAR KWA DAWA ZA KULEVYA-MSICHANA NI MFANYAKAZI WA NDEGE Posted: 08 Jul 2013 04:38 AM PDT Jeshi la Polisi Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, linawashikiliwa watu wawili, wanaodaiwa kuwa ni mtu na mpenzi wake kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin kilo mbili zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi Sh90 milioni...Msichana inasemekana ni mfanyakazi wa shirika moja kubwa la ndege hapa Tanzania..
Mkuu wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa aliliambia gazeti hili jana kuwa watuhumiwa hao ambao mmoja ni mwanamke walikamatwa juzi saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). Alisema watuhumiwa walikuwa wakisafiri kwenda Mji wa Bangkok Thailand kupitia Addis Ababa, Ethiopia ambapo walikata tiketi ya ndege la shirika hilo. “Walipoanza kufanya ukaguzi watuhumiwa hawa walijichomeka katikati ya wenzao ndipo tulipowanasa na dawa hizo ambazo walizificha kwenye mabegi yao katikati ya nguo,” alisema Nzowa. Alisema kuwa watuhumiwa hao waligawana dawa hizo kwani walipofanyiwa upekuzi na polisi walikutwa kila mtu akiwa na kilo moja. Source:Mwananchi |
KUFIKA KILELENI KWA MWANAMKE NDIO KUKOJE? Posted: 08 Jul 2013 01:16 AM PDT "Mimi ni mwanamke wa miaka 30 tatizo kubwa linalonitatiza ni kuwa wakati wa kungonoka na mr. Nitajuaje kama nami pia nimekojoa??ebu nijue shosti coz huwa napata mtihani mkubwa sana sijui kama nishawahi "kukojoa" au la!
Kuna siku nyingine huwa napata raha up to the maximum yaani hadi nalia machozi kabisa sasa sijui huwa huko ndio "nakojoa" kwenyewe au ni mautamu tu? Please i need the tips za kuniwezesha kutambua "kukojoa"thanx mumy! yours raht!" |
Posted: 08 Jul 2013 12:27 AM PDT Ripoti kutoka Afrika Kusini zinasema wanawake wawili wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa OR Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Rand million 42.6 kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa katika mpaka wowote wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa madawa (crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 ya Tanzania. Muller aliendelea kusema baada ya mizigo yao kuanza kukaguliwa ndipo timu ya maafisa uhamiaji iligundua kilo karibia 150 za madawa katika mizigo yao, kiasi ambacho ndio kikubwa kuwahi kukamatwa kama mzigo mmoja katika mpaka wowote wa Africa Kusini. “When searching their luggage which was six large bags of black holdall bags, the customs team found just less than 150 kilos of crystal meth that is what we also call Tik in South Africa. Those drugs are valued at R42.6 million which makes it the single largest seizure by the SARS customs team at any border in South Africa.” Alisema Muller. Wanawake hao ambao hawakutajwa majina wala uraia wameshikiliwa na polisi nchini Afrika Kusini. |
UMAARUFU WA WASANII WENGI WA KIKE UNATOKANA NA SKENDO ZA PICHA CHAFU Posted: 07 Jul 2013 11:07 PM PDT NCHI za wenzetu staa kupiga picha za utupu si kitu kigeni lakini Tanzania sheria na maadili ya Mtanzania hayaruhusu kufanya hivyo.
Pamoja na sheria kutoruhusu, wasanii wetu hasa wa kike wamekuwa wakihaha usiku na mchana kuusaka umaarufu wa kujulikana kwa jamii kwa njia za panya,.... Wengi wao wamepoteza sifa za uwajibikaji na badala yake wamejikita katika Skendo chafu ili jamii iwajue... Hali hii imewafanya wasanii wengi wa kike wawe na umaarufu wa skendo chafu.... Miongoni mwa skendo hizo ni: 1.Kupiga picha za uchi Hili ni kundi la wasanii chipukizi wanaosaka umaarufu kwa gharama yoyote....Ni skendo ambayo huwachafua sana, lakini pia ni skendo ambayo huwainua na kuwafanya wajulikane.... Mfano halisi wa wasanii wa kundi hili ni Rayuu,Agness Masogange, Lulu Michael,Pendo wa Maisha plus 2.Kutumia madawa ya kulevya Hili ni kundi la wasanii ambao hutumia madawa ya kulevya na kisha hukimbilia katika vyombo vya habari na kujitangaza kwamba ni wavuta bangi na kwamba "hivi sasa wameacha"3.Kuvaa nusu uchi Hili ni kundi lenye wasanii wengi sana.Hawa ni wasanii wenye imani ya kuwa mastaa kwa kuvaa nusu uchi huku mapaja na matiti yao yakiwa wazi ...Wahanga wa kundi hili ni wasanii wa kike ambao sote tunawajua. 4.Kutovaa chupi na kujipitisha mbele ya kamera Hili ni kundi la wasanii wachache ambao umaarufu wao umekwisha.Ili kujiinua tena kwa jamii, wasanii hawa hutumia skendo nzito kama hizi ambazo huifanya jamii istuke..!...Mfano halisi ni Nakaaya.Source:Mpekuzi |
PICHA ZA MPAMBANO WA NGUMI WA HALIMA MDEE NA JACK WOLPER Posted: 07 Jul 2013 10:58 PM PDT |
MWANAMUZIKI WAKAZI AMPROVE WRONG TID-APAGAWISHA SHOW YA BIG BROTHER VILIVYO Posted: 07 Jul 2013 10:46 PM PDT Baada ya Mtanzania Wakazi kuchaguliwa kuimba katika show ya Big Brother huko South Africa , Week nzima iliyopita kulikuwa na Mijadala kuwa Wakazi Ataimba nini kwa kuwa hana Hit Song iliyotamba Tanzania .."Hii Ilipelekea mpaka TID akaandika status kumzihaki ...kwa kusema Wakazi ataimba nini" Lakini Jana kijana huku amewaprove wrong wote waliokuwa wanamzihaki....baada ya kutoa show ya nguvu.... Soma hapa website ya Big Brother walivyoandika kuhusu kijana huyo wa Kitanzania .. After a whole week of waiting for the young talented Tanzanian “Wakazi” to perform on the live eviction eviction show, he has finally done his thing on the Big Brother Africa stage. He has began by performing a great jam titled “Weekend/Touch” which was a combination of both English and Kiswahili ryhmes with a lot of energy which totally left all the Big Brother Africa fans crazy and while he was putting out his rymes, all the sexy girls were tirelessly cheering the sexy Tanzanian rapper. Later after Fatima and Hakeem had been evicted from the Big Brother house, Wakazi stepped again on the Big Brother Africa stage with another killer jam titled Sexy Lady. He completely killed it off with this one because even the evicted Fatima could not hold it anymore, she stood and started dancing to the tune of the song. |
MASKINI:MWANAFUNZI AJILIPUA NA MAFUTA YA PETROL Posted: 07 Jul 2013 10:32 PM PDT MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi (VETA), mkoani Dodoma, Taliki Juma (22), amefariki dunia baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli. Mbali na mwanafunzi huyo kufariki, watu wengine wanane waliokuwa karibu na moto huo nao walijeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma na kusainiwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, tukio hilo lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka, Kata ya Nzughuni. Kamanda Misime alisema, katika tukio hilo marehemu alinunua mafuta ya petroli lita tano katika kituo cha mafuta cha Nanenane na kisha kujilipua. “Juma ambaye ni mwanafunzi wa fani ya ufundi wa magari, alimwaga petroli hiyo ndani ya saluni ya Irene Mapunda na kujilipua. “Watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo. “Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili,” ilieleza taarifa hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliojeruhiwa ni Mugina Hessein (32), Benson Mushi (11) Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim (20),Ester Silau (30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21). Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) na tathimini ya hasara iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika. |
FAMILIA YA MANDELA WASHIKANA UGONI SOUTH AFRICA Posted: 07 Jul 2013 10:22 PM PDT *Mandla amtuhumu Mbuso kuzaa na mkewe
CHIFU Zwelivelile Mandlesizwe Dilubhunga ‘Mandla’ Mandela (39), ambaye ni mjukuu mkubwa wa kiume wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amemtuhumu mdogo wake, Mbuso Mandela (22) kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe. Tuhuma hizo nzito ndani ya familia ya Mandela, zimeibuliwa na Mandla kwa kumtaja jina moja kwa moja Mbuso kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wake wa pili, Anais Grimaud, ambaye alimpa ujauzito. Mandla na Mbuso ni watoto wa Marehemu Makgatho Mandela ambaye ni mtoto wa kiume wa Mandela kwa mkewe wa kwanza, Marehemu Evelyne Maso. Watu walio karibu na familia ya Mandela, wamepata kukaririwa na vyombo vya habari vya nchini hapa wakieleza kuwa, Mandla amekuwa akilalamika mara nyingi kuwa mke wake ambaye wameshatalikiana, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa ndugu zake, lakini hakuwahi kumtaja kwa jina. Katika malalamiko yake hayo, Mandla alikaririwa akieleza kuwa, ndugu yake alimpa mimba mke wake na kuzaa naye mtoto mmoja jambo ambalo wanafamilia wamelifumbia macho wakati wanajua alitendewa vibaya. Alhamisi wiki iliyopita, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Mvezo, Eastern Cape, baada ya kushindwa kesi aliyokuwa amefunguliwa na shangazi yake, Makaziwe Mandela ya kuvamia eneo la makaburi usiku na kuiba mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mandela, Mandla alisema anashangazwa na watu wanaojiita wanafamilia ya Mandela kudai wanataka amani ndani ya ukoo wakati malalamiko yake hawajawahi kuyashughulikia. Katika mkutano wake huo, Mandla alisema mke wake aliyemuita ni mzuri, Anais, ambaye ni raia wa Ufaransa, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mdogo wake wa damu aliyemtaja jina kwa mara ya kwanza, kuwa ni Mbuso. Alisema kwamba, alipopata taarifa hizo, alishtuka na kuumia na alimtaja mtoto ambaye mke wake alizaa na mdogo wake Mbuso kuwa anaitwa Nkosi Qheya II Zanethemba Mandela. Mandla alisema alilazimika kuachana na mkewe huyo aliyemuoa mwaka 2010 na kwamba aliamua kumbadili jina mtoto aliyezaa na Mbuso na kumuita Nkosikazi Nobubule, kabla hajaondoka kwenye makazi ya Mandla na kurejea kwao Ufaransa. Tuhuma hizi zilizotolewa na Mandla juzi kwa mara ya kwanza, ziliripotiwa na Gazeti la Sunday Sun la Afrika Kusini mwaka jana na kuibuka tena wiki iliyopita. Taarifa hizo, zimezidi kuipa nguvu hofu ya baadhi ya watu wanaofuatilia mtafaruku wa ndani ya familia ya Mandela ambaye kwa sasa anapigania uhai akiwa hospitalini. Kwa zaidi ya wiki mbili sasa, familia ya Mandela imekuwa katika mnyukano wa kugombea uhalali wa eneo linalostahili kuwa maalumu kwa ajili ya kuzika marehemu wa familia hiyo baada ya Mandla kuhamisha mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mandela, waliokuwa wamezikwa katika nyumba yake iliyoko kijijini Qunu na kwenda kuwazika kwenye makazi yake ya kichifu ya Mzove. Mahakama Kuu ya Mthatha ya Jimbo la Eastern Cape ilimtia hatiani Mandla aliyekuwa akishitakiwa na wanafamilia 16, ambapo ilimuamuru arejeshe mabaki ya miili hiyo Qunu. Wakati hali ikiwa hivyo kwa familia yake, Mandela bado yuko mahututi hospitali mjini Pretoria na hakuna taariza zozote za mabadiliko ya afya yake. |
Udaku Specially |
NATAFUTA MWANAUME ALIYE SERIOUS KUWA MUME WANGU BAADAE Posted: 09 Jul 2013 12:32 PM PDT Natafuta mwanaume atakayekuwa mume baadae endapo tutaelewana na kupitia hatua zinazohusika. mume anapatikana popote na Mungu akiamua apatikane humu hakuna wa kupinga. hivyo linawezekana pia.
About me; 31 years old, Government Employee and Interprenership, education level First degree, mnene wa wastani na mrefu wa wastani, Man im looking for Age -30yrs and above education -Form four and above Job - employee or self employed Awe mrefu wa wastani anayependa maendeleo na aliye tayari kujishughulisha ili kuwa na maendelea.... Acha mawasiliano yako.... |
I GOT ASS AM BEAUTIFULL I KNOW HOW TO MAKE MONEY"AGNESS MASOGANGE" Posted: 09 Jul 2013 12:05 PM PDT |
MFAHAMU MWANADADA "MELLIS EDWARD" ALIYEKAMTWA NA MADAWA YA KULEVYA PAMOJA NA "AGNESS MASOGANGE Posted: 09 Jul 2013 12:10 PM PDT Inahisiwa kuwa huyu mwanamke wa pili aliyetajwa na Kamanda Nzowa kwa jina la “Melisa Edward” ni mdogo wake na Agnes ambaye katika akaunti ya facebook anayo tumia jina la (MELLIS EDWARD) , Agnes amemuweka katika orodha ya family kama ‘sister’ katika akaunti yake ya Facebook. |
KABLA AGNESS MASOGANGE HAJAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA ALIPO PICHA HII Posted: 09 Jul 2013 11:43 AM PDT |
WEMA SEPETU ANASAKWA NA POLISI BAADA YA KUMTUKANA MENEJA WA HOTELI WAKATI POMBE IKIWA UTOSINI Posted: 09 Jul 2013 06:18 AM PDT DIVA wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa hoteli hiyo, Godluck Kuyumbu. Songombingo hilo lilijiri saa tano usiku wa Jumatano iliyopita kwenye hoteli hiyo iliyopo Kawe Beach, jijini Dar.
Akizungumza na mwandishi wetu , meneja huyo alisema siku ya tukio majira ya saa nane mchana, Wema alifika kwenye mgahawa wa hoteli hiyo akiwa ameongozana na marafiki zake wapatao kumi. Meneja huyo akaendelea kusema, ilipofika saa tano usiku, Wema na marafiki zake walionekana kuzidiwa na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga kelele, kitendo kilichowakera wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo. Aliongeza kuwa mmoja wa marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake, aliyejulikana kwa jina moja la D, alichukua glasi na kuipasua chini kwa makusudi huku meneja huyo akishuhudia. Meneja akasema: Wakati wanaondoka, nilimfuata yule jamaa mpaka nje, nikamuuliza ni kwa nini amevunja glasi kwa makusudi, akanijibu kwa dharau huku akinitukana na kutishia kunipiga, akawa ananiuliza hiyo glasi ni shilingi ngapi kwani ?. Aliongeza kuwa swali lake kwa kijana huyo lilionesha kumkera sana Wema, kwani alitoka kwenye gari na kuanza kumlamba vibao visivyo na idadi meneja huyo huku akimpa maelekezo kwamba akashitaki popote na hawezi kufanywa kitu kwani yeye ana nguvu kwenye nchi hii. “Niliamua kupiga simu Kituo cha Polisi Kawe, wakaja kuangalia mazingira kisha nikaondoka nao kwenda kufungua kesi kituoni.” Faili la kesi hiyo linasomeka KW/RB5988/2013, SHAMBULIO. |
Posted: 09 Jul 2013 06:16 AM PDT MWIGIZAJI wa kike na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Baby Madaha Joseph amemshukia mwigizaji mwenzake wa kike Jack Wolper kwa kudai kuwa amekuwa akitumia vyombo vya habari kumsema na baadae kujifanya anamuomba msamaha huku hana dhamira ya kweli.
Akiongea na FC , msanii huyo amesema kuwa Jack Wolper anatumia jina lake ili apande na kuwa Maarufu (nyota ). “Mimi ni mwanamke mpigaji na ninajua ninachofanya katika maisha yangu... "Kuna wanawake hawajui misingi ya sanaa.Ni wanawake ambao wamevamia fani na kutuharibia sifa zetu kama wasanii.. "Mimi siwezi kugombana na mtu mwenye fani moja ,tena ya kubebwa . Jack hana cha kufanya akifeli kuigiza labda arudie kazi yake ya kuuza vipodozi...Atafanya nini kingine hapa mjini zaidi ya kujiuza?,”alisema Baby Madaha na kuongeza: “Jack anataka kukiki kwa kunichafulia jina langu, lakini mimi ni Star mwenye vision na najua nafanya nini katika Industry.. "Mimi ni kiongozi mtarajiwa .Nategemewa niongoze watu , sasa nikianza kugombana na watu itaniharibia ndoto zangu za kisiasa,” |
AGNESS MASOGANGE NAE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI Posted: 09 Jul 2013 05:23 AM PDT HATIMAYE wale Wanawake wawili walionaswa na madawa ya kulevya Afrika kusini wametambuliwa kuwa ni mabinti wa KITANZANIA ..
Mabinti hao wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania. Akizungumza na mwandishi wetu jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani. Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE) ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini. Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo. Jumapili iliyopita mtandao huu ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania. Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania. Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8. Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini. Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo. Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani. Pinda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania. Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya. Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani. Melezo Kwa hisani ya Nipashe. |
HATIMAYE:AMBER ROSE AND WIZ KHALIFA WAFUNGA NDO-CHECK WALICHO ANDIKA TWITTER Posted: 09 Jul 2013 12:19 AM PDT |
MASKINI:MWANAMUZIKI LAURYN HILL AANZA KUTUMIKIA KIFUNGO CHAKE JELA Posted: 09 Jul 2013 12:14 AM PDT Four months after she was sentenced to 3 months in Federal prison for tax evasion, Grammy award winning singer Lauryn Hill has turned herself in...
Lauryn Hill has just reported to federal prison in Connecticut, where she will begin her 3 month sentence for tax evasion. Officials tell TMZ ... the former Fugees singer was booked into the Federal Correctional Institution in Danbury at 11:15 AM EST. (Yesterday July 8th) We're told the FCI is a "minimum security type facility" where inmates live in "barracks type" housing. We're also told 38-year-old Hill will not be isolated in the facility -- and will be housed with the general population. |
FAMILIA YA MANDELA YAZIDI KUTIBUANA Posted: 09 Jul 2013 12:08 AM PDT *Mandla Mandela aendelea kulikoroga WAKATI mgogoro kati ya watoto wa Mandela na wajukuu ukizidi kutokota kuhusu uhalali wa uchifu wa Mandla Mandela, yeye amejibu mapigo akisema Mfalme Buyelekhaya Dalindyebo wa kabila la abaThembu ”hana akili timamu”. Hiyo inatokana na madai yaliyotolewa na mfalme huyo kwamba Mandla hakuwa chifu sahihi wa ukoo wa Madiba. Alidai kwamba hakukuwa na cheti chochote halali kilichotiwa saini wakati mandla alipotawazwa kuwa chifu mwaka 2007 – sherehe ambazo zilisimamiwa na Mandela mwenyewe. Gazeti la Mail & Guardian wiki iliyopita liliripoti kuwa uchifu wa Mandla ulilalamikiwa kabla ya Mandela kulazwa hospitalini, ikielezwa kama kweli anafaa kuendelea kuwa chofu ikizingatiwa kuwa mama na baba yake walimzaa bila kuoana. Mgogoro unaoendelea hivi sasa kati ya Manla na shangazio yake, Makaziwe Mandela, na wanafamilia wengine unaonekana kama kichocheo kwa baadhi ya wanafamilia hiyo ambao wangetaka Mandla avuliwe uchifu. Jumamosi iliyopita, Dalindyebo alisema hawezi kumheshimu mtu “ambaye haheshimu familia yake” na kusema Ndaba ambaye ni mdogo wake Mandla ndiye anastahili kuwa chifu. Lakini juzi, Mandla alijibu mapigo kupitia kwa msemaji wake, Freddy Pilusa akisema: “Tamko lililotolewa na Mfalme Dalindyebo kwamba amemuondolea Mandla madaraka yake ya kimila ni kichekesho. “Ni mchakato mrefu wa kimila kumuondoa chifu. Huwezi kuamka tu asubuhi na kuitisha mkutano wa wafuasi wako na kuchukua uamuzi mzito kama huo,” alisema Pilusa. |
AMUUZA MWANAE WA KUMZAA KWENYE FACEBOOK Posted: 08 Jul 2013 11:55 PM PDT RIYADHI, Saudi Arabia
JAMAA mmoja amemuuza mwanae wa kumzaa kutokana na matatizo ya kifedha aliyonayo. Saud bin Nasser Al Shahry, raia wa Saudia Arabia aliweka picha ya mwanae huyo wa kiume kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii ‘Facebook’ akimnadi kwa bei ya dola milioni 20. Baba huyo alidai kuwa kitendo cha kumuuza mwanae ndiyo njia pekee ya kuondokana na maisha ya kimaskini aliyokuwa nayo kutokana na madeni. Mahakama ya nchini humo ilifunga biashara yake ya kukusanya madeni isiyo rasmi aliyokuwa akiifanya ili kujikimu kimaisha, hivyo alibaki hana mbele wala nyuma hivyo kushindwa kumudu gharama za maisha. ‘Mfanyabishara’ huyo alidai aliomba Serikali imsaidie fedha, lakini ilimkatalia kwa kuwa umri wake ni zaidi ya miaka 35 ambao ni mdogo. Alisema akifanikiwa atatumia fedha hizo kumtunza mke wake na mwanae mwingine wa kike. |
BAADA YA SHULE KUFUNGULIWA JANA GIZA NENE KIDATO CHA TANO Posted: 08 Jul 2013 11:33 PM PDT Matokeo mabaya ya kidato cha nne ya mwaka 2012, yameendelea kuitikisa sekta ya elimu nchini baada ya shule kufunguliwa jana bila kutangazwa kwa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu. Kwa kawaida, wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ualimu, hutangazwa mapema ili kutoa fursa kwa wanafunzi na shule husika kufanya maandalizi ya mahitaji. Lakini tofauti na ilivyozoeleka, wanafunzi wa kidato cha sita walianza masomo yao jana huku wale wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ualimu wakiwa hawajatangazwa. Mkanganyiko huo pia unazigusa shule za sekondari za binafsi kwani baadhi zilishachukua wanafunzi wa kidato cha tano na nyingine ziliahirishwa kufunguliwa jana kutokana na kutokuwa na wanafunzi hao. Hali hiyo imewaacha njia panda baadhi ya wakuu wa shule ambao waliwaambia waandishi wetu kwa nyakati tofauti kwamba wanasubiri maelekezo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu suala hilo, huku wengine wakitishia kufunga shule hizo na kuzigeuza kuwa vyuo vya taaluma nyingine. Akitangaza matokeo mapya ya kidato cha nne Mei mwaka huu, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa aliahidi kwamba majina ya watakaojiunga na kidato cha tano yangetangazwa mapema ili wapate muda wa kujiandaa na kuripoti kwenye shule husika mapema kadri itakavyowezekana. Jana, Dk Kawambwa hakupatikana kuzungumzia suala hilo na msemaji wa Wizara hiyo, Bunyanzu Ntambi alisema suala la kutangaza majina hayo lipo kwenye ngazi za uamuzi. “Sababu hasa siwezi kujua, lakini kwa kuwa matokeo yenyewe yalichelewa kutangazwa ni rahisi hata mchakato wa kutangaza waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano uchelewe,” alisema Bunyanzu. Wakuu wa shule Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Morogoro, Thomas Chihwalo alisema: “Ninachosubiri ni maelekezo ya wizara, nini kifanyike.” Mkuu wa Sekondari ya Azania, Dar es Salaam, Benard Ngoyaye alipoulizwa alisema: “Nenda kwa Ofisa Elimu wa Wilaya, yeye anafahamu kwa nini majina yamechelewa kufika wakati walikwishachaguliwa.” Mkuu wa Shule ya Sekondari Arusha, Christopher Malamusha alisema walitarajia wizara ingetangaza majina hayo mapema lakini hadi jana walikuwa hawajapokea taarifa zozote. Mkuu wa Sekondari ya Tambaza aliyejitambulisha kwa jina moja, Zuberi naye alisema wanasubiri maelekezo ya Ofisa Elimu Wilaya ya Ilala. Hata hivyo, Ofisa Elimu ya Sekondari wa Manispaa ya Ilala, Germana Mng’aho alisema asingeweza kuzungumzia suala hilo na kwamba mhusika mkuu ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ilboru, Arusha, Julius Shula alisema hata majina ya wanafunzi wanaojiunga na shule yao hawayafahamu. Mmoja wa walimu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, Dar es Salaam, alisema kwa kawaida wanafunzi wa kidato cha tano huripoti shuleni wiki mbili kabla ya wale wa kidato cha sita kitu ambacho mwaka huu kimekuwa tofauti. Msaidizi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwiru Wavulana ya Mwanza, Malongo Charles alisema wanasubiri wanafunzi watakaopelekwa na Serikali. Hata hivyo, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Moshi, Fanuel Angalo alisema anaamini wizara husika itatangaza wiki hii. “Ni jambo jipya kidogo limetokea lakini tunaamini Waziri atatoa tangazo lake wiki hii halafu wanafunzi hao wa kidato cha tano waripoti shuleni wiki ijayo,” alisema Angalo. Mkoani Tanga, walimu katika Shule za Sekondari za Tanga Ufundi, Gallanos na Usagara kwa nyakati tofauti, waliilalamikia wizara kwa kuwachelewa kuwapelekea wanafunzi wa kidato cha tano na kusema kuwa hiyo imevuruga utaratibu wa ufundishaji. Hakuna athari Baadhi ya wadau wa elimu walisema kilichotokea si kigeni kwani kimepata kutokea miaka ya nyuma na mihula ilirekebishwa na kwenda sawa na wenzao ambao walikuwa wameanza masomo. Mkuu wa Kitengo cha Habari na Ushauri wa HakiElimu, Nyanda Shuli alisema kubadilika kwa muhula wa kuanza masomo si jambo kubwa ambalo linaweza kuathiri elimu na kwamba anaamini wizara itakuwa imetoa mwongozo. Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Kitila Mkumbo alisema si mara ya kwanza kwa muhula wa masomo kubadilika kwani imewahi kutokea siku za nyuma na marekebisho yakafanywa ili kufidia muda ambao wanafunzi wanakuwa wamepishana na wenzao. “Sidhani kama ni jambo kubwa sana ambalo linaweza kuathiri chochote katika masuala ya elimu, la msingi ni kuhakikisha kuwa waliochelewa kuanza masomo wanapata muda wa kumaliza mtaala (mtalaa) wa masomo kama inavyotakiwa.” Kwa siku tatu mfululizo, kuanzia Juni 29, mwaka huu, wakuu wa shule za sekondari za Serikali walikutana katika Chuo cha Ufundi, Arusha kupitia majina ya waliochaguliwa na kuiachia kamati ya kukamilisha kazi hiyo. Hata hivyo, habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema tatizo kubwa lilikuwa ni idadi ya wanafunzi kuwa ndogo ikilinganishwa na nafasi za kidato cha tano kutokana na kufeli kwa wanafunzi wengi katika matokeo ya kidato cha nne, 2012. |
Udaku Specially |
RIHANNA TENA ATEMBEA KITAANI NDANI YA KIVAZI KINACHO MUONYESHA MPAKA NDANI Posted: 10 Jul 2013 11:44 AM PDT |
MAISHA YA OSAMA KABLA HAJAKAMATWA YAFICHULIWA Posted: 10 Jul 2013 11:35 AM PDT TUME ya Abbottabad imesema kuwa Osama bin Laden aliishi kama mtu wa kawaida bila wasiwasi wowote kwa karibu miaka 10 na aliwahi hata kusimamishwa na polisi katika eneo la Swat huko Pakistan kwa kupeleka gari kwa kasi mno, lakini hakukamatwa.
Ripoti hiyo iliyofichuliwa na Televisheni ya al Jazeera na kuoneshwa juzi jioni, inaonesha kinagaubaga maelezo ya kusisimua kuhusu maisha ya Osama bin Laden, mtu hatari aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba, na aliyekuwa akivaa kofia la mchunga ng’ombe katika tambarare za Marekani, kuepuka kugunduliwa kutoka angani. Ripoti hiyo ya kurasa 336, iliandikwa na tume ya Abbottabad inayoongozwa na jaji na iliyoundwa na Serikali ya Pakistan muda mfupi baada ya vikosi maalumu vya Marekani kumuua bin Laden Mei 2 mwaka 2011. Misingi ya ripoti hiyo ni mahojiano yaliyofanywa na vyanzo 201, wakiwemo jamaa wa familia yake na maofisa mbalimbali. Matokeo ya uchunguzi huo ambayo hayajachapishwa rasmi, yanajumuisha ushahidi wa uzembe mkubwa katika karibu kila ngazi ya vyombo vya usalama vya Pakistan. Ripoti inakosoa vikali namna Marekani ilivyofanya uvamizi katika makazi ya bin Laden huko Abbottabad, ikisema ilichukua hatua kama jambazi mhalifu. Inauweka katika kiti moto utawala wa Pakistan kwa kushindwa kugundua shughuli za Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), katika ardhi yake, na hautupilii mbali uwezekano wa kuhusika maofisa walaghai katika idara ya ujasusi ya Pakistan, suala tete kuligusia katika uchunguzi wa hali ya juu namna hiyo. Ripoti inatoa maelezo kuhusu usiku wa kifo cha bin Laden na kutoa taswira ya mtu aliyekuwa akibabakia na kama mwenda wazimu ambaye kila mara alikuwa mbioni kukwepa kutiwa mbaroni. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Bin Laden aliwasili nchini Pakistan msimu wa machipuko mnamo mwaka 2002, na wakati mmoja aliishi Haripur kwa miaka miwili kabla kuhamia katika makazi yake ya mjini Abbottabad na familia yake kubwa mnamo Agosti 2005. Ripoti inasema maeneo yote alikoishi hayajulikani kikamilifu, lakini miongoni mwao ni FATA yani Waziristan kusini na Bajaur, Peshwar, Swat na Haripur. Ripoti imegundua bin Laden aliingia Pakistan akitoa eneo la Tora Bora nchini Afghanistan, ambako majeshi ya Marekani yalikuwa yakimsaka mwaka 2002. Familia yake ilihamia Karachi, Pakistan kutoka Kandahar, muda mfupi baada ya mashambulio ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani dhidi ya jengo la Shirika la Biashara la Kimataifa (WTO) mjini New York, makao makuu ya wizara ya ulinzi, Pentagon nje ya mji wa Washington, na uwanja mmoja huko Pennsylvania. Osama hakupenda mali Katika ushuhuda wao wake wa bin Laden walisema hakupenda sana mali zake binafsi na alikuwa na nguo chache sana. Ripoti hiyo imesema kabla kwenda Abbottabad bin Laden alikuwa na mavazi matatu ya kitamaduni yajulikanayo kama shalwar kameez aliyoyavaa wakati wa msimu wa kiangazi na mengine matatu kwa ajili ya msimu wa baridi. Wakati alipojihisi anaugua, Osama bin Laden alijitibu mwenyewe kutumia dawa za kienyeji za Kiarabu. Kwa mujibu wa ripoti zisizo rasmi za Marekani, bin Laden alikuwa akiugua ugonjwa wa Addison, upungufu wa adrenalini mwilini, na kila mara alipojihisi mvivu angekula tufaha na chokoleti. Maofisa wa Serikali na usalama nchini Pakistan hawakuweza kupatikana ili kutoa kauli kuhusu ripoti hiyo. Baadhi ya maofisa wa Marekani wameelezea wasiwasi wao wakiyashuku mashirika ya ujasusi ya Pakistan kwa kumlinda bin Laden, lakini Pakistan imelipuuzilia mbali wazo hilo. |
HOT PHOTO OF THE DAY KUTOKA KWA MDAU Posted: 10 Jul 2013 08:09 AM PDT Kama una picha nzuri na ungependa itoklezee hapa nitumie kwenye e-mail hii : udakusp...@gmail.com
|
"VYOMBO VYA HABARI HUWA VINAHONGWA NA WAPINZANI ILI VIWAANDIKE VIZURI".....SPIKA WA BUNGE Posted: 10 Jul 2013 08:07 AM PDT Spika wa Bunge, Anne Makinda, ameibuka na kauli yenye utata mkubwa akivituhumu vyombo vya habari kwamba vinahongwa na wabunge wa kambi ya upinzani ili viandike habari zao vizuri.
Bila kufafanua ni kwa jinsi gani wabunge hao wanatoa hongo hiyo mbali tu ya kusema wanatoa kitu kidogo ili waandikwe vizuri, pia alikana kuwakandamiza wabunge wa kambi hiyo na kuwabeba wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wako upande wa serikali. Alisema hana upendeleo katika uendeshaji wa vikao vya Bunge kama anavyoshambuliwa na baadhi ya watu na kwamba lawama zinazoelekezwa kwake zinatokana na watu kuangalia upande mmoja. Spika Makinda alitoa ufafanuzi huo jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu vurugu mbalimbali zinazotokea katika vikao vya Bunge mjini Dodoma na hasa juu ya kuporwa au kugeuzwa kwa hoja za upinzani. Spika Makinda alikuwa ametoka kuzungumza na Spika wa Korea Kusini, Kang Chang Hee. "Ndiyo najua mnapewa 'kitu kidogo' na hawa wanaoanzisha vurugu bungeni, lakini kusema Spika anapendelea hili siyo kweli hata kidogo," aliongeza Spika. Alisema iwapo angekuwa na kawaida ya kuwakandamiza wabunge wa upinzani kwa kiasi kinachosemwa wengi wa wabunge hao wa upinzani wasingekuwapo bungeni. “Mimi siwapendelei wabunge wa CCM, ningekuwa hivyo hawa wapinzani wasingekuwapo bungeni,” alisema Makinda muda mfupi baada ya kuzungumza na ujumbe wa Bunge la Korea Kusini uliomtembelea ofisini kwake. Makinda alisema wakati wa kuendesha vikao vya Bunge haitakiwi kuwa na itikadi za vyama na kwamba kufanya hivyo kunaweza kusababisha vurugu. Wakati Spika akitoa utetezi huo, wabunge wa upinzani kwa nyakati tofauti wamekuwa wakimtupia lawama za wazi hususani wanapokuwa katika vikao vya Bunge kwamba anawapendelea wabunge wa CCM. Miongoni mwa mambo ambayo Spika Makinda amekuwa akilaumiwa ni pamoja na kukalia zaidi ya taarifa 10 za ushahidi juu ya kauli za wabunge wa upinzani zilizowasilishwa kwake na yeye kuzikalia kwa muda wote bila kusema lolote. Miongoni mwa ushahidi huo, umo wa mawaziri kusema uongo bungeni. Pia Spika amekuwa akilaumiwa jinsi mjadala wa hoja binafsi za wabunge wa upinzani ‘zilivyoporwa’ na serikali, kama ile ya Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia, kuhusu mitalaa ya elimu; ya mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, kuhusu hali ya upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es Salaam, na hata ya Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari, kuhusu ardhi ya Meru. Zote hizi ama ziligeuzwa na kupoteza maana yake hali iliyosababisha mvutano mkali bungeni ukiacha picha ya upendeleo wa dhahiri kwa baadhi wafuatiliaji wa mijadala ya Bunge. Akizungumzia mchakato wa kupata Katiba mpya, Spika Makinda alisema Bunge la Katiba litakutana Novemba, mwaka huu na litawajumuisha wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na wajumbe 160 ambao hata hivyo alisema sheria haijasema wanapatikana vipi. Alisema mwezi ujao serikali inatarajia kupeleka muswada wa sheria ili kufanya marekebisho ya namna ya kupata wajumbe hao 160 ambao siyo wabunge. Spika alisema katika Bunge hilo, yeye hatakuwa mwenyekiti na kwamba wajumbe wenyewe watachagua kiongozi atakayewaongoza. Kauli ya Makinda iliwahi kusemwa pia na Naibu wake, Job Ndugai, mara baada ya kuahirisha kikao cha Bunge kwenye mkutano uliopita, kufuatia vurugu zilizotokea baada ya hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani Wizara ya Mambo ya Nje, Ezekiah Wenje, kutamka kuwa Chama cha Wananchi (CUF) kina uhusiano na vyama vinavyounga mkono mashoga. Wakati vurugu zikiendelea nje ya viwanja vya Bunge kwa wabunge wa CUF na Chadema kuzozana, Ndugai alipita ndipo aliulizwa na waandishi Kulikoni, lakini katika hali ya kushangaza, alivituhumu vyombo vya habari kwamba ndivyo vimesababisha hali hiyo. “Haya yote mmesababisha ninyi waandishi, mnawadekeza sana wabunge wa upinzani, hata wangefanya nini mnawapamba pamba, lakini mkumbuke siku wakiingia madarakani watafanya haya haya wanayofanya leo,” alisema Ndugai bila kufafanua kauli yake. Kwenye mazungumzo yake na ujumbe wa Bunge la Korea uliomtembelea ofisini kwake, Spika alisema unalenga kudumisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali zikiwamo za uwekezaji na kuendeleza uchumi wa nchi hizo mbili. Kwa upande wake, Spika wa Korea, Chang Hee alisema nchi yake imepiga hatua kubwa ya maendeleo ingawa haina chanzo chochote cha kuzalisha nishati ya umeme ikilinganishwa na Tanzania. Alisema Bunge la Tanzania linafanya vizuri kwa upande wa nafasi za viti maalum ikilinganishwa na Korea Kusini ambayo idadi ya wanawake bungeni ni ndogo. Nipashe: |
Posted: 10 Jul 2013 07:58 AM PDT Vilabu vinne ambavyo vilihusika na njama ya kupanga matokeo ya mechi vimepigwa marufuku nchini Nigeria. Katika mechi moja klabu moja iliilaza nyingine magoli 79-0 na magoli 67-0 katika mechi ya pili. Jumla ya magoli 146 yalifungwa katika mechi hizo mbili, idadi ambayo inaingia katika vitabu vya kumbukumbu kama mechi iliyokuwa na idadi kubwa zaidi ya magoli duniani. Klabu ya Plateau United Feeders iliilaza timu ya Akurba kwa mabao 79-0 wakati timu ya Polisi ya Machine FC kwa upande wake ikailaza Bubayaro magoli 67-0. Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria, Muke Umeh amesema ufisadi na ulaghahi wa kiwango hicho hakiwezi kukubalika katika soka ya sasa. Umeh ametangaza kuwa baada ya mkutano wa kamati hiyo, ilibainika wazi kuwa vilabu hivyo vina kesi ya kujibu na hivyo vyote vinne vimepigwa marafuku ya kushiriki katika mecho yoyote, hadi uchunguzi utakapokamilika. Kabla ya mechi hiyo vilabu vya Plateau United Feeders na Police Machine vilikuwa na alama sawa na vilikuwa vikipania kupandishwa daraja hadi ligi daraja ya pili. Feeders ilipata magoli 72, katika kipindi cha pili ili hali Machine nao wameripotiwa kufunga magoli 61 katika kipindi cha mechi yao. Kufuatia matokeo hayo Plateau ilimaliza ya kwanza kwenye msimamo wa ligi na idadi kubwa ya magoli ikifuatwa na timu hiyo ya polisi. ''Tutachunguza sakata hii na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika'' Alisema Ummeh. Mkurugenzi wa michezo na mashindano wa Shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria, Dkt. Mohamed Sanusi, amekariri tangazo lililotolewa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi kuwa waliohusika wataadhibiwa vikali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NFF, vilabu vilivyohusika, wachezaji,, maafisa wa kiufundi wa timu na wasimamizi wa mechi hiyo watakaopatikana kuhusika kwa njia moja au nyingine, katika kashfa hiyo ambayo imetajwa kuwa mbaya zaidi katika historia ya soka nchini Nigeria watachukulia hatua kali za kisheria. Source:Shafii Dauda |
OBAMA KAINZIA KAZI TANZANIA:AMCHAGUA AMSAIDIZI WAKE WA KARIBU KUWA BALOZI WA TANZANIA Posted: 10 Jul 2013 07:52 AM PDT Rais wa Marekani Barrack Obama amemteua msaidizi wake wa karibu, Mark Childress kuwa balozi wa nchi hiyo, hapa nchini.
Childress ni msaidizi wa Obama katika Ikulu ya Marekani (White House) akiwa Naibu Mkuu wa Utumishi anayeshughulikia mipango katika Serikali ya nchi hiyo na aliwahi kufanya kazi katika Bunge la Seneti. Obama amefanya uteuzi huo ikiwa ni wiki moja tangu alipohitimisha ziara yake katika nchi tatu za Bara la Afrika, Tanzania ikiwa mojawapo. Pia alizitembelea Senegal na Afrika Kusini. Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani jana ilisema nafasi hiyo inahitaji kuidhinishwa na Bunge la Seneti la nchi hiyo. Uteuzi wake unaweza kuwa na maana kubwa katika kutekeleza sera za nje za Marekani. Katika miaka ya karibuni, Tanzania imeshuhudia ziara za viongozi wakuu wa nchi hiyo nchini ambao ni Bill Clinton, George Bush na Obama. Kuteuliwa kwa Childress, kunaashiria kwamba Balozi wa sasa wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt anakaribia kumaliza muda wake. Awali, Childress ambaye aliwahi kuwa msaidizi na msiri wa muda mrefu wa Seneta wa zamani, Tom Daschle, alitarajiwa kushika moja ya nyadhifa mbili katika utawala wa Rais Obama ambazo ni Mkuu wa Utumishi katika Idara ya Huduma ya Afya ya Jamii (HHS) au Naibu Mkurugenzi katika Ofisi ya Maboresho ya Afya katika Ikulu ya Marekani. Hata hivyo, jina lake liliondolewa katika mapendekezo ya uteuzi wa kuongoza ofisi hizo baada ya kuhusishwa katika masuala ya kodi Februari 2009, hivyo kubaki pasipo na jukumu maalumu. Pamoja na mkanganyiko uliojitokeza awali kuhusu majukumu yake, Childress alimudu kufanya kazi kubwa katika kuwezesha kupitishwa kisha kutekelezwa kwa mabadiliko makubwa katika sekta ya afya ya nchi hiyo. Aliteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Utumishi wa Marekani, 2012. Mwaka 2009, mpigania mabadiliko na maboresho ya sekta ya afya Marekani ambaye sasa ni Seneta, Edward M. Kennedy alimwomba Childress kujiunga na timu yake ya ushauri wa masuala ya afya, elimu, wafanyakazi na pensheni. Timu hiyo pia ilikuwa na kazi ya kumshauri kuhusu masuala ya mabadiliko ya afya na Childress alikuwa miongoni mwa watu walioshiriki kutoa rasimu ya kwanza ya muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Afya 2009. Baada ya muswada huo kupitishwa Februari 2010, Childress aliondoka katika kamati hiyo na kujiunga na Idara ya Huduma ya Afya ya Jamii Marekani ambako alikuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo mpya akiwa Kaimu Msimamizi Mkuu wa idara hiyo. |
Posted: 10 Jul 2013 07:42 AM PDT POLISI wapatao sita Jumamosi iliyopita walivamia nyumbani kwa staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu maeneo ya Kijitonyama kwa lengo la kumkamata kufuatia kesi iliyofunguliwa katika Kituo cha Polisi Kawe jijini Dar.
Awali taarifa zilidai kuwa, tuhuma zinazomkabili staa huyo asiyekaukiwa na matukio ni za kumtukana na kumpiga vibao Godluck Kuyumbu ambaye ni meneja wa hoteli moja maarufu jijini Dar. Baada ya kesi hiyo yenye jalada KW/RB5988/2013 SHAMBULIO kufunguliwa kituoni hapo Julai 6, mwaka huu mishale ya saa 5 asubuhi, maafande hao wakiwemo wa kike wawili wakiwa wamevaa kiraia walifika mtaa anaoishi staa huyo na kuufunga kabla ya kwenda kugonga katika geti la nyumba yake. Mara baada ya kugonga geti hilo, alitoka mwanaume aliyefahamika kwa jina la Petman, alipoulizwa kuhusu Wema, alijiumauma huku kijasho kikimtoka kabla ya kutoa jibu la kwamba hakuwepo. Majibu hayo hayakuwaridhisha polisi hao ambapo walilazimika kuzuia kila gari lililokuwa linatoka Hata hivyo, hawakufanikiwa kumuona ndipo walipolazimika kumuita mjumbe wa eneo hilo na kuomba ruhusa ya kuingia ndani kufanya upekuzi lakini hawakumtia mikononi na taarifa zikawa mwanadada huyo yuko Zanzibar. Maafande hao waliomba namba ya simu ya Wema na walipompigia alisema yuko Zanzibar, kesi hiyo anaijua na atakaporejea atajisalimisha mwenyewe polisi. SOURCE: GPL |
AGNESS AWAJIBU WATU INSTRAGRAM BAADA YA TUHUMA KUENEA KUWA AMEKAMATWA Posted: 10 Jul 2013 07:34 AM PDT Baada ya habari za kukamatwa kwa mtanzania Agness Gerald na Melisa Edward, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6 kuenea na kuthibitishwa na kamanda wa polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya "Godfrey Nzowa". Agness Jerald ambae wengi wanahisi ni Aggy Masogange ambae pia yuko nchini South Africa mpaka dakika hii, (ambapo haijajulikana kama ni yeye kweli) ameonekana akiendelea kuandika kupitia mtandao wa instagram licha ya kutangazwa kwa habari hizo. masaa matatu yaliyopita Aggy alipost picha hii hapo chini na kuandika maneno haya na baadae kupost pichaa hii yenye caption hiyo hapo chinijessolomon@renatusleonard naomba nijuze kunani?? hasnajalangoMh muulize wewe maana kang'ang'ana keshasema keshasema......amesea wapi nini ama udaku 2...@jessolomon minashabaniMumy nimekuwazia mengi nakukusikitikia sana@aggnesfineassgirl mwenyezi mungu akusaidi kama nikweli upo pouwa na afute hizi husda za midomo yawatu waliyo kuchuria mumy wangu leahna1112Pole sana mumyto kwanini wanakusingizia hivyo? Pls ukirudi wafungulie kesi haiwezekani wakuchafulie Jina kiasi hichi mpolesam@wolpergambe akupigii ngoo sababu sio yeye na ukimwambia ukweli anakublock ni mumewe anawazuga watu wanyamaze nishabebee88Tunasemaga BUH BUH BUH likimpata mtuu timua vumbiiiiiii BUHHHHHHHHHHHH .. love u bby boo salmakbarbinadamu haswa watz tumezoea kuona wenzetu wasiendelee wakuache mumy wng @aggnesfineassgirl , miss kisses zhussein777hata ingekuwa kweli its non pipoz bussnes .... unatafuta zako huwa tafutii wao kula zako maisha @aggnesfineassgirl tarinawhtAm hapi������,watasonyajeeeeee!!do ur thing hun achana na wazushi Kama nawaona hii hii ���� dats y I lov u@aggnesfineassgirl mamyluqMimi midomo yangu bado iko wazi uku kungekuwa na nzi ningemeza nzi nilivyoshaangaa wabongo tumefikia apa mtu anaropoka tu duuu pole mdada ila du |
BRAND NEW SONG FROM STEVE RNB FT MR BLUE - HUYU DEMU Posted: 09 Jul 2013 10:36 PM PDT |
SWALI:MALAYA NI NANI? MWANAUME AU MWANAMKE? Posted: 09 Jul 2013 09:59 PM PDT The title above is concerned!
Malaya ni nani? Ni mwanaume au mwanamke? Je, kila mtu anaweza kumwita mwanamke/mwanaume malaya? Hata kama hawajawahi kukutana naye kimwili? Kwa upande wangu huwa naona vigumu kumwita mwanamke malaya wakati sijawahi mgegeda... Nini kipimo cha kuwa malaya? kuna wadada wanapenda sana pesa tena kwa uwazi kabisa.. je, hawa ni malaya? lastly..kuna tofauti gani kati ya majina haya hapa chini na malaya? i. kahaba ii. changudoa.. Hebu tujadiliane.. Ladies & Gentlemen.. |
MANDELA APUMULIA MASHINE..MADAKTARI WAPANGA KUIZIMA Posted: 09 Jul 2013 09:53 PM PDT MADAKTARI wanaomtibu Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, wanakubali kuwa kiongozi huyo basi tena kwani hali yake ni tata na sasa wanasubiri kiungo kimojawapo cha mwili wake kishindwe kufanya kazi ndipo wazime mashine inayomsaidia kupumua. Kutokana na subira hiyo madaktari hao sasa wamebadili msimamo wao wa awali wa kuiondoa mashine hiyo inayomsaidia kupumua. “Madaktari hao, wameishauri familia yake kuachana na ushauri wa awali wa kuiondoa mashine hiyo hadi tu pale moja ya kiungo chake muhimu cha mwili kitakaposhindwa kufanya kazi,” alisema rafiki wa Mandela, Denis Goldberg ambaye alikuwa mpigania uhuru aliyewahi kufungwa pamoja na Mandela. Amesema madaktari hao waligusia kuhusu suala la kuondoa mashine lakini baadaye walikataa kwa kuwa kiongozi huyo aliweza kusogeza baadhi ya viungo na kutambua sauti. “Ni kweli kuwa hali ya Mandela ni mbaya lakini si kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika,” alisema Goldberg. Juzi vyombo vya habari vya hapa nchini vilitoa hati ya kiapo ya mahakama, ikionyesha kuwa madaktari hao waliishauri familia ya Mandela kuondoa mashine ya kumsaidia kupumua kwani asingeweza kuendelea kuishi. Hata hivyo, msemaji wa Rais Jacob Zuma,Mac Maharaj alikataa kuzungumzia kuhusu hati ya mahakama ambayo ilieleza kuwa Mandela mwenye miaka 94 yupo mahututi. |
FLORA LYMO AMPONDA SPORAH NJAU KWA KUMWAMBIA TID NI MGONJWA KWENYE LIVE INTERVIEW Posted: 09 Jul 2013 09:42 PM PDT Sasa wewe Sporah hebu jisikize Mwenyewe tena ,na tena 'huwezi na huruhusiwi hata kama ungekuwa Dactari'Afya ya Mtu au Ugonjwa wake unatakiwa kumuuliza yeye mwenyewe in a private'Or labda kama mmekubaliana na mkaandikiana na to be sign that you are agree with it' na siyo kama hivi kumuanika Live''kumwambia mtu yeye Afya yake siyo nzuri na huku umeshikilia mauchafu ulosomba huko mitandaoni ya Haters wake ambayo mengi ni ya Kimburulas na yenye kumtuhum kwamba anatumia Madawa ya kulevya (Drugs)na pia amekonda hata akivaa nguo hapendezi ,Ina maana hao hao wanaosema pia anatumia sembe 'ndo wamempa au ? mara anadokoa, Kusema kweli ungetakiwa uchague maswali yaku muuliza mengi yakiwa ni yako wewe Mwenyewe Sporah what your doing to T.I.D. Here is just ' ,abuse '' I'm sorry but you are and make me feel bad about you and All of those mamburulas'' Stop Abusing Him na kumuharibia Biashara yake ''Kudadadeki Watanzania tena kama wewe Sporah nilidhani ni Mtu ambae unatakia watu Mema kumbe ndo umeshakuwa wakuwatakia watu Mabaya tena kuwaharibia Biashara zao''so you just want to see all Watanzania not attend his Show kama wewe unavyofanya alafu ndo tukae Vibarazani na kwenye Vistudio tukiwasubiria waje ndo tuwashambe na hasa to Abuse them ? yani sikutaka kuambiwa nilitaka nione na kusikia mwenyewe and I just did that''na ndo maana nikaamua kukujibu pale nilipoweza '' kwani ninakazi zangu sina Muda huu wa Mamburula maswali ya Kijinga 'upumbavu mtupu' Tupa kule and I hope Wasanii wengine hutowafanyia hivi tena maana ndo will be the end of Sporah Show'' Mbuta Nanga'' Jirekebishe Mono Njau''Ruwa Mangi''
Hivi ni kwanini ulikuwa una taka aku hagi hagi ,akukumbatie huku umeketi chini ? how can you ask someone to give you a hug huku wewe kama mpokea wageni wako umekaa chini ? ungetakiwa kuamka ,kusimama then unamuuliza ask him for hug' au ndo ulikuwa wataka kumshika shika ili uone kama kweli kakonda ? why were you crying for His hug? yani mpaka nilitamani kuvunja my Laptop ''you were so annoying and Abusing Him' and that made me so Upset and Angry ''I don't want to watch the show anymore' you need kumuomba T.I.D Msamaha'' I mean wewe mbona Nguo zako zingine huwa hazikupendezi na huwa ni kubwa mwilini'so tuseme pia kukonda kwako ni Ugonjwa na hiyo ndo sababu au pia wewe unatumia sembe? what you feel watu tukianza kuuliza mitandaoni kukuhusu''and oh 'what happen with you and Jestina G' ulimchukulia Mme wake ? ndo sababu mkavunja penzi lenu na mlikuwa mashosti wa mwiko na ugali?'Yani Sporah don't even go there kuwauliza Haters wa Mtu wakuandikie vitu vya ku muuliza unae mfanyia Interview kabisa. Kumbuka hapa Duniani ukishakuwa na Kitu ambacho wengi hawanacho lazima utakuwa na Haters tena kibao 'so chakufanya ni kutokuwapalilia'kama unavyofanya wewe'' Anyway 'ni hayo tu from Flora Lyimo'Msema kweli wenu'mbuta nanga"WATANZANIA MSOENDA KWENYE SHUGHULI ZAO''Nikianza na wewe Sporah 'huendagi kwenye Shughuli zao hata Moja mimi tangu nianze kukusikia na kukutane na wewe uso kwa uso kwenye your studio sijawahi kukuona hata siku moja umehudhuria show zao 'Wasanii wa Tanzania hapa UK 'na huku wao wakija kwenye studio yako unaanza kuwauliza Maswali ya kimburulas'' Au hata ukijishughulisha na kuhudhuria mambo yanayo wahusu Sisi Watanzania tuliopo Majuu UK 'Ningeomba siku moja ufanya Live Television show ambayo itakuwa broadcast at exactly the same time as you are interviewing Mtu' alafu uone kama kuna atakae kuja utaniambia Flora Lyimo ' nimekuonea hapa au hapana nimekuambia Ukweli wako'' Usione hawa Wenzetu waliokuwa fasta kukutumia maswali yao ya umburulas ukadhania wana mapenzi mema na T.I.D au hata ambae utakae mfanyia hiyo Interview '' Wasanii wanapata shida sana kupewa Pesa zao kihalali hapo na hapo tena kabla ya show au ya safari zao 'na vile vile Watanzania wenzao wakiwa ndo wanaogoma kwenda kwenye show zao kwa sababu zao binausi kukosa pesa pia kunachangia. Kwani kuishi majuu kwa Wengi ni hasara tupu ila wapo wapo tu 'anyway pia huwa wanambizana wasiende'' yani hii yakwako japo itakuwa pia ni bure licha ya kulipisha £10 pound pesa ndogo hivyo na inawashinda uone kama hiyo ya Live show watakuja''You know how good we are kwa kuangushana..Right'' na hicho ndicho tunashotakiwa kukipinga 'hasa kutokuwapa nafasi HATERS''Ila hapa wewe Sporah unaanza kuwashirikisha na kukukufanya wewe mwenyewe kuonekana Mburula''TUPENDANENI JAMANI AND YES YOU NEED TO APOLOGIZE''Flora Lyimo Fashion Police " You might also like: |
SINA MUDA WA KUMJIBU RAIS KIKWETE...NASUBIRI MUDA MWAFAKA WA KUMUONESHA MIMI NI NANI" PAUL KAGAME Posted: 09 Jul 2013 09:32 PM PDT Nikiwa katika upekuzi wangu, nimeshtushwa sana na kauli za KIHUNI za Rais Paul Kagame dhidi ya Rais wetu Kikwete na nchi yetu kwa ujumla....
Rais Kikwete ameepuka malumbano na Kagame kwa kukaa kimya , lakini inaelekea Kagame anadhani ukimya wa Kikwete ni uoga kwake au labda anatafsiri kuwa anadharauliwa..... Nadhani huu ni wakati mwafaka kwetu sisi watanzania kuungana na kumuunga mkono rais wetu juu ya huu UPUMBAVU wa Kagame.... Kagame ni lazima atambue kwamba watanzania tupo tayari kuilinda nchi yetu kwa gharama yoyote na kamwe hatuwezi kuwa VIBARKA wa Rwanda... Ifuatayo ni Kauli ya Kihuni aliyoitoa Rais Kagame Kwa Taifa letu: ------------------------------------------------------------- .....“Those people [Tanzanian President Jakaya Kikwete] you just heard siding with Interahamwe and FDLR and urging negotiations… negotiations? Me, I do not even discuss this topic, because I will just wait for you [Tanzanian President Jakaya Kikwete] at the right place and I will hit you! He[Tanzanian President Jakaya Kikwete] did not deserve my answer. I did not waste my time answering him…It is well known. There is a line you cannot cross, there is a line, a line that you should never cross. It is impossible…”“ It is in these ominous terms that the Rwandan dictator General Paul Kagame threatened to get even with Tanzanian President Jakaya Kikwete, while addressing Rwandan Youth on June 30, 2013 during a summit called “Youth Konnect”“, sponsored by his wife, Janet Kagame. Relations between Tanzanian President Jakaya Kikwete and Rwandan leaders have soured in the last weeks. On several occasions Rwandan leaders called the Tanzanian President “a genocide and terrorist sympathizer”, “ignorant”, “arrogant”, and “mediocre leader”. The relations have deteriorated following the recommendation by President Jakaya Kikwete of open negotiations between Rwandan, Ugandan and Congolese leaders and their respective armed opposition in order to bring durable peace and security in the African Great Lakes region.... source..I will Just Wait For You At the Right Place And I will Hit You, Rwandan General Paul Kagame Threatens Tanzanian Jakaya Kikwete |
Udaku Specially |
SINA HAMU NA MWANAMKE TENA HATA AWE MZURI KIASI GANI Posted: 11 Jul 2013 12:15 PM PDT Najisikia sihitaji mwanamke yeyote yule hata akiwa mzuri kiaisi gani. Sina hamu naye na wala siwezi kumfanya chochote. Naogopa kusema i hate you women kwani ni kama neno lisilo sahihi. Nina mke wa muda mrefu sasa na mtoto mmoja, tulioana kwa upendo sana hasa mimi nikiwa na furaha sana kwenye ndoa yangu, lakini cha ajabu mambo yalibadilika sana mara nyingi mke akawa ni wa kulalamika tu, mara nyingi anashinda amenuna, maongezi hakuna kabisa ndani,. Nilijitahidi sana kumuweka chini na kuzungumza naye nikijishusha na wakati mwingine kuomba anisamehe na aniambie makosa yangu yanayomfanya asiwe na furaha. Mara nyingi nilidhani ni mambo ya "kitandani" labda sifanyi vizuri lakini cha ajabu amekataa sana juu ya hili na kusema anaridhika sana na tena kwa kiwango cha juu na mara nyingi tumekuwa tukifanya hilo tendo hubadilika na kuwa mpole sana na hata kusema ananipenda sana. Nimemwambia kwa lolote analoona liko tofauti aniambie mara nyingi najishusha sana kwake na nina msikiliza san, lakini nimegundua hana nia ya dhati maana kila kukicha anakuwa vilevile tena wakati mwingine hufanya makusudi kabisa. Sikutarajia maishani mwangu kuwa na ndoa ya hivi inaniuma sana, nilimuoa kwa taratibu zote za kikanisa na ndoa kubwa na yenye maana, najiuliza kumwacha inakuwa siyo solution maana moyo huwa unaniuma sana kiasi kwamba natoa machozi na kumbembeleza, ninavyoelewa nimefuata moyo wa mama yangu ni mpole saaana tena sana nadhani hata mimi nimerithi huko. Umefika wakati sasa nimechoka machozi yananitoka kila wakati, ofisini kazi zimenishinda sasa, na siwezi chochote, najihisi sisitahili kuishi duniani lakini natakiwa kuwasaidia wanaonitegemea, nahisi wanawake wote wanaroho mbaya za kinyama kiasi kunitesa hivi, lakini mbona mama yangu ni mtaratibu kiasi hicho? Kuna kitu kimoja kimenijia nimelia sana, nilikuwa namchumba mpole sana ila alinikataa ghafla bila kosa na kwenda masomoni, kumbe hakunikataa ila alifanya hivyo ili tusisumbuane wakati anasoma amemaliza nikiwa nimeoa, aliposikia amelia sana, na mimi nimelia sana. Dunia haijanitendea haki. Nimetulia chumbani nalia sana saivi sipati solution zaidi moyo wangu unawachukia wanawake zaidi. Wanawake hamna jema kabisa yaani hata mkipendwa na kulelewa kama watoto mnakuwa hivi? Source:Jamii forums |
PREZZO AMPONDA DIAMOND....AMWITA DOMO Posted: 11 Jul 2013 11:49 AM PDT Majigambo ya Diamond kwenye vyombo vya habari kabla ya Tamasha la Matumaini kufanyika kuhusu kumgalagaza Prezzo kwenye show hiyo hayajampendeza Rapcellency na sasa ameamua kujibu. Prezzo ambaye jina lake halisi ni Jackson Makini alianza kwa kuweka picha ya gazeti inayowaonesha akiwa na Diamond kwenye habari iliyohusu tamasha hilo na kuandika ‘Hahahaha #DomoSeriously???? Rapper huyo hakuishia hapo aliweka picha nyingine ya Diamond na kuandika: “U talkin money or u talkin nonsense au anashindana na ndovu kun***a? Mwisho alimalizia kwa kujibu tweet ya mtu mmoja aliyemwambia kuwa huyo ni Diamond kwa kuandika: Unfortunately only “diamonds” I know is the ones on ma neck fam.” |
NIMETEMBEA NA WANAUME 10 BAADA YA KUOLEWA- MUME WANGU HAJUI Posted: 11 Jul 2013 06:15 AM PDT I know my story will lead people to attack me but I will appreciate any help I can get. I got married to my loving husband in April 2010. Although at first, I was not really in love with him, but because I was getting older, and I could not find any good man from my religion and tribe, my parents introduced me to him and pressured us into marriage. The first time I had an affair, it was a mistake. I ran into my ex and we exchanged Blackberry pins. We chat all the time and at that point, I was not really happy in my marriage so I encouraged him. Soon after, we started to hang out and started sleéping together. He eventually moved from Nairobi to Kisumu so that ended our affair. Since then, I have had a few flings with 9 more men including my friend's husband. I currently have two children with my husband but I feel unsatisfied. My husband is very loving and kind, and I have grown to love him but I'm not able to stop this extra-marital affair. The sad thing is that my husband has no clue what is going on. I never give him any reason to suspect. I delete all my phone messages even though he does not even check my phones. I make sure I cover my tracks because I want to keep my family together. Recently I talked to my Pastor who encouraged me to keep praying and fasting but this isn't helping because still keep my men outside and I still see them. I know I need to stop, but I don't know how. Please Help. Rachael. |
KIJANA WA KIAFRIKA WA MIAKA 23 AMUOA KIBIBI KIZEE CHA KIJERUMANI CHENYE MIAKA 83 Posted: 11 Jul 2013 05:50 AM PDT |
WEMA SEPETU, MARTIN KADINDA... WATIBUANA Posted: 11 Jul 2013 05:01 AM PDT KIMENUKA! Beautiful Onyinye au ‘Madam’ Wema Isaac Sepetu anadaiwa kutibuana na yule meneja wake, mwanamitindo Martin Kadinda kwa kurushiana maneno mtandaoni, Amani limesheheni.
Kwa mujibu wa chanzo makini, ishu ilianzia mbali na kusababisha hali kuwa tete kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na kuibua gumzo la aina yake huku mashabiki wa Wema wakidai yao ni macho tu, kuona nini kitakachojiri. Chanzo hicho kilitiririka kuwa ‘sosi’ ya kutibuana kwao ni baada ya Kadinda kutundika picha ya nyumba yake akiwa amepaka rangi mpya ambapo baadhi ya watu walimpongeza lakini Wema yeye akaguna bila kusifia kama wengine walivyofanya. Mpashaji wetu aliendelea kutonya kuwa kitendo cha Madam kuguna kilimuumiza Kadinda na kuanza kumwandikia maneno ambayo yalionekana hayakumpendeza Wema. “Nilijua tu una kiroho na roho ya hasidi iliyojaa uzandiki,” aliandika Kadinda akimjibu Wema. Ilidaiwa kuwa maneno hayo yalimpandisha hasira Wema na kuamua kumtahadharisha meneja wake huyo kuwa asimwambie maneno ya aina hiyo katika mtandao wa kijamii unaosomwa na wengi. “Please don’t talk to me like dat on social network (tafadhali usizungumze na mimi hivyo kwenye mtandao wa kijamii),” aliandika Wema. Mtoa habari wetu aliendelea kumwaga ‘unga’ kuwa baada ya ujumbe huo kumfikia Kadinda naye alijibu mashambulizi kwa kumwandikia Wema: “Umezoea kuogopwa…anyway cut it short (basi yaishe).” Ilisemekana kuwa baada ya Kadinda kuandika hivyo, wadau mbalimbali kwenye mtandao huo waliwasihi kuweka tofauti zao pembeni au wazimalize wenyewe na siyo kubishana mtandaoni na kufaidisha wasiohusika. Baada ya habari hizo kutua kwenye ‘deski’ la gazeti hili, mwanahabari wetu aliwatafuta wahusika kwa njia ya simu ambapo Kadinda alipopatikana na kuulizwa juu ya kutibuana na Madam, alikiri kutofautiana na Wema lakini akadai walishaweka mambo sawa. “Ni kawaida, hata vikombe vikikaa sehemu moja hugongana lakini namshukuru Mungu kwa sasa tupo sawa,” alisema Kadinda anayemiliki lebo ya mavazi ya Single Button. Kwa upande wa Wema alipoulizwa juu ya ishu hiyo, alicheka na kusema kuwa wao ni binadamu na si malaika hivyo kukwaruzana ni jambo la kawaida. “Umenichekesha sana, unajua sisi ni binadamu eeeh… siyo malaika, hayo mambo yaliisha siku ileile na hapa baada ya dakika kumi anakuja (Kadinda) kwa ajili ya kupata chakula cha mchana,” alisema Wema. |
DIAMOND AFICHUA KISA CHA KULALA NA UWOYA! Posted: 11 Jul 2013 03:55 AM PDT SIRI nje! Lile skendo la Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kudaiwa kulala na mwigizaji Irene Uwoya ambaye ni mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ limevuja.
KISA KAMILI Huku akijua kabisa kuwa ataibua zogo kwa kuwa Uwoya ni mke wa ndoa wa mtu, kwa mara ya kwanza, Diamond ameamua kuanika kisa kilichomfanya kujiweka kwa muda kwa Uwoya. Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika cha gazeti hili, kilichomfanya Diamond kufikia hatua ya kumtongoza na kutoka naye kimapenzi, ni kitendo cha Uwoya kutoa maneno ya kumponda huku akionesha waziwazi hali ya kumchukia kila walipokutana. UWOYA ALIKUWA HAMPENDI DIAMOND “Unajua Irene (Uwoya) alikuwa hampendi Diamond hata siku moja na mara nyingi alikuwa kila akimuona lazima amponde. Habari hizo zilikuwa zikimfikia mwanamuziki huyo kupitia mashoga wa mwigizaji huyo ambazo ndiyo zilichochea. “Kufuatia hali hiyo, Diamond naye kila alipofikishiwa taarifa na mashosti wa Uwoya, alikuwa akijisikia vibaya mno ndiyo maana ‘Sukari ya Warembo’ alilazimika kumvizia Uwoya kwa hali na mali ili kumfanya ampende. CHIKOKA ATAJWA “Nakumbuka kwa mara ya kwanza Diamond alimtuma (Juma) Chikoka ‘Chopa’ kwa Uwoya ili amfikishie ujumbe wa yeye kumtaka. “Chikoka hakufikisha taarifa hizo, kitendo ambacho kilimuuma sana lakini siku moja Diamond alikutana na Uwoya akiwa na Chikoka, maeneo ya Sinza-Mori (Dar), akamuomba tena Chikoka namba, akampa, hapo ndipo uhusiano ulipoanzia. “Siku mbili baadaye Diamond alizungumza vizuri na Uwoya. GLOBAL NOMA “Diamond aliomba ahadi ya kukutana na mwigizaji huyo, bila kuchelewa, Uwoya aliiva na kukubali ambapo walikutana kwenye ile hoteli mliyoandika (Global) kule Mbezi Beach (Dar) wakamalizana. “Unajua Diamond alifanya hivyo kwa sababu ya kupondwa na washikaji zake kuwa anatamba kutembea na mastaa lakini hamuwezi Uwoya. “Kwa hiyo utagundua chanzo cha yote ni mdomo wa Uwoya kutangaza kutompenda Diamond kwani alikuwa akimsema vibaya sana kwa watu wake wa karibu,” kilidai chanzo chetu. BOFYA HAPA KUMSIKIA DIAMOND Baada ya kujazwa habari hizo, mwanahabari wetu alilazimika kumtafuta Diamond ili kuhakikisha kama alichoelezwa kina ukweli ndani yake ambapo bila kinyongo, mkali huyo wa wimbo wa Kesho alifunguka: “Dah! Japo yalishapita ila ni kweli Uwoya nilikuwaga nikipata taarifa kutoka kwa marafiki zangu kuwa alikuwa ananichukia sana. “Nilikuwa nikijiuliza sababu za yeye kunichukia lakini nikawa sizipati hata kidogo na hata nilipochunguza niligundua kweli alikuwa hanipendi kabisa. “Sipendi sana kuzungumzia ishu hiyo ila naweza kukubali kweli kuwa marafiki zake na wangu ndiyo walionichochea sana kukutana na Uwoya na sasa hatuna tatizo na tunaishi kwa amani na upendo ingawa mengi yamepita na yaliyosemwa sina sababu ya kuyashikilia, kikubwa tumuombe Mungu.” KAMA KAWA UWOYA HAPOKEI SIMU Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimwendea hewani Uwoya lakini kama kawaida, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa. TUJIKUMBUSHE Miezi kadhaa iliyopita, gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda liliripoti habari ya Uwoya na Diamond kunaswa usiku katika moja ya vyumba vya hoteli maarufu kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi huko Mbezi Beach, Dar ambapo habari hiyo iliibua maneno lakini sasa mwanamuziki huyo amemaliza utata kwani nguzo na sifa kuu ya Global Publishers ni kuandika ukweli siku zote. |
Posted: 11 Jul 2013 03:16 AM PDT Ni takribani siku sita sasa toka wasichana wawili raia wa Tanzania Agnes Gerald na Melisa Edward kukamatwa katika uwanja wa ndege wa OR Tambo Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya zaidi ya billion 6 za Tanzania.
Swala linalozua maswali mengi ni jinsi gani wasichana hao waliweza kupita katika uwanja wa ndege Julius Nyerere na karibia kilo 150 za dawa hizo za kulevya, kiasi ambacho Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini imesema ndio mzigo mkubwa zaidi wa dawa za kulevya kuwahi kukamatwa katika mipaka yote ya nchi hiyo kama mzigo mmoja (kwa lugha nyingine imevunja rekodi). Idara ya polisi nchini Tanzania imekiri kuwa Agnes na Melisa walipitia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, na walisafiri na ndege ya shirika la ndege la South African Airways inayomilikiwa na serikali ya Afrika Kusini. Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa akiongea na NIPASHE jana (June 10) waliotaka kujua wasichana hao walipitia uwanja gani wa ndege na kama walikaguliwa. Alikiri kuwa wasichana hao walikaguliwa kama abiria wengine, lakini akadai kwamba si jukumu la Jeshi la Polisi kufanya ukaguzi kwenye viwanja vya ndege, na kuongeza kuwa ni jambo la kawaida mtu kukamatwa nchi nyingine na dawa za kulevya wakati katika nchi aliyoanzia safari hajakamatwa kwani inategemea utalaamu wa watu wenyewe wanaokagua. “Kila mtu anapopita uwanja wa ndege anakaguliwa na kama ana kitu ambacho ni kibaya ndipo anakamatwa, hawa wasichana walikaguliwa maana huwezi kupita uwanja wa ndege bila kukaguliwa,” Alisema. Kamanda Nzowa aliongeza kuwa watu wa uwanja wa ndege ni lazima wawe na mtu au mkaguzi ambaye ni mtaalamu sana wa kutambua dawa za kulevya kwa kuwa ziko za aina nyingi na mbinu nyingi zinatumika kuzisafirisha. “Utakumbuka Juni 23 mwaka 2010 nilikamata mabalozi wawili, hawa watu walitoka Brazil wakaenda Afrika Kusini, lakini tukawakamatia hapa Tanzania,” alisema Nzowa Kamanda Nzowa alisema uchunguzi unaendelea kumbaini mmiliki wa dawa hizo na kuna dalili za kuwabaini wahusika hao. Aliendelea kusema Dawa hizo zilisafirishwa kama mizigo mingine inayokaa sehemu za mizigo ndani ya ndege kwani uzoefu unaonyesha kwamba kwa namna yoyote ile abiria hawezi kuruhusiwa kwenda kukaa na mzigo wake ndani ya ndege unaofikia kilo 150. Aliongeza kuwa Katika hali ya kawaida, hata kama wasichana hao wangeamua kugawana dawa hizo kwa usawa, kila mmoja angebeba kilo 75, kiasi ambacho hata hivyo abiria haruhusiwi kupanda nacho kama mzigo wa mkononi, wala mzigo ambao haulipiwi. Taarifa kuhusiana na kukamatwa kwa wasichana Agnes Gerald (25) na Melisa (24) wakiwa na mzigo mkubwa wa dawa za kulevya wenye thamani ya zaidi ya billion 6 kumezua maswali mengi ikiwa ni pamoja na hofu kubwa kutokana na ongezeko kubwa la watanzania wanaozidi kukamatwa wakitaka kusafirisha au kuingiza dawa hizo nchini. Hivi karibuni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika taarifa yake ilisomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, mjini Dodoma, katika maadhimisho ya kitaifa ya ‘Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani’ alisema tatizo la dawa hizo ni janga la kitaifa hivi sasa nchini. Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani. Mwezi huu (July) pekee watanzania watano wamekamatwa wakisafirisha dawa za kulevya zenye thamani ya shilingi billion 9. Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa Agnes Gerald na Melisa Edward wameshafunguliwa mashitaka nchini Afrika Kusini. SOURCE: NIPASHE |
DIVA AJIPACHIKA TATOO NYINGINE JUU YA KIUNO Posted: 11 Jul 2013 03:01 AM PDT |
"SIPO TAYARI TENA KUMVULIA NGUO MR. BOND.".....AUNT LULU Posted: 10 Jul 2013 11:48 PM PDT Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amesema yeye na aliyekuwa mpenzi wake, Bond Bin Salim imebaki historia na kamwe hawawezi kurudiana naye japo anayajua mapenzi.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema ameshaamua kujituliza kwa mpenzi wake wa sasa hivyo hata iweje hawezi kurudiana na Bond. “Jamani kwa sasa mnaona nimebadili kabisa staili ya maisha yangu hivyo Bond atabaki kuwa rafiki kama walivyo marafiki zangu wengine. “Niliwahi kuachana naye kipindi flani baadaye tukarudiana kutokana na ukweli kwamba ni mwanaume anayejua kupenda na anayajua mapenzi ,lakini hii ya sasa ndiyo imetoka, kamwe siwezi kurudiana naye,” alisema Aunty Lulu. |
Posted: 10 Jul 2013 11:22 PM PDT Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Transparency International, Kenya imeshika nafasi ya nne kwa ufisadi ikiwa ni miongoni mwa nchi 107 ambako utafiti huo ulifanywa. Ripoti hiyo ilibaini kwamba Wakenya saba kati ya 10 waliohojiwa walisema wamewahi kutoa hongo maishani mwao ili waweze kupata huduma moja hadi nane kati ya zilizochunguzwa. Kulingana na utafiti huo, maofisa wa polisi ndio waliopatikana kuwa mafisadi zaidi nchini wakifuatiwa na wabunge, vyama vya kisiasa, mahakama na wafanyakazi wa Serikali. Wakenya wengi walisema vyombo vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za kidini hazina ufisadi mwingi. Nchi fisadi zaidi duniani ni Sierra Leone ambako asilimia 84 ya watu waliohojiwa walikubali kwamba wametoa hongo. Sierra Leone inafuatwa na Liberia (asilimia 75) na Yemen (asilimia 74). Nchi ambazo zilipatikana kuwa na ufisadi finyu ni Finland, Japan, Australia, Denmark, Uhispania, Canada, Ureno, Uruguay, Norway, New Zealand, Korea Kusini na Malaysia ambako watu zaidi ya 95 kati ya 100 waliohojiwa walisema hawajaona ufisadi wowote nchini mwao. Katika eneo la Afrika Mashariki, Kenya ndiyo nchi fisadi zaidi ikifuatwa na Uganda (asilimia 61) na Tanzania (asilimia 56). Kulingana na utafiti huo ambao watu 114,000 walihojiwa, Rwanda ilipatikana kuwa na ufisadi mdogo zaidi katika eneo la Afrika Mashariki. Raia 13 pekee kati ya 100 wa nchi hiyo walikubali mwamba wametoa hongo. Ufisadi ulipatikana kukithiri zaidi barani Afrika. Baadhi ya nchi fisadi zaidi Afrika ni Zimbabwe, Msumbiji, Libya na Cameroon (zote zikiwa na asilimia 62) na Nigeria (asilimia 44). |
HUYU NDIO MREMBO AMBAE GELLY WA RYMES AMESEMA ANAFAA KUISHI NAE Posted: 10 Jul 2013 11:21 PM PDT Gelly wa Rhymes ni mmoja wa wabongo ambao wamewahi kumilikishwa namba nzuri kwenye chati za radio mbalimbali Tanzania na Kenya hasa kupitia single ya ‘Mama Ntilie’ ft Ray C.
July 10 2013 Gelly ameiweka hii siku kama kumbukumbu baada ya kulihutubia taifa la bongofleva kupitia hii video mpya inaitwa ‘lovely’ Please jisikie huru kuitazama na kuacha maoni yako hapo chini mtu wa nguvu. |
BLOGS MBALI MBALI ZAMKOSOA WEMA KWA KUWEKA PICHA ZINAZOONYESHA MICHIRIZI YA MAPAJA Posted: 10 Jul 2013 10:56 PM PDT Jana na juzi topic katika mitandao mbali mbali imekuwa ni Mapaja ya wema Sepetu baada y kuweka picha akionyesha mapaja yake ambayo yana michirizi....Blogs nyingi zimeandika kuwa ni adhari za kujichumbua .... Soma hapa blogs zilivyomuandika: Sangofesto blog Zeddilicious blog Bongoclantz blog |
Udaku Specially |
PICHA ZA MTANZANIA ANAYE TEMBEA KWA MGUU KUTOKA MBEYA MPAKA DAR Posted: 12 Jul 2013 12:57 PM PDT Anakwambia safari yake ya kutembea kwa mguu kutoka 87.8 Mbeya mpaka Dar es salaam anaiita Uzalendo Tour kuisupport Taifa Stars na anategemea baada ya kuimaliza, watu wengi wataiunga mkono timu ya taifa Taifa Stars.
Anavyotembea kwa sasa anakutana na watu wengi sana na watu wengi wamekua wakimpigia simu baada ya namba yake kutajwa hewani Clouds FM, wengine amekutana nao njiani na wamekua wakimpa vitu mbalimbali vikiwemo viatu na nguo mpya. Katoka Mbeya saa kumi alfajiri akafika Makambako saa moja na dakika 19 akiwa tayari katembea kilometa 186, akachukua gari mpaka 92.9 Iringa mjini kwa sababu ilikua imeshakua usiku tayari… akachukuliwa na gari la Wambura mdau wa Power Breakfast ya Clouds FM na kumuacha Iringa mjini alikolala mpaka asubuhi na kuianza safari tena. Anakwambia saa nane kamili alikua anauanza mlima Kitonga na akaumaliza kwenye saa tisa na dakika kadhaa, baada ya hapo alitembea mpaka kitongoji cha mwisho kabla ya kuianza Ruaha kisha akachukua gari mpaka Morogoro mjini kwa sababu ilikua usiku tayari, ameamkia 88.5 Morogoro mjini na sasa anakuja 88.5 Dar es salaam. Anasema hii ni idea aliyokua nayo kwa muda mrefu sana lakini akashindwa kuifanya kutokana na kukosa mda ila anamshukuru sana Gerald Hando wa Power Breakfast @Cloudsfm ambae amemsaidia sana kufanikisha hii safari. Sio sehemu zote anatembea kwa mguu, usiku ukiingia inamlazimu apande gari. Source:Millard Ayo |
HATIMAYE AGNES MASOGANGE AKUBALI AMEKAMATWA HUKO S.AFRICA Posted: 12 Jul 2013 07:56 AM PDT HUKU skendo ya kunaswa akiwa na madawa ya kulevya ikiendelea kumtesa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ anatarajiwa kupandishwa kortini nchini Afrika Kusini leo kujibu shitaka ambalo mwenyewe hajaliweka wazi, Ijumaa linakupasha.
Agnes Gerald ‘Masogange’. AWALI YA YOTEMwishoni mwa wiki iliyopita, habari ya mjini ilikuwa Masogange kanaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini. Habari zilisambaa kwamba sanjari na Masogange, mwingine aliyenaswa naye ni mdogo wake (mtoto wa mama yake mdogo Agnes) aitwaye Melisa Edward. Kwa mujibu wa habari hiyo ya mjini, wawili hao walinaswa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oriver Tambo uliopo Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania wakiwa na ‘mzigo’ wa kilo nyingi aina ya ‘crystal methamphetamine’ wenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni 6.8! IJUMAA LAANZA KUSAKA UKWELI Baada ya kunasa habari hiyo, Ijumaa liliingia mzigoni kuusaka ukweli ambapo hata hivyo, madai hayo yalikuwa yakijifungafunga sana. Mtu mmoja wa karibu na Masogange alipoulizwa kuhusu ukweli au uongo wa habari hiyo alikuwa na haya ya kusema: “Ni kweli Agnes amekamatwa akiwa na madawa ya kulevya kule Sauzi. Lakini si yenye thamani hiyo ya bilioni sita bali ni milioni arobaini tu. Hata hivyo, ameachiwa kwa dhamana ila paspoti yake imezuiliwa. “Nadhani kuna mambo yanawekwa sawa ikiwezekana atarudi nyumbani.” JIJINI DAR, KAMANDA WA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA ANENA Jumatatu iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliviambia vyombo vya habari kuwa, Watanzania wawili walikamatwa nchini Afrika Kusini na mamlaka ya mapato wakiwa na madawa ya kulevya kutoka Tanzania yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8. Kamanda Nzowa aliwataja Watanzania hao kuwa ni Agnes Gerald ambaye ana miaka 25 na Melisa Edward mwenye miaka 24. Alisema wawili hao baada ya kukamatwa na chombo hicho walikabidhiwa kwa polisi ambapo mahojiano yanaendelea. IJUMAA LAMWIBUKIA KAMANDA NZOWA Baada ya Kamanda Nzowa kuwataja kwa majina wawili hao Jumatatu iliyopita, siku iliyofuata, Ijumaa lilipiga hodi kwenye ofisi za kamanda huyo kwa lengo la kutaka kujua kama Agnes Gerald aliyemtaja jana yake ni Masogage au majina yanafanana tu. Kamanda huyo hakuwepo ofisini kwake asubuhi hiyo na kwa mujibu wa wasaidizi wake, alikuwa kwenye kikao cha dharura kwenye Ofisi za Polisi wa Kimataifa ‘Interpol’. APIGIWA SIMU Ilibidi Ijumaa limsake kwa njia ya simu ya kiganjani kwa mara kadhaa. Alipopokea akaulizwa kuhusu Agnes Gerald aliyemtaja kama ni Masogange yule staa. Kamanda Nzowa: “Eee, mimi siwezi kusema ni huyo, ninachojua ni Agnes Gerald tu basi. Sasa kama ni Masogange mimi sifahamu lolote.” JUMANNE USIKU SIMU KUTOKA SAUZI Mpaka hapo, timu nzima iliyokuwa ikifuatilia habari hiyo haikuona ukweli wa Agnes Gerald kuwa ni Masogange na kwa vile siku zote Global Publishers inasimamia utafiti kabla ya kuandika habari iliamua kuiweka pembeni kwanza ili kuendelea kuichimba. Saa 2:14 usiku wa siku hiyo, Ijumaa lilipokea simu yenye kuashiria wito (code number) ni ya nje na kabla haijapokelewa, ilibainika ni ya Afrika Kusini. Ijumaa: Haloo. Sauti: Haloo, mimi Masogange. Ijumaa: Mambo Agnes, pole sana na mkasa uliokupata bwana, pole sana. Agnes: Kwanza naumizwa sana na maneno ambayo watu wanazidi kuyaeneza sehemu mbalimbali bila kuwa na uhakika wowote, mimi sikukamatwa kwa sababu ya madawa ya kulevya. “Mkasa nilioupata siyo ambao watu wanaueneza kwenye mitandao mbalimbali na katika vyombo ya habari.” Ijumaa: Kwa hiyo madai ya kukutwa na madawa ya kulevya si ya kweli? Agnes: Kweli nilikamatwa huku kwa matatizo f’lan ila siyo ishu ya madawa kama watu wanavyosambaza. Ijumaa: Ni tatizo gani sasa? Agnes: Unajua sipendi tena kuwapa watu faida ila lilikuwa ni tatizo la kawaida, nilikamatwa na baada ya hapo nilitoka na niko huru. Nasubiri tu kwenda mahakamani Ijumaa (leo) mara moja kisha n’tarudi Bongo. Ijumaa: Mh! Sasa Egg, mbona huku mpaka viongozi wa polisi wamesema ni madawa? Agnes: Hapana, siyo, ipo ishu ndogo tu. Ijumaa: Haya pole sana kwa misukosuko. Agnes: Asante sana, nitakuja huko siku si nyingi. Habari hii imeandikwa na Imelda Mtema, Haruni Sanchawa na Musa Mateja. |
DIDA APIGWA DONGO"TULIA SASA NA HIYO NDOA TUMECHOKA KUHUDHURUA SHEREHE ZA NDOA ZAKO" Posted: 12 Jul 2013 07:45 AM PDT BAADA ya hivi karibuni Mtangazaji wa Radio Times, Khadija Shaibu ‘Dida’ kufunga ndoa na mwanaume aitwaye Ezden, mashosti zake wamemtaka kutulia sasa na asijaribu kugeuza ndoa kuwa fasheni. Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, baadhi ya mastaa walioomba hifadhi ya majina yao ambao walihudhuria ndoa hiyo iliyofungwa Ijumaa iliyopita Ubungo jijini Dar walisema, wamechoka na mialiko ya ndoa zake kila baada ya kipindi kifupi hivyo ni wakati sasa wa kutulia, Hii ni ndoa ya Tatu ya Dida. “Asifanye ndoa kama fasheni, tumechoka kuhudhuria sherehe za ndoa yake, kama ana kasoro, ajirekebishe ili atulie sasa ajenge maisha yake,” alisema staa mmoja ambaye ni rafiki wa karibu na ndugu wa Dida. Hata hivyo, akizungumzia kuhusu kuolewa huko, Dida alisema safari hii ndoa yake ikivunjika haolewi tena. Kwa hisani ya Na Hamida Hassan /GPL |
MADAWA YA KULEVYA NA AIBU YA TANZANIA-YATOSHA SASA JAMANI Posted: 12 Jul 2013 07:37 AM PDT Hatuwezi kuendelea kukaa kimya. Taifa letu linaaibika vibaya sana.
Wahusika wanajulikana. Wametajwa mara nyingi na mbinu wanazozifanya kwa kutumia wasanii wa kizazi kipya na waigizaji almaarufu kama 'Bongo Movie'. Inaudhi, inakera na inatuongezea chuki sana kwa serikali iliyo madarakani. Kaeni kimya na endeleeni kulichafua taifa, kuna siku mtatueleza yote. Au kwakuwa wahusika ni wanenu? Au kwakuwa wakuu wa juu ni wale waliowawezesha kuingia madarakani kisiasa? Ndugu zangu, hii ni aibu kubwa kwa Taifa. Inasikitisha sana na inazidi kutuaibisha wengine tunaosafiri ng'ambo. Taifa kama halina rais, taifa kama halina Vyombo vya Dola. Ni upumbavu, ni ufedhuli na mtambue sasa tumechoka. Mambo haya mlimchomekea mtoto wa Mengi, mambo haya mnawachomekea wanyonge wenye njaa kali na hadi mmeua vijana wetu kwa kuwabebesha mizigo michafu hivi! |
NIMGUSE WAPI SHEMEJI YENU ILI ASISIMKE? Posted: 12 Jul 2013 07:27 AM PDT Hodi hodi wana udakuz
Mie ni mdada wa makamo naishi Dar es salaam .... shida yangu kubwa naombeni msaada wa kujua maeneo gani ya mwili wa mwanaume yakiguswa au kufanyiwa chochote yanampa raha muhusika kupitiliza....... Nia na madhumuni ya haya yote ni maandalizi kabambe ya kumtuliza shemeji yenu nyumbani....... nataka akitoka kazini afikirie nyumbani na si kwingineko..... Pls majibu yenu ndio dawa yangu. Mimi Sarah |
JESHI LA POLISI TANZANIA LAAMUA KUMFUATA AGNESS MASOGANGE AFRIKA KUSINI Posted: 12 Jul 2013 07:21 AM PDT Jeshi la Polisi litapeleka askari wake Afrika Kusini kuwahoji washiriki wa video za wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Agnes Gerald ‘Masogange’ na mwenzake Melisa Edward waliokamatwa nchini humo na dawa za kulevya.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aliliambia gazeti hili kwa simu jana kuwa watawapeleka polisi kuwahoji na wanaamini wahusika watawaeleza wahusika wa mzigo huo. Wasichana hao walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania wakiwa na kilo 150 za dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine. “Tutawapeleka askari wetu kuwahoji, tumekwishaanza uchunguzi wa hili...wote watakaohusika katika hili tutawakamata, lakini tunakwenda polepole hatua kwa hatua kuhakikisha tunawanasa wahusika sahihi,” alisema Nzowa. Naye Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, (JNIA), Moses Malaki alieleza kushangazwa na kiasi kikubwa kupitishwa kwenye uwanja huo licha ya kuwa wapo watu wenye dhamana ya kuangalia usalama. “Sitaki kusema tutafanya nini, lakini ninachotaka kukwambia ni kwamba uchunguzi umeanza na suala zima tumewaachia polisi na sisi tutatoa ushirikiano kwa kila hatua watakayotutaka, lazima kukomesha hili. “Tutaangalia nani walikuwa zamu siku hiyo,” alisema Malaki. |
WAKENYA WAMKOSOA PREZZO BAADA YA KUMTUKANA DIAMOND-SOMA WALICHOMWAMBIA Posted: 12 Jul 2013 07:17 AM PDT Msanni Prezzo wa Kenya atakuwa amepata sample ya majibu ya baadhi ya fans wake ambao wengi ni wakenya baada ya kumdiss Diamond Platinumz wa Tanzania kupitia akaunti yake ya twitter July 10. Sample ya majibu hayo inaweza kuonekana kupitia comments zote za fans kwenye habari iliyowekwa na mtandao wa ghafla wa nchini Kenya, ambapo asilimia 99 wameonesha kutokubaliana na alichokifanya. Edwin Mwashegwa : ah, Diamond achana na huyu mbulula, wewe unda hela!, bifu za kisenge hazifai. Top Commenter: Prezzo umepita hiyo age ya beef za kishenzi. Ingia studio utoe kitu, otherwise kwa musiki diamond ako juu. I feel you bro! anything to remain relevant and grab some headlines. Bellah Ongachi : aaarggh Diamond is waaayy better.. n am sure by the time he hits the years prezzo has stayed in the entertainment scene he'll be miles ahead..so your thing diamond. Caroline Karijo : Mhhhhh who even listens to to him Jaguar and Diamond r much better than him n we all knw,,,,,,, he can continue playing women who stoops low for him. Yvonne De Cole : Prezzo ni wivu nini,,,, leave the highest paid musician in East Africa alone,,, ana mulla en he is still simple doesn floss,,,, prezzo inherits yet flosses De Sheriff : Diamond, silence is the best weapon. let the baby throw tantrums. Prezzo, its tym to mature up. Diamond hadi sasa bado hajazungumza chochote. |
Posted: 12 Jul 2013 07:18 AM PDT SERIKALI ya Tanzania imeipa onyo kali nchi ya Rwanda ikiitaka isijaribu kuota ndoto za kuishambulia kijeshi, vinginevyo itajibu mapigo kwa nguvu zote na kuhakikisha kuwa imeichakaza.
Kauli hiyo ya kwanza nzito imetolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa kufuatia taarifa ya matamshi makali yanayodaiwa kutolewa na Rais Paul Kagame wa Rwanda, dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na kutishia kuishambulia Tanzania. Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa wizara hiyo, Mkumbwa Ally, alisema ingawa Serikali ya Tanzania hadi sasa inajua haina ugomvi wowote na Rwanda, lakini amekiri kuwapo kwa kile alichokiita ‘kupishana lugha’ kwa Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame. Mkumbwa alikiri Serikali ya Tanzania kunasa matamshi yanayodaiwa kutolewa na Rais Kagame katika moja ya hotuba zake aliyoitoa Juni 30, nchini kwake wakati akihutubia katika hafla moja ya vijana. Kwa mujibu wa hotuba hiyo, ambayo kwa wiki sasa imesambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii, Kagame anadaiwa kusikika akitoa matamshi ya vitisho dhidi ya Rais Kikwete, kwamba anamsubiri katika wakati aujuao na kumchapa. Baadhi ya maneno yanayodaiwa Rais Kagame aliwaambia vijana waliokutana katika mkutano wao uliojulikana kama ‘Youth Konnect’ na kufadhiliwa na mke wake, Janet Kagame, yanasema: “Huyu mtu mliyemsikia akiwa upande wa Interahamwe na FDLR na akashauri majadiliano….majadiliano?” Aidha, Kagame anadaiwa kusema kuwa hatakuwa tayari kujadili jambo hilo, isipokuwa atamsubiri Rais Kikwete sehemu muafaka na ‘kumtandika’. “Sitapoteza muda wangu kumjibu Kikwete, inajulikana maana kuna mahali hataweza kuvuka…haiwezekani,” alikaririwa akisema Rais Kagame, akilenga kumtisha Rais Kikwete. Mbali na Kagame, baadhi ya viongozi kadhaa wa serikali ya Rwanda wamekuwa wakimshambulia Rais Kikwete wakimpachika majina ya kejeli ya; “Rais mhurumia magaidi, wauaji wa kimbari, mkorofi na mwenye dharau.” Mkumbwa hata hivyo alisema Serikali ya Tanzania haina sababu ya kuingia katika vita na Rwanda, kwa sababu tu ya ushauri alioutoa Rais Kikwete wa kuitaka ikutane na wapinzani wake wanaoishi ndani ya nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kujadiliana kuhusu amani ya nchi za Maziwa Makuu. Alisema msimamo wa Tanzania utabaki kuwa uleule wa kuitaka nchi hiyo ikubali kukaa meza moja na wapinzani wake, ili kumaliza migogoro inayoendelea katika nchi hizo za maziwa makuu, ambao unaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na SADC. “Unajua mgogoro wa DRC na Rwanda hauwezi kumalizika bila ya nchi hizo kukaa meza moja na wapinzani wao ili kupata suluhu ya kudumu,” alisema Mkumbwa. Aliwataka Watanzania kuwa watulivu na kuendelea na kazi zao kama kawaida, kwani serikali yao iko makini katika kulinda mipaka yake. Chanzo cha mzozo Msuguano baina ya nchi hizi mbili ulianza siku chache tu baada ya kumalizika kwa kikao cha viongozi wa nchi za Maziwa Makuu na ambacho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, chini ya uenyekiti wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni. Rais Kikwete wakati akimtaarifu Rais Museveni kile walichokuwa wamekijadili katika kikao hicho kwa vile aliketi kwa muda kwa kuwa alichelewa kuwasili, alisema ni vema serikali za Rwanda na Uganda zifungue mlango wa mazungumzo na waasi wao na akaanza kutaja majina ya vikundi vya uasi vya nchi hiyo vilivyopo nchini DRC. Habari zinasema kauli ya Rais Kikwete iliungwa mkono na Rais Museveni akisema: “Bila mazungumzo hatutafika popote pale”. Hata hivyo, matamshi hayo yalijibiwa kwa ukali na serikali ya Rwanda, kiasi cha kumlazimu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kutoa tamko bungeni. Kwa kauli yake, Membe alisema serikali ilikuwa imeshangazwa na shutuma hizo za Rwanda kwani halikuwa jambo baya kutoa ushauri uliolenga kuleta mapatano na kuepusha umwagaji zaidi wa damu wa wananchi. Akaongeza kuwa, ilikuwa ni wajibu wa Serikali ya Rwanda kuupokea ama kuukataa, na wala si kutoa maneno ya kejeli na vitisho. Kauli ya Zitto Akizungumzia kauli hiyo ya vitisho, mwanasiasa machachari hapa nchini na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, alisema ushauri wa Rais Kikwete kwa Rwanda ulikuwa wa busara mno na akashangaa kuona nchi hiyo jirani ikitoa vitisho, kejeli, dharau na ukosefu wa adabu kwa Kikwete. Katika moja ya tamshi lake alilolitoa jana katika mitandano ya kijamii, Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) alisema Marekani wanaongea na waasi wa kundi la Taliban, hivyo hakuna dhambi kwa Rwanda pia kufanya hivyo. “Pia kama hutaki ushauri si unakataa tu, sasa kuanza kurushiana maneno ya nini tena? Hutaki ushauri basi. Maneno ya kila siku ya nini? Tangu Kikwete amesema kule Addis, hajasema tena. Membe (waziri) akajibu Dodoma Tanzania haijasema tena. Kigali inasema mambo haya kila siku kwa ajili ya nini? “Taliban na Al Qaeda si wale wale? Wale watoto waliozaliwa mwaka 1994 na wakimbizi wa Kihutu waliopo Kongo nao ni wauaji? Tufikiri vizuri mambo haya. Kuna ‘genociders’ wasakwe, wakamatwe wahukumiwe. Kuna watu wana haki kabisa ya kutaka kushiriki kwenye siasa za Rwanda na wanazuiwa, wameshika silaha. Hawa lazima wakae meza moja wakubaliane,” alisema Zitto. Mwanasiasa huyu alisema kwa sasa serikali za nchi hizo mbili zinatakiwa kuingia katika vita ya kupambana na kuondoa umasikini wa watu wake na si vita ya mtutu wa bunduki. “Busara itumike kwa viongozi ‘neutral’ kama Uhuru Kenyatta kuwaweka pamoja Kagame na Kikwete wamalize tofauti zao. Haya maneno hayana maana yoyote,” alisema. Alisema vita haitamuumiza Rais Kagame wala Rais Kikwete na familia zao, bali itaumiza wananchi wa kawaida wa mikoa ya Kagera na Kigoma na mikoa ya mpakani ya Rwanda. “Vita itaturudisha nyuma sana kwenye juhudi za maendeleo. Vita itazima harakati za kujenga demokrasia nchini. Busara itumike tu,” alisema Zitto. Tanzania Daima |
VIDEO YA WEMA SEPETU AKIPIGWA KISSES YAVUJA Posted: 12 Jul 2013 07:07 AM PDT Video inayomuonesha staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akidendeka na mwanaume imevuja mtandaoni... Haikuweza kufahamika mara moja lengo la Wema na mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Aidany ‘kujishoot’ wakifanya vitendo hivyo ila wanaonekana wakiwa katika mazingira ya ki-Mr & Mrs. Aidha, katika video hiyo, Wema anaonekana kutumia nguvu kubwa kumshawishi Aidany amsogezee mdomo lakini mwanaume huyo anasita na hata alipokubali kudendeka hakutoa ushirikiano wa asilimia 100. Mwanaume fegi mkononi Katika video hiyo, mwanaume huyo anaonekana kutumia muda mwingi kuvuta sigara yake huku Wema akiwa bize kumpapasa kimahaba. Ni filamu? Baada ya video hiyo kunaswa swali lililokuja ni je, ni sehemu ya filamu za mwanadada huyo anayemiliki Kampuni ya Endless Fame au ni uhalisi wa mambo! Katika kujua ukweli, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Wema kupitia simu yake ya mkononi lakini mara nyingi imekuwa ikiita bila kupokelewa. Aidha, mwandishi alichukua hatua ya kwenda nyumbani kwake maeneo ya Kijitonyama jijini Dar lakini alimkosa na hata alipokwenda ofisini kwake hakuweza kumpata. Source: Gazeti la ijumaa |
Udaku Specially |
SAD:MCHUMBA WA NEY WA MITEGO AANGUKA, MIMBA YACHOROPOKA Posted: 13 Jul 2013 11:34 AM PDT Rapper Nay wa Mitego leo anasherehekea siku ya kuzaliwa ya mchumba wake aliyekuwa mjamzito kwa huzuni kubwa baada ya mchumba wake huyo kukipoteza kichanga chao kufuatia kuanguka jana usiku.
“Jana usiku mke wangu alianguka, alifikia tumbo kwahiyo akawa anasikia kizunguzungu nilipompeleka hospitali daktari akasema mtoto amekufa,” Nay Awali, Nay wa Mitego ameweka picha ya mchumba wake kwenye Instagram akiwa hospitali na kuandika: Happy bday my lv, Mungu akupe maisha marefu na yenye mafanikio tele. Japo imekukuta uko vibaya tumempoteza kijacho bt ni mipango ya mungu, nakupenda sana mke..!! #966# happy bday 2u ma.” |
HUYU NDIO RAY C KWASASA, AWA KIBONGE BALAA Posted: 13 Jul 2013 11:08 AM PDT Mwanamuziki staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye amepotea katika anga la muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya, amejitokeza akiwa amefutuka.
Hivi karibuni, Ray C ameibuka na kuanza kutundika picha na vipande vya video zake katika kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya kujiweka karibu na mashabiki wake. Kufuatia ishu hiyo, kumeibuka mshtuko mkubwa kwa baadhi ya watu kutokana na picha hizo kumuonesha ‘bidada’ akiwa amenenepeana ghafla tofauti na alivyozoeleka. UNENE UNATOKANA NA DOZI? Baadhi ya mashabiki wake katika mtandao wa Instagram walidai kuwa inawezekana unene huo unatokana na dozi ya kuacha ‘unga’. Hata hivyo, wengine walimshukuru Mungu kwa kuwa sasa afya ya mwanadada huyo inaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida tofauti na miezi kadhaa aliporipotiwa na gazeti hili akiwa amezimika kutokana na matumizi ya unga. Katika picha hizo, Ray C anaonekana kufutuka usoni, kifuani na mapajani ambapo awali kabla ya matatizo hakuwa hivyo. Wengi walimshukuru Mungu kumuona tena Ray C akiwa mzima pamoja na ukimya wake katika muziki. Ray C amekuwa akitundika picha hizo kwa ajili ya mashabiki na marafiki hasa kupitia Instagram akiambatanisha na maelezo huku nyingine zikizungumza zenyewe. HATAKI KUTAJA ANAPOISHI Maelezo ya picha hizo yamekuwa yakielezea maisha ya Ray C kwa sasa akiwa kwenye mjengo wa maana bila kutaja ni sehemu gani. Kwa mujibu wa mashabiki wa Ray C, mwanadada huyo kwa sasa anakula bata tu huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anamuita ‘Daddy’ kwa kuwa ndiye aliyemsaidia kimatibabu. Daktari mmoja maarufu jijini Dar aliyehojiwa , alibainisha kuwa kinachosemwa na mashabiki wa Ray C kwamba kinachomnenepesha ni dozi ya kuacha madawa ya kulevya, kinaweza kuwa kweli au kisiwe kweli. Aliongeza kuwa kunenepa kunachangiwa na vitu vingi kama kupata maisha mazuri yasiyohusisha msongo wa mawazo au mihangaiko ya hapa na pale hivyo anachofanya ni kula, kulala na kustarehe tu. GPL |
NINI SABABU YA MWANAUME KUMWAGA KABLA YA TENDO Posted: 13 Jul 2013 11:03 AM PDT |
HATIMAYE K-LYNN AMUWEKA MUMEWE MH MENGI NA WATOTO WAKE Posted: 13 Jul 2013 08:14 AM PDT |
MSHIRIKI WA TZ NANDO AAMBUKIZWA GONJWA LA ZINAA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER Posted: 13 Jul 2013 08:10 AM PDT In a hushed conversation between Nando and Bimp, Nando narrated how he got infected with an STD after his liason with Selly! For the past days we have been seeing Nando and Selly who were once an item getting distant and avoiding each other but not knowing what happened between them. Thank God that nothing can be kept secret forever and so we had to know the cause why the two fell out. Nando disclosed that Selly gave him chlamydia a Sexually Transmitted Disease, but we can’t tell how true this is. However, if we are to go by the Tanzanian’s revelations, it explains why the two are no longer getting along well as it was the case at the beginning. Nando for the past days has been ill, down in bed and if at all his words are to be believed, they answer the question; “What has he been suffering from?” The Tanzanian lad and the Ghanaian dame had strong feelings for each other that it didn’t even take them a day to open the sexual gates and enjoyed each other’s package through the deed. Despite the fact that he enjoyed Selly’s goodies, Nando made it crystal clear that he wasn’t ready for a serious relationship but just wanted to satisfy the hungry Nando in him. All in all, we are not sure whether it was Selly who gave Nando the STD or he had it before. And there is also a possibility that he was suffering from another disease. But let’s scrutinize this; For Nando to have been sick and seeing doctors for the past days and with Selly mentioning to Oneal that Biggie told her to be using protection (condoms), it explains that she has also been treated for it. The same Nando also openly called Selly out on her arena failure right before everyone else causing her to run off crying saying they should nominate her out to go home if that is how badly they all feel about her. Did Selly make a mistake by getting involved with Nando who has only disgraced her every step of the way since then? What is your view on this issue? |
BABU ANAYETAKA KUMFUFUA MWALIMU NYERERE AGEUKA GUMZO Posted: 13 Jul 2013 02:41 AM PDT Mzee (pichani) aliyeibuka hivi karibuni akidai kuwa ana uwezo wa kumfufua Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere amezua gumzo. Babu huyo aliibuka katika studio za Kyera FM huko mkoani Mbeya akihitaji msaada wa kumfikisha Butihama alipozikwa Mwalimu Nyerere mwaka 1999 ili amfufue. Mzee huyo alikuwa na ufunguo mkononi ambao anadai ndiyo utakaotumika kumfufua Nyerere. Anaeleza kuwa akishamfufua Mwalimu Nyerere ndiye atakayesimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. |
ANGALIA KAMERA ZA SIRI ZILIVYOFICHUA UCHAFU WA HOUSE GIRL KWA MTOTO Posted: 13 Jul 2013 02:40 AM PDT Upo uwezekano mkubwa wa haya mambo kutokea kwenye familia nyingi hasa za Kiafrika ambazo desturi yetu ni kuajiri wasichana wa kazi kabisa.
Hii video hapa chini ni ripoti ya kusikitisha ambayo ilitolewa nchini Kenya baada ya Kamera kutegeshwa kwa siri ili kuona Wasichana wa kazi huwa wanafanya nini wakiwa wamebaki wenyewe nyumbani? ANGALIA VIDEO HAPA: |
JINI MAHABA LINAVYONITESA LINANIINGILIA MPAKA KINYUME NA MAUMBILE-HELP Posted: 12 Jul 2013 10:00 PM PDT Hi ni history ya kweli ya maisha yangu naomba mnishauri wadau.
Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 29 ni mkristu na ni mzaliwa wa morogoro mwenye asili ya mkoa wa kilimanjaro.Wakati wa utoto wangu nilikuwa ni mtu mwenye akili sana.Kuanzia la standard 1 mpaka form 4 nilikuwa naongoza nikishuka sana nakuwa mtu wa pili au wa tatu.Kifupi nilizaliwa nikiwa na akili sana pia nilikuwa na nyota ya kupendwa na watu na nililelewa kwenye mazingira mazuri nikiheshimu kila mtu. Tatizo hili lilinianza nilipokuwa shule ya msingi yaani nilipofika std 7. Nilikuwa napita karibu na mto na kuna mti mkubwa.Nilihisi nywele kusisimka na nikawa kila nikipita hapo naokota pesa. Tabia hiyo iliendelea kila siku mpaka jamaa na wazazi wakawa wananiambia nawaibia na kusingizia naokota.Mpaka namaliza std7 nilikuwa sijawahi kutana na mwanamke.Nilipofika form 2 nikibalehe bt hapo ndipo nilipoanza hisi utofauti.Nilianza kupata wet dream ila nilijua ni kawaida kama mwalimu wa biology alivyotufundisha bt cha kushangaza ndoto hizo zilikuwa ni endelevu.Mwaka huo huo nilipata dada mmoja akawa mpz wangu ila nilipokuwa namdu sikuwa nahisi raha kama ambavyo naota.Pia nikaanza tabia ya uongo, uchonganishi, unafki, hasira pia nikawa nachukiwa na wanafunzi na hata walimu bila sababu. Nilipomaliza form 4 nilifaulu kwenda A level pindi hko nilikuwa na mwanamke m1 ambae alikuwa na mimba yangu bt cha kushangaza ile mimba ilitoka kwa mazingira ya ajabu. Nilipofika A level nikawa na tabia ya kujichua na kupenda wanawake kupitiliza.Nilikuwa natoroka shule na kutafuta wanawake kuanzia mabaamedi, mama guest mpaka wanaojiuza nikikosa napiga punyeto huku na zile tabia zingine zikiendelea. Nilienda chuo kikuu k1 moro na kuendeleza hizo tabia mpaka nilipomaliza chuo na kuanza kazi arusha.Wakati nilipokuwa chuo nilimtia dada m1 mimba ila pia mtoto alifia tumboni bila sababu. Nikiwa kazini arusha mabosi na wafanyakazi wenzangu wakawa wananichukia bila sababu mwisho nikafukuzwa. Siku 1 nikiwa arusha wakati nimefukuzwa kazi nikaenda kanisa la safina.Nilijishangaa nilipopandisha mashetani baada ya maombezi na kuanza ku confess na hayo mashetani yakasema yote tangu kuniingia mpaka walivyosababisha kuua watoto wangu pia kunisababishia UKIMWI, kuchukiwa, kutopata maendeleo mi na familia yangu yote. Nilimshukuru mungu na kuanza maisha mapya ya maombi ila sasa kuna lingine limeibuka.Nikipitiwa na kulala bila kusali huwa naingiliwa sana kinyume na maumbile nikiamka najikuta nimechafuka.Nguo zangu za ndani zinachafuka sana.Nateswa na haya majini natamani kujiua husasani kwa vitendo ninavyofanyiwa pia mi ni muathirika bila kupenda.Nimechoka na maisha haya sijui nitafanyaje?Mnanishaurije wana jf?Natamani nikipata pesa niende nigeria kwa tb joshua kwa ajili ya maombezi.Naombeni ushauri wenu. Source:Jamii Forums |
MESSAGE ZA KIKWETE KUMUUZIA OBAMA NCHI SAWAFIKISHA WAT WAWILI POLISI Posted: 12 Jul 2013 09:52 PM PDT Jeshi la polisi Geita linawashikilia watu wawili kwa kosa la kusambaza ujumbe kwa njia ya simu usemao, UMEPOKEA SHILINGI 50,000.KUTOKA KWA RAIS KIKWETE KAMA SEHEMU YA MGAO WAKO BAADA YA KIKWETE KUMUUZIA OBAMA NCHI!!
Kamanda wa polisi mkoani hapo alisema kwamba watu hao walikamatwa baada ya kukutwa msg hizo ktk simu zao za mikononi huku wakiwa wanasambaza kwa watu wengine. Aliendelea kudai kua jeshi la polisi linatoa onyo kwa wale wote wanaowachafua viongozi wa kitaifa kwa njia za ujumbe kwa simu na kwamba watawachukulia hatua kali. Source; Radio Free Afrika Matukio! |
Udaku Specially |
WALIOMRUHUSU MASOGANGE APITE NA 'UNGA' AIRPORT NI HAWA! Posted: 13 Jul 2013 10:50 PM PDT HAKUNA sababu ya kumkamata ‘mchawi’ kwenye skendo ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ kudaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini wakati ukweli upo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Watu mbalimbali ambao wamesoma sakata hili kwenye vyombo vya habari, walitoa maoni yao wakisema kuwa watu wanaotakiwa kuwajibishwa ni waliokuwa uwanjani hapo siku Masogange aliposafiri na kuruhusu mizigo ya mrembo huyo na mdogo wake, Melisa Edward ipite bila ukaguzi makini. “Kuna uwezekano kabisa wa kuwajua watu hao,” alisema msomaji wetu, Mbande Kinaka, mkazi wa Kariakoo, Dar. Risasi Jumamosi lilimtafuta Mkuu Kitengo cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Kamanda Godfrey Nzowa, alipopatikana na kuulizwa namna ya kuwabaini waliomruhusu Masogange akapenya na mzigo airport, alisema lazima watawapata. Taarifa tulizozipata zinasema Agnes na mdogo wake Melisa Edward waliondoka nchini Julai 5, mwaka huu kwenda Afrika Kusini. |
TEAM YA TAIFA STARS MGUU NJE, NDANI CHAN Posted: 13 Jul 2013 10:47 PM PDT Mfupa wa Waganda bado mgumu kwa Taifa Stars. Ni baada ya jana timu hiyo ya Tanzania kushindwa kufurukuta mbele ya wageni wao kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu kushiriki fainali za Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) kufuatia kipigo cha bao 1-0.
Kwa matokeo hayo, Stars inahitaji miujiza kushinda mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo kwenye uwanja ambao utaamuliwa baadaye na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kati ya Namboole au Nakivubo. Katika mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa, Taifa Stars ilitawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza na kuwapa wakati mgumu Uganda, lakini cha kusikitisha ni washambuliaji wake kukosa magoli yasiyo na idadi. Bao pekee la Uganda lilifungwa dakika ya 46 kupitia kwa Iguma Dennis aliyemfunga kipa Juma Kaseja kwa shuti la pembeni ya lango akimaliza pasi ya shambulizi la kushtukiza kutoka kwa Mpande Joseph. Kwa matokeo hayo, Stars inaendelea kuwa mteja wa The Cranes, na sasa ili isonge mbele itahitaji ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya marudiano. Washambuliaji, John Bocco, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa waliinyima Stars mabao mengi ya hasa kipindi cha kwanza walichotawala sehemu kubwa ya mchezo. Uganda waliokuwa wakitumia nguvu nyingi kufika lango la Stars, hawakupata nafasi nyingi za kufunga, lakini nafasi moja waliyoipata ambayo haikuonekana kuwa ya hatari, ndiyo iliyowapa bao pekee. Stars walikuwa wa kwanza kupiga hodi lango la Uganda dakika ya kwanza, baada ya krosi ya John Bocco kushindwa kuunganishwa wavuni na Amri Kiemba aliyekuwa kiasi cha mita tano kutoka langoni.Mrisho Ngassa aliyekuwa akiwakimbiza vizuri Waganda, alifanya makosa kama ya Kiemba baada ya kushindwa kutikisa nyavu dakika ya 20 kufuatia pasi ya Bocco, ambaye naye dakika moja kabla alikosa bao la wazi. Taifa Stars waliendelea kuwanyong’onyesha mashabiki wake baada ya kushindwa kufunga kupitia kwa Bocco katika dakika 21 na 23, na baadaye dakika tatu Ngassa naye alikosa bao la wazi. Shambulizi kubwa la The Cranes lilikuja dakika za 30 na 39, ambapo wangeweza kufunga mabao kama siyo nafasi hizo kupotezwa na Edema Patrick. Pamoja na Kocha wa Stars, Kim Poulsen kusema bado kuna nafasi ya kushinda mchezo wa marudiano na kufuzu kwa michuano hiyo, matumaini ni kidogo. Akitetea wachezaji wake kupata nafasi nyingi na kushindwa kufunga, Kim alisema: “Katika soka kukosa mabao ni jambo la kawaida, bado tunaweza kushinda kwenye mchezo wa marudiano.” Kocha wa Uganda, Sredojevic “Micho” Milutin alisema wachezaji wake walicheza kwa kujituma na ndiyo maana wakapata ushindi ugenini. |
KUMBE:MAMA NTILIE USWAHILINI WATUMIKA KUUZA MADAWA YA KULEVYA Posted: 13 Jul 2013 10:43 PM PDT Biashara ya dawa za kulevya nchini inazidi kuchukua sura mpya ambapo sasa wanawake wanaouza vyakula, maarufu mama ntilie, hutumika kusambaza dawa hizo kwa wateja.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa muda mrefu katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam unaonyesha kuwa biashara hiyo inafanyika katika maeneo ya Tandika, Manzese, Vingunguti, Temeke, Tandale, Mtongani na Keko. Wanawake hao wamekuwa wakitumia mwanya wa kuuza chakula kama kinga yao, huku biashara yao kubwa ikiwa ni kuuza dawa za kulevya aina ya heroin, bangi na aina nyingine. Mbinu hii mpya ya usambazaji wa dawa za kulevya kwa kutumia wanawake wanaouza vyakula imeelezwa kuwa inawasaidia wahusika wakuu, kuendesha biashara yao kwa ufanisi zaidi. Uchunguzi umeonyesha kuwa wafanyabiashara wa dawa hizo wameamua kuwatumia mamalishe kutokana na kuwa waaminifu na kuhudumia wateja wengi, hivyo ni vigumu watu kuwashtukia wakiwamo askari polisi. Imebainika kuwa dawa hizo huuzwa kulingana na maeneo, wakati maeneo ya watu wasiokuwa wa uwezo hupimwa kwa kutumia kipimo kidogo zaidi kwa bei ya chini ambayo watumiaji husika huweza kuimudu. Aidha dawa hizo hufungwa katika mitindo miwili tofauti, ukiwa katika unga wa vidonge na wa kawaida ingawa bei zake hazitofautiani sana. Uchunguzi unaonyesha kuwa vidoge huuzwa vikiwa vizima au vipande, huku unga wa kawaida ukiuzwa kwa kipimo maalumu. Kwa kawaida ‘unga’ huo huuzwa kwa Sh1,000 kwa pointi huku kete moja ikiuzwa kwa Sh2,000, wakati vidonge, kizima huuzwa kwa Sh2,000, huku kipande huuzwa kwa Sh1,000 zikitofautiana kulingana na maeneo. Gazeti hili lilifanikiwa kuongea na baadhi ya wanawake wanaojihusisha na uuzaji wa dawa hizo. Dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Asha (28) ambaye siyo jina lake halisi ni muuzaji mkubwa wa dawa hizo. Awali alikuwa akifanya shughuli zake hizo za uuzaji katika maeneo ya Yombo Kilakala, ingawaje hivi sasa amehamia Temeke. “Unajua siku zote dhumuni la kufanya biashara ni kupata faida, hivyo naweza kusema niliingia kwenye biashara hii kwa sababu tu ina faida zaidi kuliko biashara nyingine,” anasema. |
MASKINI:WANAJESHI SABA WA TANZANIA WAUWA DARFUR Posted: 13 Jul 2013 10:35 PM PDT Dar es Salaam. Wanajeshi saba wa Tanzania, ambao ni miongoni mwa kikosi cha Umoja wa Mataifa, cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanadaiwa kuwa wameuawa. Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilisema kwamba wanajeshi hao wa Tanzania, wamekufa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali. Kwa mujibu wa taarifa hizo, miili yao wanajeshi hao bado ipo nchini Sudan ikisubiri taratibu za kusafirishwa kuletwa nchini. Hii ni mara ya kwanza kuripotiwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kufa kwa wakati mmoja. Agosti mwaka jana wanajeshi watatu wa Tanzania huko Darfur waliripotiwa kuuawa kwenye tukio kama hilo. Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Kanali Kapambala Mgawe alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi. Hii ni mara ya pili kwa wanajeshi wa Tanzania kuuawa katika Jimbo la Darfur, ambapo Agosti mwaka jana, Kanali Mgawe alinukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea kwa vifo vya askari watatu ambao gari lao lilizolewa na maji walipokuwa wakivuka mto uliokuwa umefurika maji. Kanali Mgawe aliwataja askari hao kuwa ni Sajini Julius Chacha, Sajini Anthony Daniel na Koplo Yusuph Said na kwamba askari wengine walinusurika baada ya kuogolea. Tanzania ina askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani jimbo la Darfur, ambao ni sehemu ya askari 1,081 wa kulinda amani katika jimbo la Darfur. Wanajeshi hao wa Tanzania wametawanywa kwenye miji ya Khor Abeche na Muhajeria kusini mwa Darfur. Aprili mwaka huu Tanzania ilipeleka wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kupambana na kikundi cha waasi wa nchi hiyo M23 kinachopigana kuiangusha serikali ya DRC. Majeshi ya Tanzania yalipelekwa kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa. Tanzania inaungana na nchi za Afrika Kusini na Malawi kukamilisha kikosi cha wanajeshi 3,000. Tanzania imepeleka wanajeshi 850. |
Udaku Specially |
DIAMOND DENIES HAVING ANY BEEF WITH PREZZO-LISTEN TO HIM HERE Posted: 15 Jul 2013 09:17 AM PDT Today, Mzazi Willy M. Tuva was on air on his wildly popular radio show Mambo Mseto and he sought to get to the bottom of the issues between Prezzo and Diamond if indeed there was one. and he tried to call Prezzo but the President wasn't picking up. So he instead reached out to Diamond Platinumz and Diamond said that he had no problem with Prezzo and he was unaware of the existence of bad blood between the two of them and went as far as saying he respects the lad.Check out the sound clip below: |
HAYA NDIO MAJINA NA PICHA ZA WANAJESHI WA TANZANIA WALIOKUFA KATIKA MAPAMBANO NA WAASI DARFUR SUDAN. Posted: 15 Jul 2013 09:05 AM PDT Askari hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan ni :- (1.) Sajenti Shaibu Othuman, (2.) Koplo Oswald Chaula, (3.) Koplo Mohamed Juma, (4.) Koplo Mohamed Chikilizo, (5.) Pte. Rodney Ndunguru, (6.) Pte. Peter Werema, (7.) Pte. Fortunatus Msofe. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao (ambaye hakutajwa) ambaye alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi nchini humo. Wakati wakijiandaa, ghafla walizingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa. Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina. Picha na habari : JF |
KWA MWENENDO HUU, TAIFA STARS ITAFUNGWA KILA SIKU MPAKA MABADILIKO YAFANYIKE…..! Posted: 15 Jul 2013 06:43 AM PDT KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, maarufu kama Taifa Stars juzi kilipoteza mechi yake ya kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Uganda, The Cranes kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kabla ya mchezo huo, matarajio ya wengi yalikuwa ni Taifa Stars kuibuka na ushindi kutokana na muonekano wa mechi yenyewe na rekodi ya Taifa Stars kwa siku za hivi karibuni. Sasa matumaini ya Taifa Stars kucheza CHAN ni madogo mno kulinganisha na hali ilivyokuwa hapo awali. Hii ina maana, Taifa Stars inatakiwa kupata ushindi usiopunguwa bao 1-0 kwenye mechi ya marudiano itakayochezwa wiki mbili zijazo kwenye Uwanja wa Namboole huko Uganda. Mengi yalitokea katika mchezo wa jana, ambao uliwatoa vichwa chini Watanzania wengi waliodhani timu yao ingeweza kufanya vizuri baada ya hivi karibuni kuwa na matokeo ya kuridhisha. TAIFA STARS ILIWAKOSA WAWILI, UGANDA ILIWAKOSA KUMI….LAKINI BADO MAMBO YAKAWA MAGUMU KWAO Taifa Stars iliingia uwanjani ikiwa imewakosa wachezaji wake wawili tu wa kikosi cha kwanza kutokana na kanuni kuwabana, nao ni Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya DR Congo. Samatta na Ulimwengu hawakuweza kucheza mechi hiyo kutokana na ukweli kwamba, hiyo ni michuano maalum kwa wachezaji wa ligi za ndani ya nchi pekee. Shirikisho la Soka Afrika, CAF lilianzisha michuano hii ili kutoa fursa kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani za nchi zao nao kuonekana na kutoa michango yao kwa timu zao za taifa ambazo mara nyingi zilikuwa zikisheheni wachezaji wanaocheza nje ya Afrika. Wachezaji wanaocheza ligi za ndani katika nchi kama Nigeria, Ivory Coast na Senegal, huwa hawapati nafasi ya kucheza michuano ya aina yoyote katika vikosi vya nchi hizo ambavyo husheheni idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya Afrika hasa Ulaya. Kwa kutambua hilo, CAF ikaamua kuanzisha michuano hii ya CHAN ambayo Tanzania imeshiriki mara moja na Uganda pia imeshiriki mara moja. Kwa kutaka michuano hii ichezwe na timu kutoka pande zote za Afrika, CAF ikawa inahakikisha kila pembe ya Afrika inashiriki michuano hii, ndiyo maana leo Tanzania na Uganda zinawania nafasi ya kufuzu kucheza fainali hizo. Wakati Taifa Stars ikiwakosa wachezaji wawili tu, Uganda iliwakosa wachezaji kumi (10) ambao mara nyingi huwamo katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Hii ina maanisha Uganda ilikuwa na wachezaji wawili tu wa kikosi cha kwanza kinachojumuhisha hata nyota wanaocheza nje ya Uganda. Wachezaji wa Uganda waliocheza mechi ya jana ambao mara nyingi huchezea timu ya taifa ni Hamza Muwonge na Hassan Waswa ambaye jana alikuwa nahodha. Wengine wote waliocheza jana, huwa hawana nafasi katika kikosi cha Uganda. Kazi ipo. TANZANIA LIGI DUNI, UGANDA LIGI BORA…. Kwa matokeo ya mechi ya jana, imedhihirika wazi kwamba Ligi Kuu ya Tanzania Bara, haina ubora kulingana na ile ya Uganda. Wachezaji wengi wa Taifa Stars hawakuweza kucheza vizuri mbele ya wenzao wa Uganda walioweza kutawala na kucheza kwa malengo katika eneo la kiungo kwa muda mwingi. Kabla ya mchezo ilionekana wachezaji wa Tanzania wangeweza kuwapiku wa Uganda lakini muda mfupi baada ya mchezo kuanza, ubora wa wachezaji wa Uganda ulikuwa ukitawala kila mara. Viungo kama Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa na Mwinyi Kazimoto hawakuweza kuwa imara na kuisaidia timu. Bado wachezaji hao wanacheza na majukwaa huku wakipoteza malengo ya timu mara kwa mara hasa kwa kukariri mfumo wa kucheza pasi za nyuma wakati timu ikipanda, na hata uanzishwaji wa mipira mara nyingi umekuwa ule ule, kwamba mpira anaanziwa Aggrey Morris au Kelvin Yondani halafu utaenda kwa Erasto Nyoni, naye ataupeleka kwa Sure Boy halafu Sure Boy anaupeleka kwa Shomari Kapombe au unarudi tena kwa Morris ambaye ataupiga juu katikati halafu John Bocco atashindana nguvu na mabeki wa Uganda kisha anaupoteza halafu kazi ya kukaba inaanza. Kwa mchezo wa jana wa Taifa Stars, hakika kila siku tutalia kama hatutakubali kufuata yafuatayo; KUREKEBISHA MFUMO WA SOKA TANZANIA… Timu zote tunazocheza nazo kisha zikatufunga, ukizitazama utagundua zina mfumo wa kuopoa vipaji vya wachezaji wake, hasa kuanzia ngazi ya shule za msingi, sekondari hata katika vyuo vikuu. Mtazame mfungaji wa bao pekee la Uganda, Dennis Guma huyu anatokea timu ya Victoria University ambayo pia inashiriki Ligi Kuu ya Uganda. Timu hii ina timu kibao za watoto wadogo ambao wanapitia katika mfumo mzuri wa soka na hata kupata elimu ya dunia kwa pamoja. Leo hii wachezaji wengi kutoka Kenya au Uganda mpaka wanapofikia hatua ya kucheza Ligi Kuu wengi wao ni agharabu kuwakuta na elimu chini ya kidato cha nne au kidato cha sita kutokana na mfumo wao wa elimu dunia na ile ya michezo hasa soka. Siwakosoi kwa kutokuwa na elimu, lakini utawasikia wameshindwa kuendelea na elimu ya sekondari kutkana na matatizo ya kifamilia. Academy nyingi za nchi hizo, zinawapa fursa wachezaji kupata elimu zote hizo (soka na elimu ya darasani) kwa pamoja na ndiyo msingi wa mafanikio yao leo hii. Hao wanakua kiakili huku wakijua namna ya kupokea mafundisho. Hapa kwetu leo hii kitazame kikosi cha Taifa Stars, kisha omba rekodi za walipotokea wachezaji wake halafu uliza kuhusu elimu zao, utashangaa, lakini ndiyo aina ya wachezaji tulionao. Tufanyeje? Hakuna jinsi. Wachezaji wengi wa Taifa Stars hawajulikani wanapotokea, unashtukia mtu anacheza Simba, Yanga au Azam au hata timu nyingine ya ligi kuu bila hata ya kucheza mechi moja ya ligi daraja la tatu au ile ligi ya taifa. Sasa huyu atawezaje kupambana na mtu aliyepitia mfumo sahihi wa soka? Huu ni utani. Siyo siri, Taifa Stars inaundwa na wachezaji wengi wa Simba, Yanga na Azam, lakini ni Azam pekee yenye mfumo mzuri wa usajili wa wachezaji kwa kuwa na academy yake inayozalisha wachezaji kila siku. Hizo Simba na Yanga bado zina mfumo wa kuita lundo la wachezaji katika mazoezi yao na kutazama uwezo wao kisha kuwasajili. Sipo hapa kuisifia timu fulani au kuiponda timu nyingine, natoa machungu yangu ya rohoni kutokana kuumizwa na kipigo cha jana cha Taifa Stars dhidi ya Uganda iliyoonekana kuwa dhaifu pengine kuliko hata kikosi cha Taifa Stars. KUKOSEKANA MAKOCHA WENYE UWEZO NALO NI TATIZO LETU… Lazima tukubali kwamba, Tanzania ina tatizo la makocha wenye uwezo wa kufundisha hasa vijana wadogo. Hata kama leo hii serikali ya Tanzania itakubali kubadili mtaala wa elimu yake na kuruhusu soka kuingia ndani yake. Tunaweza kupata tatizo la ukosefu wa makocha. Kuna haja ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wadau wengine wa soka kujitolea kuwafundisha makocha wa timu za watoto ili wawe wengi watakaoweza kutoa elimu stahiki kwa watoto. Leo hii utazunguka mitaani na kukuta watoto wanafundishwa na kocha wao, lakini ukimchungumza kocha huyo utagundua anafanya kazi hiyo kwa utashi wake tena kwa kujitolea huku akikosa elimu hata ya msingi ya ukocha. Hivi hapo unategemea kupata mchezaji bora? Hakuna. Kozi zinazotolewa na TFF lazima zitazame hali halisi ya uwezo wa mtanzania, kwamba kozi inaletwa na kuwataka washiriki kuchangia kiasi cha fedha, basi kisiwe kingi kiasi cha kuwafanya wengine kutomudu kulipia kwani udhamini wakati mwingine unakuwa mgumu. HITIMISHO…… NI LAZIMA TUFE ILI TUFIKE PEPONI…..! Kwa vyovyote vile, ni lazima mambo ya msingi yafanyike katika mfumo wa soka la Tanzania ili kuiletea mafanikio nchi hii katika soka, nje hapo tutakuwa tunaimba nyimbo zisizo na muitikiaji kila siku. Mafanikio hayatakuja. Lazima TFF na klabu za soka za Tanzania zikubali kuendesha soka kitaalam na siyo kibabaishaji kama ilivyo leo, pia ziwepo program zitakazokuwa zinafanya kazi kikamilifu na siyo zipo zipo tu kama geresha. SOURCE:SHAFII DAUDA |
CHADEMA YAIVURUGA VIBAYA CCM UCHAGUZI WA MADIWANI ARUSHA Posted: 15 Jul 2013 06:38 AM PDT Arusha. Chadema kimethibitisha umwamba wake katika siasa za Jimbo la Arusha Mjini, baada ya kutetea kwa kishindo kata zake nne kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana. Katika uchaguzi huo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na ambao ulichukuliwa kama kipimo cha siasa za Arusha ambazo zimekuwa na mvutano mkubwa, Chadema kiliongoza katikia vituo vyote 136 vya kupigia kura Kata za Elerai, Kaloleni, Kimandolu na Themi. Kata hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011 baada ya Chadema kuwatimua wanachama wake waliokuwa madiwani Estomih Mallah(Kimandolu), John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda (Kaloleni). Matokeo Katika matokeo yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Kata ya Elerai, Obedi Meng’oriki mshindi alikuwa Jeremiah Mpinga wa Chadema aliyepata kura 2,047 dhidi ya 1,471 za Emmanuel Laizer wa CCM. Katika Kata hiyo kulikuwa na wagombea wengine ambao ni John Bayo (CUF; kura 302), Seif Shimba (CCK; kura 3) na Boisafi Shirima (TLP;1). Katika Kata ya Themi, Kinabo Edmund wa Chadema aliibuka na ushindi baada ya kupata kura kupata kura 674. Msimamizi wa Uchaguzi Kata hiyo, Ezeka Mboya alisema Kinabo alifuatiwa na Victor Mkolwe aliyepata kura 326 na Lobora Ndarpoi wa CUF alipata kura 307. Kata ya Kaloleni, Msimamizi wa Uchaguzi, Anna Ledisa alimtangaza Kessi Lewi wa Chadema kuwa mshindi kwa kura 1,470 dhidi ya Emmanuel Mliari wa CCM aliyepata kura 330 na Abbas Mkindi wa CUF aliyepata kura 275 na Ngilishi Pauli wa Demokrasia Makini aliyeambulia kura mbili. Kata ya Kimandolu, Msimamizi wa Uchaguzi, Suleiman Kilingo alimtangaza Mchungaji Rayson Ngowi wa Chadema kuwa mshindi kwa kura 2,761 na kumshinda Edna Saul wa CCM aliyepata kura 1,163. Kwa matokeo hayo, Chadema sasa kimefikisha madiwani 12 wakati CCM kimebakiwa na kumi na moja na TLP kina wawili. Ushindi huo wa Chadema una athari kwa nafasi ya Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo kwani CCM kina wajumbe 14 tu kwenye Baraza la Madiwani, TLP wawili wakati Chadema sasa kimefikisha 15. Wabunge wa majimbo na wale wa viti maalumu pia ni madiwani. Aidha, Chadema kina nafasi ya kuongeza kiti kingine cha udiwani kwani Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kinatarajiwa kuitisha uchaguzi mdogo Kata ya Sombetini. Mkurugenzi wa NEC, Julius Malaba alimwambia mwandishi wetu kuwa tume yake inatarajia kuitisha uchaguzi mdogo hivi karibuni baada ya kata hiyo kutangazwa wazi na Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi. Malaba alisema uchaguzi huo utaitishwa baada ya aliyekuwa Diwani wake, Alphonce Mawazo kujitoa CCM na kujiunga na Chadema hali inayokifanya chama tawala kuwa katika wakati mgumu kukitetea kiti hicho. |
MAMA AMCHOMA MWANAWE MCHANGA MARA 90 KWA MKASI KISA ETI ALIMG'ATA ZIWA WAKATI WA KUNYONYA Posted: 15 Jul 2013 05:20 AM PDT Ni kama miujiza kwa mtoto wa kichina kuwa hai mpaka sasa licha ya kuchomwa chomwa mara 90 na mama yake mzazi huko China kwa madai kuwa alimng’ata ziwa mama yake wakati akinyonyeshwa.
Kwa mujibu wa Daily Mail mtoto huyo Xiao Bao mwenye miezi 8 tu ameshonwa zaidi ya nyuzi 100 ili kuurudisha uso wake katika hali nzuri baada ya shambulizi hilo lililotokea katika jiji la Xuzhou mashariki mwa China. Bao anaishi na mama yake pamoja na wajomba zake wawili ambao wanajishughulisha na ukusanyaji wa taka kwaajili ya kipato. Mmoja wa wajomba hao ndiye aliyegundua kuwa Bao ameumizwa baada ya kumkuta akiwa amelala kwenye damu iliyotapakaa nyumbani hapo kabla hajamkimbiza hospitali Mama wa mtoto huyo baadaye alikiri kumchoma choma mwanae na mkasi mara 90 hususan eneo la usoni baada ya mtoto huyo kumng’ata ziwa wakati akimnyonyesha. Baada ya tukio hilo majirani wa familia hiyo wameiomba serikali imnyang’anye mama huyo wa kichina mtoto kwa sababu za kiusalama, lakini ombi hilo limekataliwa kwa madai kuwa hakuna uthibitisho wowote mpaka sasa kama mwanamke huyo anamatatizo ya akili, lakini wameongeza kuwa hata hivyo mtoto huyo bado ana walezi wengine wawili anaoishi nao (wajomba zake) Mtoto huyo anaendelea kupata nafuu akiwa hospitali. Source:Bongo 5 |
MTOTO ABAKWA NA KUWEKWA MIWA SEHEMU ZA ZILI MPAKA KUFA...!!! (+18) Posted: 15 Jul 2013 04:39 AM PDT Vanusia Silva Pereila mdada mwenye miaka 9 mkazi wa kijiji kimoja nchini brazil,mapema wiki hii amebakwa karibu na shamba la miwa na watu wanaoaminika kuwa ni watumiaji wa madawa ya kulevya. MAELEZO ZAIDI KUTOKA CHANZO CHA HABARI HII HAYA HAPA. The horrific crime happened in Arataca, state of Bahia, Brazil. Vanusia Silva Pereira was taken to a vacant lot, punched in the face, raped and then had a sugar cane forced up her snatch. The victim’s father, identified as Mr. Wilson, an agricultural laborer told police that Vanusia chose bad company to hang out with lately and that was her demise. Police do not suspect that her murder was a crime of passion, however coroner who examined the body said the woman had been subjected to exceptional violence before death which brought the possibility of this being the crime of passion back into question. |
WEMA: SIACHI MKOROGO HADI MADUKA YAFUNGWE Posted: 15 Jul 2013 12:17 AM PDT THE big boss wa The Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu ametundika mtandaoni picha zinazoonesha mapaja yake jinsi yalivyoharibika na kuweka michirizi ambapo alipoulizwa na shushushu wetu kulikoni, alisema kuwa hataacha mkorogo hadi maduka yafungwe.
Wema katika pozi linaloonesha mapaja yake jinsi yalivyoharibika. Baada ya staa huyo wa filamu za ‘kikwetukwetu’ kuulizwa na kujibu hivyo wikiendi iliyopita, alitundika picha nyingine kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa BBM zikimuonesha akiwa nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar huku madhara ya mkorogo yakionekana waziwazi kwenye mwili wake...Mapaja ya mrembo huyo. Baadhi ya marafiki zake walianza kujadili namna alivyoharibika na wengine kudai matumizi ya vipodozi vikali maarufu kwa jina la mkorogo ndiyo vimemfanya apasuke kiasi hicho.Wema, baada ya kupokea maoni mengi juu ya picha hizo mengine yakiwa ni ya kejeli, aliwajibu kwa kuandika kuwa hataacha matumizi ya mkorogo hadi maduka yanayouza yafungwe. Wema alipotafutwa na gazeti hili ili aweze kuweka wazi madai haya hakutoa ushirikiano kufuatia simu yake ya kiganjani kuita muda wote bila kupokelewa. Source:Global Publisher |
UKWELI KUHUSU BINTI KIZIWI KUNYONGWA CHINA BAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA HUU HAPA Posted: 15 Jul 2013 12:14 AM PDT MTANDAO wa wauza madawa ya kulevya unazidi kupukutika Bongo kufuatia madai ya kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kujishughulisha na ubebaji ‘punda’ wa biashara hiyo haramu, Ijumaa Wikienda lina mtiririko wote.
Hivi karibuni, Video Queen wa Wimbo wa Masogange, Agnes Gerald ‘Masogange’ amedaiwa kunaswa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ akiwa na kilo mia moja na hamsini za unga unaoaminika ni sehemu ya madawa ya kulevya. Ameshapanda kortini mara moja Ijumaa iliyopita. Wakati Masogange akisota Sauzi kwa madai hayo mazito, habari ya mjini kwa sasa ni ya mtalaka wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Mohammed ’Z-Anto’, Sandra Khan au Binti Kiziwi kudaiwa kutupwa jela miaka mitano kwa sakata la ‘unga’. HABARI YA MJINI KWA SASA NI BINTI KIZIWI Kuanzia Alhamisi iliyopita, habari zilizoligubika Jiji la Dar ni kuwa Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya. Kwa mujibu wa mitandao, Binti Kiziwi alinyongwa wiki mbili zilizopita. Hata hivyo, mitandao hiyo haikusema kama mrembo huyo alinyongwa hadi kufa au la! Sheria za hukumu hiyo, mwenye hatia anatakiwa kunyongwa hadi kufa. UKWELI WA BINTI KIZIWI NI HUU Baada ya kusambaa kwa manenomaneno hayo, Ijumaa Wikienda liliingia mtaani kuisaka familia ya Binti Kiziwi lakini bila mafanikio. Kwenye makazi ya mama yake, Buguruni, Dar, majirani walisema mzazi huyo amehama baada ya kufunga ndoa siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. IJUMAA WIKIENDA LAZIDI KUCHIMBA Ijumaa Wikienda lilizidi kuzama ndani katika kuchimbua tetesi hizo ambapo lilifanikiwa kumpata ndugu wa kiume wa Binti Kiziwi na kufanya naye mazungumzo kama ifuatavyo: Wikienda: Samahani, nimeambiwa wewe ni ndugu wa Binti Kiziwi, ni kweli? Ndugu: (huku akitaja uhusiano wao) Ni kweli, nikusaidie nini? Wikienda: Kuna manenomaneno kwamba Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya, ni kweli? Ndugu: Sijui hizo habari watu wanazipatia wapi?! Watanzania wana maneno sana. Si kweli ndugu mwandishi. Wikienda: Ukweli ni upi? Ndugu: Kwanza kabisa Binti Kiziwi hakukamatiwa China, alikamatiwa Hong Kong, kwa sheria za kule mtu akipatikana na hatia ya kukutwa na ‘unga’ anahukumiwa jela tu. “Binti Kiziwi amehukumiwa miaka mitano jela Hong Kong, na si China. Watu wajue hilo na miaka mitano si mingi, atatoka.” Wikienda: Nashukuru sana kwa ushirikiano ndugu yangu. Ndugu: Asante, waambie Watanzania waache kuongeaongea sana. |
WOLPER: MADAHA HANA LOLOTE ANATAFUTA ‘KIKI’ TU KUPITIA KWANGU Posted: 15 Jul 2013 12:08 AM PDT STAA wa sinema za nyumbani, Jacqueline Wolper amemtemea cheche msanii mwenzake, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ kuwa anatafuta ustaa (kiki) kupitia jina lake
Akifafanua kauli yake mbele ya kinasa sauti cha Stori 3, Wolper alisema anamshangaa msanii huyo kumsemea vibaya, kutoa lugha ya matusi mtandaoni bila sababu za msingi “Namshangaa Baby Madaha kwa aliyoyasema kuhusu mimi, anatafuta kiki. Watu wanafahamu mimi ni staa kuliko yeye kwa hiyo sidhani kama ana sababu ya kugombana na mimi,” alisema Wolper. |
CHADEMA NOMA:YASHINDA UCHAGUZI KATA ZOTE NNE ARUSHA Posted: 15 Jul 2013 12:00 AM PDT Uchaguzi uliofanyika jana Jumapili, Julai 14, 2013 wa kuwapata madiwani wa Kata Nne --Themi, Kaloleni, Kimandolu na Elerai-- za mkoani Arusha umemalizika.
Huku Tume ya Uchaguzi ikisubiriwa kuwatangaza rasmi washindi, taarifa za awali zinasema kuwa CHADEMA imepata ushindi kwa kunyakua Kata zote Nne kama ifuatavyo: KATA YA THEMI: CHADEMA 678; CCM 326; CUF 313 KATA YA KIMANDOLU: CHADEMA 2,665; CCM 1,169 KATA YA KALOLENI: CHADEMA 1,019; CCM 389; CUF 169 KATA YA ELERAI: CHADEMA 1,715; CCM 1,239; CUF 213 Vyama vingine vilivyoshiriki vilikuwa ni TLP, CCK na Demokrasia Makini. |
UPDATE: MATOKEO YA UCHAGUZI KATIKA KATA NNE ZA ARUSHA. Posted: 14 Jul 2013 11:44 PM PDT |