Ben Komba/Pwani-Tanzania/17-10-2021
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu wanane kwa kosa la kumshambulia Polisi na kuharibu mali kufuatia ajali iliyotokea eneo la Kwa Mathias mjini Kibaha
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Kamishna Msaidizi, WANKYO NYIGESA amesema watu hao wanane wakitumia mawe na vitu vigumu, walimshambulia Askari wa Usalama Barabarani aliyefika eneo kufuatia Basi la SAULI kuigonga bodaboda na kusababisha kifo cha abiria aliyepakizwa EMMA NGOLE na majeruhi ambaye ni dereva wa bodaboda, BW. EDWIN MWENDA.
Watu hao ambao wanasadikiwa kuwa ni bodaboda walianza kwa kulishambulia kwa mawe, Basi lililosababisha ajali hiyo ya SAULI yenye namba za usajili T 668 DCF Gari aina ya SCANIA lililokuwa lianaendeshwa na BW. TITO GADAU, likitokea Mbeya kwenda DAR ES SAALAM.
Kamanda WANKYO amesema sababu ya ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi kulipita bila kujali gari lililokuwa limesimama na matokeo yake kugongana uso kwa uso na pikipiki iliyokuwa inakuja mbele yake, aidha ametoa onyo kwa wananchi kujichukulia sharia mikononi ilihali kuna vyombo vyenye jukumu hilo.
END