Ben Komba/Pwani-Tanzania/19-02-2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, SAMIA SULUHU HASSAN, siku ya Jumatano Februari 23 atafanya ziara ya kikazi kuzindua Chuo cha Siasa kilichopo mjini Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, ABUBAKAR KUNENGE akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha amesema ziara hiyo ina lengo la kuzindua Chuo cha Siasa katika eneo la Viziwaziwa mjini Kibaha.
Ameongeza kuwa kbala ya uzinduzi wa Chuo hicho, Katibu wa CCM, DANIEL CHONGOLO akiambatana na Makatibu wa vyama wa nchi zilizokuwa na kambi zao za kijeshi wakati wa harakati za kugombea uhuru wa nchi zilizokuwa bado zinatawaliwa na wageni........