Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-11-2021
Agizo lililotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, GEORGE SIMBACHAWENE akiwtaka wananchi wanaomiliki silaha kinyume cha Sheria kuzisalimisha silaha zao limeanza kupata mafanikio Mkoa wa Pwani, Baada ya Jeshi la Polisi kupokea Silaha kutoka wamiliki wasio halali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi, WANKYO NYIGESA amesema Silaha Zilizosalimishwa ni Magobore 21, Pistol 1 na risasi 7, rifle 2 na risasi 40 ikiwa ni kipindi cha siku 22 toka kutolewa agizo hilo.
Ameongeza Silaha hizo zimesalimishwa katika kituo cha Polisi Bagamoyo na Kituo cha Polisi Chalinze.
Amewahimiza wananchi kwa muda wa siku saba uliobaki kuzisalimisha silaha wanazomiliki kinyume na taratibu.
END