MAMA SAMIA AMWAGA FEDHA CHALINZE

5 views
Skip to first unread message

Bernard Komba

unread,
Dec 22, 2021, 1:38:45 AM12/22/21
to Startvhabari, matukio, Josephine Mwaiswaga

Ben Komba/Pwani-Tanzania/21-12-2021

Juhudi za serikali ya awamu ya sita, kufikisha fedha za miradi ya maendeleo karibu kwa wananchi, zimepata sifa nyingi kutoka kwa wadau mbalimbali wanaofuatilia utendaji wa serikali kwa karibu.

 

Diwani wa Kata ya Ubena BW.GEOFREY KAMUGISHA, akizungumza katika kikao cha halmashauri ya CCM kuelezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, ameelezea kutekelezwa kwa miradi mbalimbali kufuatia serikali kutoa fedha kwa Kata kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na maeneo mengine ya kisekta.

 

Kufuatia kupelekwa kwa fedha hizo ngazi ya Kata kumejenga Imani kubwa kutoka wananchi kutokana na kuona mabadiliko makubwa katika mgawanyo wa fedha kupelekwa karibu ya wananchi.

 

Naye mbunge wa viti maalum kutoka kwa Mkoa wa Pwani, SUBIRA MGALU amepongeza juhudi zinazonyeshwa na serikali ya awamu ya sita kutoa fedha za kutosha katika halmashauri nchini.

 

END



Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages