WAFUGAJI WATAKIWA KUTOINGIZA MIFUGO KWENYE SKIMU YA RUVU

2 views
Skip to first unread message

Bernard Komba

unread,
Oct 31, 2021, 11:59:11 AM10/31/21
to Startvhabari, matukio

 

Ben Komba/Pwani-Tanzania/31-10-2021

Serikali Mkoa wa Pwani imeazimia kukabiliana na wafugaji wanaoingiza ngombe zao katika Skimu ya umwagiliaji Ruvu kwa kutumia mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migongano kati ya jamii ya wakulima na wafugaji.

 

Mganga wa mifugo Mkoa wa Pwani akizungumza katika kilele cha wiki ya Chama cha ushirika wa umwagiliaji Ruvu wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, BW. RAMADHAN MWAIGANJU amebainisa kuwa Serikali inalitambua tatizo hilo na hatua zimeshaanza kuchukuliwa kukabiliana nayo.

 

Mwenyekiti wa Ushirika huo, BW. SADALLAH CHACHA amewaambia wafugaji kuwa hawatakiwi kuingiza Ngombe katika skimu hiyo toka wao wana maeneo yao katika Ranchi ya Taifa ya NAFCO iliyo katika eneo la Vigwaza, kitendo chochote cha kuingiza mifugo katika skimu hiyo kitachukuliwa kama uchokozi na hatua staili zitachukuliwa kwa watakaokiuka.

 

Naye Mkulima SEIF MKANA ameitaka serikali kuwalipa mishahara mizuri watendaji na wenyeviti wa vitongoji na mitaa ili waweze kuepuka vishawishi vya wenye mifugo ambao wanatumia fedha zao kuwapofusha watendaji.

 

END





Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages