Wananchi katika Kata ya Vigwaza wamemuangukia Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, SAMIA SULUHU HASSAN kuwaruhusu kuvuna mazao yao yaliyoshakomaa badala ya hatua ya dharura ya kuzuia matumizi ya Bonde la Mto Ruvu kwa shughuli za Kilimo.
Mwakilishi wa wananchi hao, Diwani wa Kata ya Vigwaza, BW.MUSSA GAMA amemuomba Rais kuangalia upya zuio kwa wananchi kutotumia Mto huo kwa shughuli za Kilimo ambapo aslimia 90 ya wakazi wa Kata ya Vigwaza wanategemea kilimo kama njia ya kujikimu na maisha kwa miaka dahari sasa.
Naye Mkazi ALLY OMARY amesema wanaiomba serikali iwaangalie kwa jicho huruma toka Askari wamekuwa wanawakataza kuvuna hata mazao yao waliyolima kabla ya marufuku kutokea ikizingatiwa wametupa nguvu zao kuandaa mashamba.
END