VITUO VYA WALEMAVU VINAHITAJIKA KILA TARAFA

3 views
Skip to first unread message

Bernard Komba

unread,
Nov 22, 2009, 1:17:41 AM11/22/09
to VOICE NEWS, MATUKIO GOOGLE
Ben Komba/Pwani/11/22/2009 8:42 AM
Kukosekana kwa shule maalum za kutosha, kumedumaza ustawi wa watoto wenye ulemavu mkoani Pwani.

Utafiti unaoendelea kufanyika wilayani Kibaha la kuwatambua watoto wenye ulemavu kuanzia miaka 0 mpaka 17, na kusimamiwa na Chama cha Albino Tanzania, Tawi la Mkoa wa Pwani kwa kufadhiliwa na PLAN,TANZANIA-KIBAHA.
Ambapo mpaka sasa imegundulika tatizo kubwa linalowakabili watoto walemavu ni kukosa huduma rafiki ambazo zingeweza kuimarisha hali yao. BW.MATTHEW CHUNGU mtaalam katika masuala ya jamii ambaye anashiriki katika utafiti huo amesema kundi la walemavu ni kundi dogo tu katika jamii hivyo ni vyema serikali ikawasaidia kwa hali na mali.

BW.CHUNGU amebainisha kwamba kumlea mtoto mlemavu kukiachiwa wazazi tu, kunanyima fursa kwa mtoto mwenye ulemavu kupata huduma stahili, na wakati serikali ina uwezo kabisa wa kuwajengea mazingira bora watoto wenye ulemavu kwa kuwajengea vituo ambavyo vitakuwa na wataalam wenye wito wa kutunza walemavu.

Ameshauri ikiwezekana kuanza kujenga vituo maalum vya kutunzia vya kutunzia watoto wenye ulemavu katika kila Tarafa ili kuweza kuyafikia makundi yote katika jamii, kwa kuyawezesha kwa kadiri ya mahitaji yao.

BW.ALLY FUNUA, Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Mwanabwito ambaye mwenyewe ni mlemavu, ameelezea kushangazwa na tabia ya watu kupita na kujifanya kutaka kutambua walemavu katika maeneo yao halafu kuwaacha bila kujua kinachoendelea, Moja ya ambao wameshapita na kuchukua majina yao ni pamoja na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha.
END.


Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages