MWANAMKE ALALAMIKA KUCHOMWA MOTO NA ALIYEKUWA MUMEWE WALIYETENGANA

4 views
Skip to first unread message

johnnygagarini

unread,
Jun 28, 2023, 11:02:56 AM6/28/23
to matukio
Polisi mkoa wa Pwani wanamsaka  Bw Elewa Mahali (53) mkazi wa Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumchoma moto na kumjeruhi mwanamke ambaye alikuwa mke wake na kumjeruhi.

Imeelezwa kuwa mtuhumiwa alimchoma mwanamke huyo Bi Dorisi Ogiro (40) anayeishi Bungo Wilaya ya Kibaha ambapo alimfuata mwanamke huyo nyumba waliyokuwa wakiishi na kumwagia mafuta na kumchoma moto mikononi na mapajani kisha kukimbia.

Kaimu kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Muhudhwari Msuya alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 23 mwaka huu majira ya saa 2 usiku ambapo mtuhumiwa huyo alifanya tukio hilo kwa kinachodhaniwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.


Kwa upande wake Bi Ogiro alisema kuwa mtuhumiwa ambaye ni dereva alifika nyumbani akiwa na mafuta ambayo alikuwa ameyaweka kwenye chupa ya maji ya kunywa kisha kuanza kuyamwaga mlangoni na kumwagia mkononi na mapajani ambapo alikimbizwa hospitali na kupatiwa matibabu na anaendelea vizuri.

 

Alisema kuwa baada ya kumwagia ambapo alitaka amwagie kichwani lakini alikwepa na kumwagikiwa mikononi na mapajani kisha akchukua kiberiti na kumchoma na kuungua hali iliyomfanya ajitahidi na kuvua nguo na kuungua kwa kiasi kidogo baada ya kufanikiwa kuuzima moto kisha kuomba msaada.


Aidha alisema kuwa walikuwa na ugomvi ambapo alimtuhumu kuwa na uhusiano na mwanaume mwingine hali iliyosababisha kuwe na ugomvi na mtuhumiwa akataka waachane na mahakama ikawatenganisha Aprili mwaka huu na kutakiwa kugawana mali ikiwemo nyumba hiyo waliyoijenga kwa pamoja.


Alibainisha kuwa hana shughuli yoyote ya kumwingizia kipato na anakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha kwa ajili ya kupata matibabu kwani tangu alipopata huduma ya kwanza hajapata tena matibabu ambapo anapata maumivu makali


Mwisho.



 



johnnygagarini

unread,
Jun 28, 2023, 11:05:20 AM6/28/23
to matukio
Screenshot_20230627_204326.png
Screenshot_20230628_095953.png
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages