Ben Komba/Pwani-Tanzania/11-01-2022
Wananchi mkoa wa Pwani wametakiwa kuwa makini katika makubaliano yoyote yanayohusiana na uuzaji na ununuaji wa ardhi kuepuka kukutana na usumbufu usio na lazima.
Mtaalamu wa masuala ya upimaji ardhi kutoka Kampuni ya DAGLAND, BW.DEOGRATIAS NSAMBOB NSAMBO iliyopo mjini Kibaha alipozungumza na Mwandishi wa habari hizi kutokana na kuongezeka migogoro miongoni mwa jamii kunakosababishwa na ardhi.
BW. NSAMBO amesema migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na wananchi kukosa elimu juu sharia ya umiliki, ununuaji na uuzaji wa ardhi kwa kufuata misingi na taratibu zilizopo katika kujaribu kupunguza migogoro iliyopo.
Amebainisha moja ya mambo muhimu ya kuzingatia ni kuhakikisha kunakuwepo na alama za mipaka za kudumu ambazo ni ngumu kuhamishika kwa bahati mbaya na hata kwa makusudi.
EDN