Ben Komba/Pwani-Tanzania/11-02-2022
Kampuni ya Mailimoja Auction Mart leo wameendesha mnada wa fremu za biashara katika soko la Loliondo lililopo katika halmashauri ya mji wa Kibaha, kutokana na kuwepo kwa malimbikizo ya kodi yanayokadiriwa kufika milioni 256.
Msimamizi wa Mailimoja Auction Mart, BW. PIUS MKUMBI amesema kuwa jukumu hilo la kunadi fremu zao wamepewa na halmashauri ya miji wa Kibaha na wao wameanza zoezi hilo kwa kuwatangazia wananchi wote wenye kudaiwa pango la fremu hizo.
Mwenyekiti wa Soko la Loliondo, BW. MOHAMED MNEMBWE ameongeza kuwa uongozi wa soko kwa kushirikiana na halmashauri waliweka utaratibu wa kulipa malimbikizo ya madeni ya pango.
Mfanyabiashara BW.ATHUMAN MKANGA ameiomba halmashauri ingekazania kwa kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao, kabla ya kuchukua hatua na hasa ikizingatiwa mazingira ya biashara katika eneo hilo kuzorota.
END