PAMOJA ZIARA YA DC BAGAMOYO UTATA WAGUBIKA UVAMIZI WA MIFUGO KWENYE SKIMU YA RUVU, CHALINZE

1 view
Skip to first unread message

Bernard Komba

unread,
Nov 7, 2021, 3:44:20 AM11/7/21
to Startvhabari, matukio

Ben Komba/Pwani-Tanzania/7-11-2021

Suala la mgogoro wa wafugaji kuingiza mifugo katika Skimu ya umwagiliaji ya Ruvu limeshindwa kupata ufumbuzi hata baada ya ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika eneo hilo.

 

Kushindikana kupatikana kwa ufumbuzi huo, Ni kutokana na Diwani wa Kta ya Vigwaza ambaye pia mfugaji, BW. MUSSA GAMA kuibua agenda ya kuwa Uongozi wa Skimu hiyo hawana mahusiano mema na vijiji jirani na ndio maana mifugo inaingia kula shambani humo.

 

Hoja hiyo ilijibiwa na Mwenyekiti wa Skimu ya umwagiliaji, BW.SADALLAH CHACHA ambaye ameonekana kushangazwa na madai ya Ushirika kutokuwa na mahusiano mazuri na vijiji vinavyowazunguka ilihali wana hati za heshima walizopewa na vijiji jirani kutokana na ushirikiano wanaoonyesha.

 

Akifafanua juu ya madai ya Diwani huyo ni sababu ya mifugo ya Diwani MUSSA GAMA kuwa ni sehemu ya tatizo toka kuna siku moja mifugo yake ilikamatwa na kugoma kulipa faini husika pamoja na kuidhamini na kuahidi kulipa adhabu hiyo.

 

Baada ya madai hayo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, BI. ZAINAB ABDALLAH alijikuta katumbukia katika mtego huo na kuanza kujadili mahusiano ya Vijiji vinavyozunguka Skimu na kuchukua nafasi hiyo kumbana Mwenyekiti wa Ushirika huo kwa kumtaka amuheshimu Diwani kwani yeye ndio Mkuu kabisa katika Kata.

 

Mpaka anaondoka katika Skimu Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, BI. ZAINAB ABDALLAH alikuwa hajazungumzia chochote chenye kuleta matumaini kuhusu uzuiaji wa wimbi la mifugo kuingia kwenye skimu hiyo.

 

END

 





Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages