Bernard Komba
unread,Nov 23, 2009, 7:20:30 AM11/23/09Sign in to reply to author
Sign in to forward
You do not have permission to delete messages in this group
Either email addresses are anonymous for this group or you need the view member email addresses permission to view the original message
to W I, gazeti la kenya, VOICE NEWS, reginad mengi, a b, first last, MATUKIO GOOGLE, OMMY MNGINDO, look tazama, daima freemedia, katoliki kanisa, tumaini tuma, KITU CHEUPE UKWELI, mengi r, RAIA RAIA, SANAWA CHANGAMOTO
Ben Komba/Pwani/11/23/2009 2:59 PM
Watu wenye ulemavu Mkoani Pwani wametakiwa kujiepusha na ugonjwa wa UKIMWI unaoendelea kupunguza nguvu kazi ya Taifa.
Mtaalam wa afya kutoka hospitali ya wilaya ya Kibaha, BW.ALEX UKIWAONA DITOPILE MZUZURI, amesema hayo alipokuwa anatoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI, kwa vijana kutoka kata ya Tumbi, katika kuhakikisha elimu hiyo inafika hadi ngazi ya mtaa.
BW.DITOPILE amewaeleza vijana walemavu na wasio walemavu waliohudhuria elimu hiyo juu ya UKIMWI ambayo imefanywa kupitia kikundi TUMAINI cha Mjini Kibaha, ambapo amesema kundi linaloathirika zaidi kwa sasa ni kuanzia miaka 18 mpaka 35.
Na mbaya zaidi tatizo la UKIMWI linapojitokeza katika jamii, kitu cha kwanza watu kufikiri ni kurogwa jambo ambalo linasababisha mgonjwa kufikishwa hospitali akiwa tayari amechoka sana, na kutoa nafasi ndogo ya kupona hata akipatiwa huduma.
Katibu wa kikundi cha TUMAINI,BI.REGINA MBAJI amesema wametoa mafunzo hayo kufuatia uamuzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, kuwakusanya wananchi katika makundi ya watu 15 ili waweze kuwezeshwa na kuweza kutoa elimu ya UKIMWI ngazi ya kata.
BI. MBAJI maeongeza tofauti ya kikundi chao na vingine wao ni mkusanyiko wa walemavu wenye matatizo mbalimbali, na hasa ikizingatiwa UKIMWI hauchagui iwapo mtu mlemavu au mzima na kwa dhana hiyo wameona umuhimu wa kufikisha elimu kwa kundi hilo katika jamii.
END