Wewe walionaje hili? Kujiajiri ni kugumu au ni kurahisi? Kwa nini wasema hivyo?
Mimi binafsi naona kujiajiri baada ya kumaliza chuo ni kurahisi na pia ni kugumu, yategemea na mazingira aliyonayo mtu.
Kujiajiri ni kugumu.
Kikubwa ni mtaji wa namna ya kuanza kutekeleza mradi ambao mtu amekusudia kuuanzisha. Kuna uwezekano wa kukopa Benki. Lakini ni wote walio maliza vyuo wanauwezo wa kuyakamilisha masharti? Nadhani swala la kujiajiri, ugumu wa kwanza huja kwenye namna ya kupata mtaji wa kuanzia. Vijana wengi wanaomaliza vyuo hutegemewa kuanza kuziinua familia zao kimahitaji n.k Hali hii kiukweli husabisha vijana kutafuta ajira kwa haraka kuliko kufikiri kujiajiri kwani kujiajiri kunakuwa tena ni kibarua kingine tena ambacho nacho kinahitaji mtaji mkubwa ambao uwekezaji wake utaweza kusaidia familia na jamii baada ya kipindi fulani kifupi. Ni jamii ya watu wachache sana hususani Tanzania, wenye nia na utayari kwa hiari yao kuwasaidi wale wanaotaka kujiajiri.
Kwa upande mwingine, kujiajiri kunaweza kuwa kurahisi pia. Wapo vijana wanaotoka katika familia zenye uwezo. Kikubwa hapo kwa kijana ni kuwasilisha wazo lake la kutaka kujiajiri na mchakato wa utekelezaji utaanza mara moja. Wapo walioweza kuzitumia fursa hizi ipasavyo na pia wapo walioshindwa. Washindwao kuzitumia fursa hizi kwa namna moja ama nyingine, ni lazima watakuwa na matatizo yao binafsi kuanzia ya malezi mpaka ya kuathiriwa kimtizamo na wenzao ya kuwa kujiajiri ni kugumu ilihali wameshindwa kuitumia fursa waliojaaliwa.
Nashauri kwamba, kuajiriwa kwa kijana aliyemaliza chuo kuwe ni msingi wa yeye kujiajiri na kisha yeye pia kuchukua jukumu la kuajiri wengine wanaotaka kuajiriwa, na tena waliojiriwa na wao watengeneze ajira nyingi. Kwa hiyo utaratibu uende hivyo. Kikubwa hapa ni kuwa, tusibweteke kwa kuajiriwa kwa kuona ndio mwisho. Tulioajiriwa tutumie kipato chetu kujiendeleza kimaendeleo na miongoni mwa maendeleo, mojawapo likiwa ni la kujiajiri na kisha kutegeneza ajira kwa wengine.
Nawasilisha.
Kujiajiri umekuwa wimbo, wa kila siku na wa kila anayetaka kura, na katika majukwaa hiyo ndio sentesi rahisi ya kufupisha mjadala.
Nasikitika kuwa japo kwa kiasi fulani mazingira hayajaandaliwa kuwawezesha wenye lengo la kujiajiri kufikia lengo, lakini ipo haja ya vijana kuwa wabunifu, kuunganisha nguvu zao na kuibua miradi yao tunachoshindwa ni kuthubutu.
Naalika wale walio tayari kuunganisha nguvu tuwasiliane ili 2weze kuibua miradi ye2.
AMINA!
Kaka, umetaja elimu ya ujasiriamali na mtaji kama miongoni mwa nguzo muhimu.
Kuhusu mtaji, huoni pengine kijana atakuwa na haja ya kuajiriwa wakati mwingine ili aweze kupata mtaji. Nataja kuajiriwa kama miongoni mwa namna za kupata mtaji. Sijui walisemeaje hili.
Lakini tena ile dhana ya mtaji kuwa fedha ndio unaovuruga dhana nzima ya kujiajiri. Je mtaji nh lazima uwe pesa? Je umeshapita bank ili kujua kuwa unakopesheka kwa mirad unayoibuni.
Buni, uwe nao katika writings.
Amina