Kiswahili ni lugha kuu ya
mawasiliano kwa
watanzania na ndio
maana inatambulika pia
kama lugha ya Taifa.
Kiingereza ni lugha rasmi
ambayo hutumika
maofisini na mashuleni,
hususani shule za upili
hadi vyuo vikuu.
Hutumika kama lugha
ya kufundishia na
mawasiliano mengine.
Kinyume na matarajio,
sehemu ambazo
kiingereza kilipaswa
kutumika, maofisini na
shuleni, hakitumiki
ipasavyo, bali kiswahili
ndicho kinachoshika
hatamu.
Mbali na kutoitumia
lugha ya kiingereza
mashuleni na kwenye
ofisi, nje ya maeneo
haya hali ni hiyo hiyo,
watu wanatumika
kiswahili kwa uhuru
wao kwani ndiyo lugha
pekee ituunganishayo
watanzania bila kujali
sana elimu aliyonayo
mtu. Wapo watanzania
wachache wasiokijua
kiswahili vizuri kwa
sababu wamekuwa
wakitumia lugha za
makabila yao kiasi cha
kukisahau kiswahili
lakini asilimia kubwa
tunakizungumza vizuri.
Mashuleni, walimu
wanawahimiza
wanafunzi wao
kutumia kiingereza hata
wawapo majumbani
kwao kama namna ya
kuijua zaidi lugha hii.
Kwa mantiki hii,
kiswahili kinapewa
msisitizo mdogo kwa
maana kwamba hatuna
haja ya kuendelea
kukijifunza. Au niseme
kuwa kiswahili
kinapuuzwa.
Kwa bahati mbaya
sana, pamoja na
msisitizo wa matumizi
ya kiingereza
majumbani na mitaani,
watu bado tumekuwa
hatuitumii lugha hii ya
kigeni; imebaki
kutumiwa mashuleni na
maofisini na watu
wachache. Wapo pia
baadhi ya walimu
(yawezekana ni idadi
kubwa) wafundishao
kwa kiswahili masomo
yaliyotakiwa
kufundishwa kwa
kiingereza.
Vuguvugu hili la namna
tutumiavyo lugha hizi
mbili ni janga kubwa
kwetu watanzania.
Kwa uvuguvugu huu,
kiswahili na kiingereza
zitazidi kuwa tatizo
kwetu. Kiingereza
kitazidi kuwa ni janga
letu watanzania, na
kiswahili vile vile.
Matumizi ya kiswahili na
kiingereza kwa wakati
mmoja yameshamiri
sana hususani katika
maongezi, hotuba na
hata kwenye filamu za
kitanzania. Ni za
kiswahili lakini,
kiingereza kinapachikwa
pachikwa si mchezo.
Sina hakika kama ni
kusudio la watunzi, na
kama ndivyo kwa
maudhui yapi?
Ni juzi hapa Raisi wakati
akitangaza baraza la
mawaziri, alikuwa
akiingiza maneno ya
kiingereza. Japokuwa
haikuwa kwa wingi,
lakini alichanganya
kiswahili na kiingereza.
Si kiashirio kizuri,
hususani kwa Raisi wa
nchi pale anapoongea na
wananchi ambao
inajulikana wazi kuwa
wapo wasiojua
kiingereza. Wapo
watanzania wengi
wasiokijua kiingereza,
waliokuwa wanafuatilia
Raisi akitangaza baraza
la mawaziri. Ni wazi
kuwa kuna sehemu
waliachwa, hasahasa
wale ambao hawakuwa
na mtu wa kuwapa
maana ya maneno yale
ya kiingereza kwa
kiswahili.
Si yeye tu, kwenye
vikao vya bunge,
kiswahili na kiingereza
vimekuwa vikisikika
mara kwa mara
vikitumiwa kwa wakati
mmoja. Watanzania wa
kawaida mitaani na
majumbani, mseto huu
wa lugha ni jambo la
kawaida sana.
Sina hakika kama
mchina wakati anaeleza
jambo kwa wananchi
wake kwa lugha yao, au
mjerumani, au mkorea,
na ikafika sehemu
akaingiza kiingereza.
Kama ndivyo, lugha zao
wamezipa msisitizo
stahiki mbali na kuwa
nao pasi na shaka
wanajifunza pia
kiingereza. Wanazitumia
lugha zao katika nyanja
zote. Mtanzania aendae
China kusoma, hana
budi kukijua kichina
kwanza, Ujerumani vile
vile. Huku kwetu bongo,
mwingereza anaishi
hapa miaka mitano,
hajajua kuongea
kiswahili. Watanzania
hatuna msisitizo kwa
wageni kuijifunza lugha
yetu.
Nimezisikiliza hotuba
kadhaa za hayati
Mwalimu Nyerere.
Sijamsikia akichanganya
lugha, yani Kiswahili na
Kiingereza. Alizitambua
na alikuwa na hisia
sahihi na watu wake.
Alikienzi kiswahili
ipasavyo. Alitaka
watanzania wapate
ujumbe husika bila
kukwazika na
kubabaika.
Binafsi naona kuna haja
ya kuondokana na
vuguvugu hili la lugha.
Tunazikosa zote,
hakuna upande ambao
tunaweza kuusimamia
kikamilifu na kujidai nao.
Wimbi la kuchanganya
kiingereza na kiswahili
linazidi. Litatugharimu
hapo mbeleni
Harakati za katiba
mpya ziambatane na
mabadiliko
yahamasishayo
matumizi ya lugha moja
ya watanzania wote.
Hapa namaanisha kuwa
kiswahili kipewe
msisitizo na nafasi ya
kutosha kujidai. Itumike
mashuleni; shule za
msingi hadi vyuoni.
Kiingereza kibaki kama
lugha muhimu ambayo
kila mmoja kwa wakati
wake ataona kuna
umuhimu wa
kuifahamu.
Ni uamuzi mgumu
kulingana na hali ya
Taifa letu la utegemezi
katika nyanja
mbalimbali za kiuchumi,
kielimu, kiutawala n.k.
Watu wanaweza
kufikiri kuwa muda wa
mageuzi haya ya
kihistoria ni bado, labda
baada ya Tanzania
kuwa imara kiuchumi
kiasi cha
kutokutegemea sana
misaada. K ipindi
ambacho tutakuwa
tunawategemea
wanasayansi wetu,
kipindi ambacho
tutakuwa miongoni
mwa vyanzo vya
teknologia mpya. Yote
haya binafsi naona
mwanzo wake ni
mageuzi ya kihistoria ya
kuthubutu kutumia
Kiswahili katika nyanja
zote za kimaendeleo;
kuanzia elimu na
shughuli zote rasmi na
zisizo rasmi.
Makala hii waweza pia kuisoma hapa barazani kwangu, "Mwangaza" www.nderumo.blogspot.com.