Mwisho, tuhamasishane katika ushiriki wa hali na mali, kuleta mada na hata uchangiaji wa mada husika.
Muugwana ni vitendo! Muungwana amelonga na ameliona jukwaa kutokuwa
active kwa mijadala na kuegemea upandea mwingine ulioonyesha kupoteza
muulekeo. Hili limekemewa wakati unaofaa kwa kuwa kuna changamoto
nyingi na mambo mengi ya msingi ya kujuzana. Na mambo binafsi yenye
harufu ya kadi za salamu kuyaonea kinyaa.
Inabidi wale wenye hoja zenye mashiko kama alivyosema msemaji hapo juu
waje kimashiko zaidi na mbolea ya kukuzia hoja hapa jukwaani maana
tayari ujumbe umeshafika na unahitaji kufanyiwa kazi ili kuondoka
kwenye uegemezi wa mambo binafsi kama wingi za salaam na kuanza
kujadili mambo yenye mashiko.
Kukiri kuwa kuna wenye hoja zisizo na mashiko ni hatua kubwa ya
ukomavu wa kupima hoja ya kila mtu hii inaonyesha jukwaa lina vichujo
vya kutosha kung'amua hoja nyepesi na nzito; Mfano anayetoa salamu na
anaye shauri kupunguza mfumo wa salamu na kujadili mambo ya msingi.
Hapa hapahitaji kuwa na shahada ya uzamivu kung'amua mwenye mashiko na
mwenye ukame wa fikra.
Kisima ametupa courage na kuturudisha kwenye mstari ameona kama
aliyemtangulia alivyoona! Nami nikupongeze HONGERA KISIMA KWA KUONA!
umetupa courage. kuna kakitabu niliwahi kukasoma kana msemo "No matter
how far the wrong way you have gone! Turn back! hata hapa jukwaani
"Hata kama tumeingia chaka kwa kiwango cha kukatisha tamaa! tutafute
uchochoro wa kutokea tusizidi kupotea" Hii ni courage laini lenye
ladha ya vitendo zaidi kuliko maneno yaliyozoeleka. na Courage is not
the absence of fear, but rather the judgement that something else is
more important than fear.
"Heri wale wenye hoja zenye mashiko maana wasio nazo wanachakujifunza
kutoka kwao"
Naomba kuwasilisha.
--
John M. Mkumbwa.