John, kila mwaka wa uchaguzi tutakuwa tunailalamikia tume ya uchaguzi, na itaendelea kuwa mhimili wa CCM wa kuchakachua matokeo kama tume hiyo nayo haitarekebishwa kikatiba. Wapinzani wataendelea kuambiwa wajipange tena kwa uchaguzi unaofuata, na utaratibu utazidi kuwa huo huo.
Kama usemavyo ndugu John, chama tawala kilishasema kitasaka ushindi kwa hali na mali. Kutokutoa kipaumbele katika kurekebisha katiba, hususani kwa vifungu vya uchaguzi na tume yenyewe ya uchaguzi, yaweza kuwa ni miongoni mwa matayarisho yao makubwa kwa chaguzi zijazo na upinzani utazidi kuambiwa "ujipange kwa uchaguzi ujao". Tuangalie makali ya Bunge letu, yawezekana nyingi za ndivyo sivyo zikasimamiwa ipasavyo na kuuanza ukurasa mpya wa demokrasia kwa vitendo na si zama hizi za demokrasia kwa maneno.