Yeye alidokeza kuwa, si sahihi kusema Tanzania Bara au Tanzania Visiwani kwani jina Tanzania tayari limeshajumuisha majina, Bara na Visiwani. Ulikuwa ni mtizamo wake na aliweka kigezo cha kukosolewa inapobidi, hivyo alihitaji uhalali wa alichokuwa anakiamini.
Binafsi naona ni sahihi kusema Tanzania Bara ama Tanzania Visiwani, kwani kwa kutamka hivi, ni ufafanuzi tu. Yaani, kwa kusema hivi, sioni kama inaleta maana tofauti pindi mtu asemapo Tanzania upande wa Bara au Tanzania upande wa Visiwani.
Wanakikundi, mwasemaje?
Hivyo kwa maneno mengine unaweza kusema ile dhana ya mtazamo wa Tz
visiwani haipo tena kimebaki kiini macho. Nasema hivyo maana katiba ya
sasa ya Muunganao haimtambui makamu wa kwanza na wa pili wa raisi wa
ZNZ lakini pia wakati huo huo katiba mpya ya ZNZ haimtambui waziri
mkuu wa Tanzania kwa maana ya Jamhuti ya muungano wa TZ.
Tz visiwani ilishakufa kilicho baki ni dhana na hisia kuwa iko hai. Na
ukiangalia kwa undani utaona jinsi Tanganyika inavyorudi taratibu
taratibu maana kinachounganisha Uznzbari na Utanganyika ni katiba
ambayo kwa sasa katiba zote mbili zina sigana ndio maana hata vuguvgu
la kudai katiba mpya linachagizwa kila kona.
Ili tuwe na Tanzania visiwani na Tanzania Bara yenye taswira ya kweli
kwenye kioo kisicho na nyufa muungano unahitaji kufanyiwa marekebisho
makubwa sana! Yaani kuweka mezani na kuongea upya juu ya mustakabali
wa Jamhuri ya muungano wa TZ vinginevyo ingetokea CUF ikachukua dola
ZNZ na CDM ikachukua Dola huku Bara naamini tungekuwa tunaongea
mengine maana tayari nchi mbili hizi zingekuwa vipande vipande maana
katiba zote mbili hazielezi nafasi ya vyama pinzani vinaposhika dola
ZNZ na TZ Bara kuwa muungano unakuwa na sura gani. Pata mfano wa CUF
na CDM bungeni kuhusu uongozi wa kambi ya upinzani.
kwa sasa imebaki dhana, hisia, na maneno matupu ambayo unaweza kusema
hayavunji mfupa. HATUNA TENA TZ VISIWANI WALA TZ BARA maneno hayo
yamesha koma kwenye katiba mpya ya ZNZ isipokuwa yapo kwenye vinywa
vya watawala na baadhi ya wananchi wanao amini kuwa ZNZ si nchi kamili
yenye mamlaka yake kamili.
Naomba kuwasilisha.
Mtoi
Neno la leo
"Heri mpumbavu anayeficha uchi kuliko mwerevu anayetembea tupu wazi"