Lakini kwa bahati nzuri sana, zipo shule ambazo zina umeme na komputa za kutosha kabisa. Langasani Sekondari iliyopo T.C.P na Ng'uni Sekondari ni miongoni mwa mifano hai.
Mbali na kuwepo kwa komputa za shule, pia wapo vijana waalimu, wengi wao wakitokea vyuoni, ambao kwa sasa wanamiliki komputa zao wenyewe na ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kurahisisha au niseme kuleta unafuu katika katika ufundishaji.
Je, kwa waalimu ambao wapo karibu na komputa wanazitumia komputa hizo kutayarisha SCHEME OF WORK au bado wanapoteza muda na kwa uchovu kuchora chora mistari na kutumia karatasi za kaboni ili kupata nakala? Bado wanatumia "yellow notes" kwa sababu ya uvivu wa kuandaa kwa kuwa kuandika kwa kalamu kunachosha na kusikokuwa na ari yoyote badala ya kuandaa notes kwa komputa na kuzihifadhi vyema na hata kuweza kuzibadili kwa haraka pale inapobidi?
Ni dhahiri kuwa ukishaandika "scheme of work" moja na kuihifadhi kwenye komputa yako au kwenye flash, basi mwaka unaofuata kazi itakuwa rahisi kwani ni kurekebisha (editing the scheme of work) tu. Hakika ni muda mwingi unaokolewa pamoja na kuwa kuna gharama kidogo za ku-print.
Nafahamu fika, ku-print notes yaweza kuwa gharama ila sio lazima iwe hivyo pia, hata ku-print Scheme of work pia jamani?
Si jambo la kuhitaji utafiti, bali ni jambo la wazi kabisa kuwa walimu wengi sasa wanamiliki simu zenye uwezo mzuri wa intaneti. Sina hofu kuwa ni wachache sana waitumiayo teknolojia hii kujiimarisha kwa kile watarajiacho kufundisha, kujipatia habari mbalimbali za majarida ya kisayansi, historia mbali mbali, kuondoa utata kuhusu jambo la kimasomo lililosumbua akili za walimu hata wanafunzi, kuandaa notes na mambo mengine mengi yahusuyo taaluma. Wengi wanafanya simu kuwa ni za maonesho achana na matumizi ya kawaida ya mawasiliano.
Binafsi naona kuna haja ya kubadilika na kuachana na mazoea. Walimu, tujitengenezee mazingira ya kutuwezesha kufanya kazi yetu kwa "ari" na kwa nguvu.
Kabla ya kuipata "projector" itakayotusaidia kufundisha kwa kompyuta moja kwa moja, basi hebu na tutumie teknologia hizi katika namna ambazo zitarahisisha na kufanya tuifurahie kazi yetu hii adhimu ya kufundisha.
Nawasilisha.
Hongera sana Kisima kwa kuibua hoja yenye maslahi kwa mstakabali wa taifa hili.
Naomba kuwambia kuwa alilolisema Kisima ni kweli, kwani mfano mzuri ni Kihonda sekondari ambako kuna komputa desk top 20 na laptops 4. Lakini bado ni mwalimu mmoja au wawili tu wanaotumia komputa hizo kuandaa masomo.
Inasikitisha kumkuta mwalimu kakaa mbele ya komputa kiandika notice katika daftar lale kwa mkono, kihonda hakuna gharama binafsi za kuprint kwani printer zipo pia kinakikilishi kipo. Wengi hucheza game tu.
Ipo haja ya kupeana changamoto kama hizi na kukumbushana kuwa sisi si walimu wa karne ya kumi bali ya 21 tuende na wakati. Asanteni
Amina
Yawezekana watu wanasubiria kufundishia komputa na wanasahau kuwa wanaweza kuitumia kwa mambo mengine, baadhi ni hayo niliyotangulia kuyaeleza.
Walimu tuitike katika wito huu tunaitiwa, wa mabadiliko yaambatanayo na sayansi na teknologia.