Yapo maswali manne makuu ya kujiuliza, kama ifuatavyo;
Je tupo tayari kubadilika toka kiingereza hadi kiswahili?
Je tunapata faida kiasi gani katika kutumia kiingereza kuanzia shule za upili?
Je lugha inamchango kiasi gani katika maendeleo yetu?
Je tupo huru kweli?
Kwanza kabisa kumekuwa na kutokuwa na utayari katika kubadili mitazamo, japo kwa namna ifaayo hili nalo linatokana kuwa watawaliwa kwa muda mrefu na hadi sasa. Ni vigumu kufikiri, kutafakari na kueleza au kufikisha ujumbe takiwa kwa lugha usiyoifahamu.
Ipo haja ya kuwawezesha watoto kufikiri vizuri, na kwa hiyo kuwafundisha lugha itakayotumika kufikiri ili tuwe na maendeleo ya kweli.
Kwa hali ilivyo, hapana shaka kuwa tatizo, na tunachelea kulitatua kwa woga tu.
Twaweza tukiamua