Group: http://groups.google.com/group/luxmund/topics
- Je, ni sahihi kusema Tanzania Bara au Tanzania Visiwani? [2 Updates]
- Ndugu wanajamvi. [1 Update]
albert kisima <alber...@yahoo.com> Dec 16 10:54PM -0800 ^
Hii ni mada ambayo nilikutana nayo katika ukurasa wa facebook wa rafiki yangu mmoja.
Yeye alidokeza kuwa, si sahihi kusema Tanzania Bara au Tanzania Visiwani kwani jina Tanzania tayari limeshajumuisha majina, Bara na Visiwani. Ulikuwa ni mtizamo wake na aliweka kigezo cha kukosolewa inapobidi, hivyo alihitaji uhalali wa alichokuwa anakiamini.
Binafsi naona ni sahihi kusema Tanzania Bara ama Tanzania Visiwani, kwani kwa kutamka hivi, ni ufafanuzi tu. Yaani, kwa kusema hivi, sioni kama inaleta maana tofauti pindi mtu asemapo Tanzania upande wa Bara au Tanzania upande wa Visiwani.
Wanakikundi, mwasemaje?
Mohamedi Shabani Mtoi <moudd...@gmail.com> Dec 17 01:49AM -0800 ^
Kisima.
Unaposema Tanzania Bara moja kwa moja unagusa huku kwetu yaani
Tanganyika kwa maneno megine. Na unaposema Tanzania Visiwani inagusa
Zanzibar, Kimtazamo iko hivyo na kabal ya mabiliko ya Katiba ya Zenj
ilikuwa hivyo lakini kwa sasa katiba ya Zenj inaitambua ZNZ kama nchi
kamili iliyo na mipaka yake na mamlaka yake kamili.
Hivyo kwa maneno mengine unaweza kusema ile dhana ya mtazamo wa Tz
visiwani haipo tena kimebaki kiini macho. Nasema hivyo maana katiba ya
sasa ya Muunganao haimtambui makamu wa kwanza na wa pili wa raisi wa
ZNZ lakini pia wakati huo huo katiba mpya ya ZNZ haimtambui waziri
mkuu wa Tanzania kwa maana ya Jamhuti ya muungano wa TZ.
Tz visiwani ilishakufa kilicho baki ni dhana na hisia kuwa iko hai. Na
ukiangalia kwa undani utaona jinsi Tanganyika inavyorudi taratibu
taratibu maana kinachounganisha Uznzbari na Utanganyika ni katiba
ambayo kwa sasa katiba zote mbili zina sigana ndio maana hata vuguvgu
la kudai katiba mpya linachagizwa kila kona.
Ili tuwe na Tanzania visiwani na Tanzania Bara yenye taswira ya kweli
kwenye kioo kisicho na nyufa muungano unahitaji kufanyiwa marekebisho
makubwa sana! Yaani kuweka mezani na kuongea upya juu ya mustakabali
wa Jamhuri ya muungano wa TZ vinginevyo ingetokea CUF ikachukua dola
ZNZ na CDM ikachukua Dola huku Bara naamini tungekuwa tunaongea
mengine maana tayari nchi mbili hizi zingekuwa vipande vipande maana
katiba zote mbili hazielezi nafasi ya vyama pinzani vinaposhika dola
ZNZ na TZ Bara kuwa muungano unakuwa na sura gani. Pata mfano wa CUF
na CDM bungeni kuhusu uongozi wa kambi ya upinzani.
kwa sasa imebaki dhana, hisia, na maneno matupu ambayo unaweza kusema
hayavunji mfupa. HATUNA TENA TZ VISIWANI WALA TZ BARA maneno hayo
yamesha koma kwenye katiba mpya ya ZNZ isipokuwa yapo kwenye vinywa
vya watawala na baadhi ya wananchi wanao amini kuwa ZNZ si nchi kamili
yenye mamlaka yake kamili.
Naomba kuwasilisha.
Mtoi
Neno la leo
"Heri mpumbavu anayeficha uchi kuliko mwerevu anayetembea tupu wazi"
Topic: Ndugu wanajamvi.Mohamedi Shabani Mtoi <moudd...@gmail.com> Dec 16 11:40AM -0800 ^
Wanajamvi.
Muugwana ni vitendo! Muungwana amelonga na ameliona jukwaa kutokuwa
active kwa mijadala na kuegemea upandea mwingine ulioonyesha kupoteza
muulekeo. Hili limekemewa wakati unaofaa kwa kuwa kuna changamoto
nyingi na mambo mengi ya msingi ya kujuzana. Na mambo binafsi yenye
harufu ya kadi za salamu kuyaonea kinyaa.
Inabidi wale wenye hoja zenye mashiko kama alivyosema msemaji hapo juu
waje kimashiko zaidi na mbolea ya kukuzia hoja hapa jukwaani maana
tayari ujumbe umeshafika na unahitaji kufanyiwa kazi ili kuondoka
kwenye uegemezi wa mambo binafsi kama wingi za salaam na kuanza
kujadili mambo yenye mashiko.
Kukiri kuwa kuna wenye hoja zisizo na mashiko ni hatua kubwa ya
ukomavu wa kupima hoja ya kila mtu hii inaonyesha jukwaa lina vichujo
vya kutosha kung'amua hoja nyepesi na nzito; Mfano anayetoa salamu na
anaye shauri kupunguza mfumo wa salamu na kujadili mambo ya msingi.
Hapa hapahitaji kuwa na shahada ya uzamivu kung'amua mwenye mashiko na
mwenye ukame wa fikra.
Kisima ametupa courage na kuturudisha kwenye mstari ameona kama
aliyemtangulia alivyoona! Nami nikupongeze HONGERA KISIMA KWA KUONA!
umetupa courage. kuna kakitabu niliwahi kukasoma kana msemo "No matter
how far the wrong way you have gone! Turn back! hata hapa jukwaani
"Hata kama tumeingia chaka kwa kiwango cha kukatisha tamaa! tutafute
uchochoro wa kutokea tusizidi kupotea" Hii ni courage laini lenye
ladha ya vitendo zaidi kuliko maneno yaliyozoeleka. na Courage is not
the absence of fear, but rather the judgement that something else is
more important than fear.
"Heri wale wenye hoja zenye mashiko maana wasio nazo wanachakujifunza
kutoka kwao"
Naomba kuwasilisha.