Lucky
unread,Dec 13, 2010, 1:13:13 AM12/13/10Sign in to reply to author
Sign in to forward
You do not have permission to delete messages in this group
Either email addresses are anonymous for this group or you need the view member email addresses permission to view the original message
to Lux.mund
Baraza linakosa msisimko kabisa. Sijaelewa tatizo ni nini.
Tuna kila haja ya kuliendeleza jamvi hili. Njia pekee ni ya kuleta
mada zitakazogusa hisia za watu. Moja kwa mtu aone kuwa atakuwa na
deni asipotoa mchango wake.
Kila mmoja wetu atambue kuwa anao wajibu wa kulikuza jamvi hili. Kila
kukicha hatuna budi kuumiza kichwa katika harakati za kutafuta cha
kushirikishana. Hii iwe ni tabia yetu wanajamvi, tuone kuwa tuna
wajibika na jamvi hili. Hebu tulifanye liwe chanzo cha maarifa.
Nimeamua kuandika hivi kwani, nimekuwa nikipita hapa mara kwa mara
kuangalia kama kuna mada, pongezi, shukrani, matangazo (hapa tungeweza
kuweka taarifa za mahafali ya wahitimu wa Mwenge 2007-2010 mathalani)
na kadhalika na kadhalika.
Pia, kwa wale waliopo Mwenge University, wajaribu kuwahamasisha watu
wajiunge na jamvi hili. Wahadhiri na wanafunzi, wote wanahusika. Uwepo
wa wahadhiri utatupa changamoto zaidi. Cha muhimu tu ni kuwa, tusiache
jamvi likaa bila ya chochote cha kuwafanya watu walione jamvi hili
kuwa halina maana wala msaada.