Hivi ni sahihi kweli NEC kutangaza tu idadi ya kura zilizoharibika bila kueleza zimeharibikaje? Ni idadi kubwa sana ya kura zilizoharibika. Binafsi nadhani si sahihi. Wangetoa pia namna ya kura zilivyoharibika. Kama ni watu waliwachagua kikwete na Slaa kwa wakati mmoja, watueleze na ilikuwa mara ngapi, na namna nyingine zote zilizopelekea kuharibika kwa kura. Nadhani hili lingewezekana.
Sijui wadau ninyi mwasemaje.