Cha kuongeza tu ni kuwa tujaribu kuangalia wakenya walifanikiwa vipi
kuibadilisha katiba yao. Sikuufuatilia sana mchakato huu lakini kwa
ufupi, wakenya walitoa maoni yao na kisha kupiga kura katika
kuipitisha katiba mpya. Bila shaka tunalo la kujifunza hapa. Wakenya
waliwezaje kuchangia kwa kutoa maoni yao? Hii inadhihirisha kuwa
walikuwa wakiifahamu vyema, ama kwa wenyewe kuipitia na kubaini sehemu
zenye upungufu au baada ya ufafanuzi wa sehemu zinazotakiwa
marekebisho kwa kuwatumia wataalamu na kisha wakatoa maoni yao.