UCHUMI WA LUDEWA

11 views
Skip to first unread message

Erhard Willa

unread,
Nov 4, 2011, 4:40:50 PM11/4/11
to lud...@yahoogroups.com, lud...@googlegroups.com
Ndugu zangu wapendwa katika maendeleo ya Ludewa. Nawasalimu Khamwene!
Naukubali ujio wa wageni Ludewa kwani licha ya changamoto tutakazo kuwa nazo tutafaidi mengi kutoka kwao:
1. Tabia ya ubinafsi yaani mtu hawezi kununua bidhaa isipokuwa kwenye duka la mdugu yake.
2.Uchawi utapungua kwani tulikuwa tunaogopa hata kujega majengo mazuri tukihofia kulogwa.
3.Biashara zitaongezeka kwani wanunuzi watakuwepo.
4. Ushindani wa maendeleo kwani wageni huleta ushindani mkubwa.
5.Upevu wa kidemokrasia watu tutaacha kudanganywa na kuonewa na watu wachache kwa maslahi binafsi.
6. Kupunguza ulevi utafiti usio rasmi unaonesha 90% ya wanaludewa ni walevi kuanzia mtoto hadi wazee.
7.Uvivu nao upo mtu anashinda tokea asubuhi kujadili watu walioendelea, ukimuuliza anasema sili kwa mtu.
8. Ubinafsi mtu akipata nafasi yoyoyte hawavuti watu wa Ludewa kuingia huko kutaka ila kuonekana yeye ni yeye.
9.Na kadhalika.
             MAONI
1. Kama tunavyojadili naona kila mtu moyoni mwake ajihoji amewahi kuwasaidia wana Ludewa wangapi
    kwa nafasi aliyonayo.Kama hakuna afanye hivyo.
2.Tujenge utamaduni wa kurudi nyumbani japo mara moja kwa mwaka na kujadili nani yuko wapi na anafanya nini na
     amechangia nini maendeleo ya ludewa.
3.Tuwaombe wanodaiwa kuwa ni wachawi wasituloge wanaLudewa ila Wageni watakaoleta usumbufu kwa wenyeji.
4.Tuwe na mfuko tuchangie elimu hasa kuwalipa walimu kwenye shule zenye upungufu
5.Wenye mitaji wawekeze Ludewa ili vijana wapate ajira.
6.Wasomi kuanzia kidato cha nne ndio waruhusiwe kugombea nafasi uongozi wa vijiji pia katika nafasi za udiwani tupate wenye
    shahada wa kutosha wagombee ili kuzuia ubadhilifu wa fedha za halmashauri yetu na wasimamie maendeleo kwa
    uhakika.
NAOMBA KUTOA HOJA.
                        Yuni
                          Erhard


Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages