Amani iwe kwenu.
Ni muda sasa tangu kusitishwa kwa vikao vya bunge ambalo mbunge wetu,Mh. Deo Filikunjombe ni muwakilishi wetu huko.
Kumekuwa na ukimya,pengine kuna yanayofanyika jimboni kwetu,lakini mimi sijui maana sipo Ludewa na wala sijafika huko muda mrefu kidogo.Naomba "update" mheshimiwa.
Mimi najua kimya kingi kina mshindo mkuu, ila hofu yangu ni kuwa ngoja ngoja nayo yaumiza matumbo,nakukumbusha tu kuwa,mimi nahitaji kujua KUTOKA KWAKO,tupo wapi,ZILE JITIHADA zimefikia wapi.
Nataka kujua ili kwa umoja wetu WAPENDA MANDELEO wa Ludewa tushiriki,kama ni kwenye kukosoa na iwe hivyo,na kama kwenye kupongezana basi tufanye vivyo ili kutiana moyo.
Kutujuza kutatuamsha na kukufanya nawe pia kuyakumbuka kwa urahisi na kukuepusha na KUJISAHAU katika yale yaliyo ya vipaumbele kwako,sikuzuii KUVUKA LENGO.Wewe tekeleza tu,hata na yale ambayo hayakuwa katika mipango yako,kasi ikiwa kubwa si lazima kuipunguza ili tu malengo yaende sambamba na wakati.
Si kwamba nakuunga mkono kwa JITIHADA ZAKO pekee,bali nataka hata kwa maneno matupu kuwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya Ludewa ninayoyaona mbele yako.
Naomba pia nikukumbushe kuwa sitabakia kwenye kuunga mkono tu!bali nitakosoa nikiona waenda tofauti.
Naomba sasa Mheshimiwa unijuze/utujuze tumefikia wapi katika yote muhimu kwa Ludewa,na hapa sitaki kuorodhesha maana inawezekana nikayataja machache na kwako yakawa mengi.
Mimi nakuunga mkono,
Na wewe usiniangushe.
Ngalawa Bonaventura.