Nimenyamazaaa lakini mmh naona nijitose kusema ukweli manake Lol kaazi kwelikweli.
Pamoja najua kwamba watu tuko kwenye wk ya maombolezo, lakini niwape habari njema kidogo.
NIMEAMUA KUACHANA NA UKAPELA RASMI MWEZI WA 6 TAREHE 23 YA MWAKA HUU.
Nategemea kufunga pingu za maisha na Mrembo mmoja nadhani wengi wenu mtakuwa mnamfahamu; Happiness Koda. Napenda kuwashirikisha ktk maandalizi ya harusi hii.
Kwa kifupi Bwana Gq( Grayson Elisa Kavumo, Mpare aka Shemejiiii) akishirikiana na Dr Mrita Felix ndio wenyekiti, kaka Bernard Konga akiwa kama Katibu na ndugu yangu Dezema, Deo Mahawe mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, ninapenda kuwakaribisha sanasana ktk maandalizi haya. Baadhi yenu mtakuwa mmeshapata taarifa lakini ningependa kuwataarifu wadau wengine ambao hawajafahamu kupitia groupmail hii. more details tutaendelea kupashana habari.
Napenda kuwakilisha Hoja!!!
Mungu awabariki
Alpha King aka "mume mtarajiwa"