ANOTHER REMINDER: WOTE TUNAOMBWA KUJIUNGA NA MTANDAO WA E-MAIL YA PAMOJA YA LEKIDEA (lekidea2008@googlegroups.com)

7 views
Skip to first unread message

Paul Msaki

unread,
Sep 30, 2011, 6:18:50 AM9/30/11
to ujso...@live.co.uk, s&f...@cats-net.com, pascha...@yahoo.com, juvenal...@wfp.org, efym...@yahoo.com, ema...@yahoo.com, emilia...@yahoo.com, etma...@duce.ac.tz, fky...@moi.ac.tz, louis...@yahoo.com, mamt...@yahoo.co.uk, martin...@yahoo.co.uk, noelm...@yahoo.com, peter...@yahoo.co.uk, peterk...@yahoo.co.uk, savinu...@undp.org, sma...@hotmail.com, umbel...@yahoo.com, upendo...@yahoo.com, vgkc...@yahoo.com, vsrc...@yahoo.com, mata...@gmail.com, dlyakin...@yahoo.com, sia...@yahoo.com, pauls...@yahoo.com, sshe...@tcaa.go.tz, floria...@yahoo.co.uk, stchri...@cats-net.com, lekid...@googlegroups.com, pms...@vodacom.co.tz, msa...@hotmail.com, kessy...@yahoo.com, ass...@plancom.go.tz, valence....@wits.ac.za, s...@cats-net.com, ekman...@hotmail.com, gmm...@yahoo.com, stn...@yahoo.com, msa...@gmail.com, steve...@yahoo.com, sals...@yahoo.com, elv...@yahoo.com, salvator...@yahoo.com, kila...@gmail.com, kate...@yahoo.com, er...@vodacom.co.tz, jk...@vodacom.co.tz, gmaly...@yahoo.com, ro...@yahoo.com, ra...@yahoo.com, deograt...@yahoo.com, maris...@yahoo.com.uk, jsip...@msd.or.tz, trlm...@gmail.com, balthaza...@yahoo.com, vnde...@gmail.com, shew...@yahoo.com, pascha...@yahoo.com, valens...@yahoo.com, favref...@yahoo.com
LEKIDEA (Legho-Kirua Development Association)

Hii ni taasisi iliyoanzishwa rasmi toka 2008, kwa matumaini ya kufufua, kukuza na kuhamasisha maendeleo ktk eneo letu lote la KIRUA VUNJO MASHARIKI katika masuala yote ya Kiuchumi, Kijamii, Kilimo, Mazingira, Elimu, Ulinzi katika Maeneo yote yanayozunguka Kirua Vunjo Mashariki na kubwa kabisa ni suala muhimu la Barabara zote za zinazopita ktk Vijiji vya kuanzia maeneo ya Uchira, Carumel,
Mero, Kileuo, Usangi, Kotule, Mrumeni, Legho, Lasso  hadi Kanji na mitaa yake yote.

Sambamba na malengo hayo muhimu, juhudi kubwa na Kampeni mbalimbali zimeandaliwa ili kuhamasisha kila Mzaliwa toka maeneo tajwa kuhamasika ipasavyo, kujituma, na kushiriki hatua hii muhimu ya kihistoria ya kuukomboa ukanda wetu huu ili hata ikiwezekana tuwe mbele zaidi ya jamii nyingine kama Marangu, Rombo, Kibosho nk,


Sekretariet yetu katika mikakati ya kutuunganisha nguvu, tumejiunga na Mtandao Mkubwa kabisa Duniani wa Googlegroups.com; kwa Mawasiliano ya barua-pepe (emails), na majadiliano ya hoja za moja-kwa-moja (chatting) kuhusiana na mjadala au hoja muhimu za jamii na maendeleo yetu.

Mtandao huu wa Googlegroups.com ni kati ya mikakati ya Sekretariet kuhakikisha kuwa Wanajamii wote wa Maeneo tajwa waliopo Tanzania nzima na popote pale duniani wanapata ujumbe huu muhimu, wanashirikishwa na kuwa mhimili mmoja ktk kufikia mafanikio tunayoyatamani mbele yetu. Katika Mtandao huu tumeanzisha barua-pepe (email) rasmi ya taasisi yetu inayoitwa; lekid...@googlegroups.com.

Email hii itakayowezesha taarifa na mawasiliano ya haraka, yasiyokuwa yanakwamishwa na mailbox-size au vikwazo vya mitandao mingineyo ktk sera tofauti za maofisini, tatizo hili litakwisha. Ndiyo lengo la kukupa MWALIKO HUU ili ujiunge, tuwe huru, tuwe kitu kimoja, tusonge mbele.


Ili kukamilisha hatua hii ya KUJIUNGA (join), kuna email itakuja ktk email za wanajamii wote, kila mwana-LEKIDEA, yoyote yule na popote ulipo, anatakiwa ku-ACCEPT mwaliko huu utakaokuja ktk email yake, na moja-kwa-moja utaingizwa ktk mtandao wa email ya pamoja ya lekid...@googlegroups.com, na wazo au taarifa yoyote utakalochangia itawafikia wana-LEKIDEA wote papo hapo, bila gharama au kuchelewa. Usiwe sehemu ya waliochelewa bali walio mstari wa mbele.
Hadi sasa tunao waliojiunga wachache, tunataka wote tuwe ktk mtanda huu iwe rahisi kuwasiliana na ku-attach documents and hata picha za size kubwa ambazo zinakwama ktk inbox nyinginezo.

Kama utakwama Kujiunga kutokana na kikwazo chochote, tuma neno lifuatalo "NIUNGANISHE NA LEKIDEA", tuma ktk email hii; lekid...@googlegroups.com, tutakuwezesha kukamilisha kujiunga mara moja.

Tunatanguliza shukrani kwa ufahamu wako na dhamira yako ya kuukwamua ukanda wetu.

Naomba kuwasilisha;

Regards;

Paul Z. Msaki
Mwana-Sekretariet
K.n. Sekretariet - LEKIDEA.


Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages