Ofisi za mawaziri ni 'vijiwe'

1 view
Skip to first unread message

mcha...@googlemail.com

unread,
Oct 10, 2007, 2:29:29 PM10/10/07
to KULIKONI TANZANIA
Ofisi za mawaziri ni 'vijiwe'
Zaidi ya asilimia 90 ya mawaziri wanatumia ofisi zao kama `vijiwe`
lakini muda wao mwingi wanautumia kufanya shughuli zao binafsi
zikiwemo za biashara badala ya zile walizoajiriwa kuzifanya.

Maoni hayo yalitolewa juzi usiku na Profesa Mwesiga Baregu kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, alipokuwa akichangia mada katika kipindi cha
`Jenerali on Monday` kinachorushwa na kituo cha televisheni cha
Channel Ten.

Profesa Baregu alisema, hali hiyo inasababisha mawaziri wengi
kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi.

`Watu wanajua mawaziri wengi wa serikali hii ni wafanyabiashara hivyo
ofisi kwao ni kama `kijiwe` kwa ajili ya kufanikisha shughuli zao
binafsi` alisema.

Aidha, katika kipindi hicho watu mbalimbali walitoa maoni yao juu ya
utendaji wa serikali ya awamu ya nne.

Baadhi yao walisema, hakuna dalili zozote za kutekeleza ahadi ya
serikali ya awamu ya nne ya kuwaletea wananchi maisha bora.

Akichangia mada katika kipindi hicho, Bw. Abdalah kutoka Tanga
alisema, hali ya maisha kwa wananchi wa kawaida inazidi kuwa ngumu
kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi hii.

Naye mchangiaji mwingine Bw. Benny kutoka Mwanza alisema, viongozi
wengi wa serikali hivi sasa wanachukua raslimali za taifa bila huruma
na kuzifanya mali zao.

Alisema watendaji wengi wa serikali hasa ngazi za juu hawajali
wananchi wala hawafuati sheria zinazolinda maadili ya viongozi wa
umma.

Aidha katika mjadala huo baadhi ya wachangiaji walisema, tabia ya
ufisadi iliyopo hivi sasa inatokana na viongozi wengi kipindi cha
nyuma kufuata falsafa ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa
unafiki.

Walisema Mwalimu Nyerere alikuwa na falsafa ya `Ujamaa na Kujitegemea`
kwa kuwa aliamini kwamba hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuwafanya
watu wawe wamoja.

Walitoa mfano kwa marehemu Oscar Kambona ndiye kiongozi pekee
aliyeweza kumpinga Mwalimu juu ya falsafa hiyo lakini wengine
walimkubalia kwa unafiki.

Naye muongozaji wa kipindi hicho Bw. Generali Ulimwengu alisema, kama
leo Mwalimu Nyerere angefufuka akaona ufisadi unaofanyika ndani ya
serikali angekufa mara ya pili.

Alisema ni bora mawaziri wakatangaza kwamba wao ni wafanyabiashara na
ikajulikana hivyo badala ya kuendelea kutumia nafasi walizonazo ili
kufanikisha biashara zao.

Aliongeza kuwa viongozi wa sasa wanafanya ufisadi huu bila ya uoga kwa
kuwa wanajua ifikapo mwaka 2010 kwenye uchaguzi watanunua kura kwa
kilo moja ya sukari na kipande cha kanga.

SOURCE: Nipashe

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages