Karamagi azua balaa linginee

0 views
Skip to first unread message

mcha...@googlemail.com

unread,
Oct 10, 2007, 2:23:12 PM10/10/07
to KULIKONI TANZANIA
Karamagi azua balaa linginee

2007-10-10 16:51:47
Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Wakati sakata la kusainiwa kwa mktaba wa Mgodi wa Madini ya Buzwagi
likiendelea kuzizima nchini kutokana na tuhuma wanazozitoa wapinzani
kuhusu mkataba huo, Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Nazir
Karamagi anadaiwa kuzua balaa jinginee.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinadai kuwa
Waziri huyo ametoa idhini kwa kampuni moja ya madini kuendelea na
uchimbaji katika eneo lenye leseni za wachimbaji wadogo na hivyo kuzua
mapigano makubwa.

Inadaiwa kuwa vurugu hizo zimetokea huko Mahenge mkoani Morogoro
kwenye eneo la mgodi ulikanao kama Epanko.

Taarifa zaidi zinadai vurugu hizo zilikuwa kubwa kiasi cha polisi
kulazimika kumwaga kikosi chake kwenye eneo hilo ili kuweka mambo
sawa.

Inadaiwa kuwa baada ya uamuzi huo unaodaiwa kuwa wa Waziri Karamagi
kutolewa, wachimbaji wadogo na wananchi katika eneo husika walikuja
juu na kujiingiza kwenye mapigano makali baina yao na wafanyakazi wa
kampuni husika.

Hali hiyo ilizusha mapigano makali baina ya wafanyakazi wa kampuni
hiyo ambao walilazimika kumwaga risasi na kujeruhi vibaya wachimbaji
wadogo wawili.

Imeelezwa kuwa baada ya tafrani hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Meja
Jenerali Mstaafu Said Kalembo alilazimika kwenda haraka eneo hilo na
kuwakuta wachimbaji wawili waliojeruhiwa wakiwa wamelazwa hospitalini.

Wachimbaji hao wametajwa kuwa ni Lazaro Chalo na Issa Ramadhani, ambao
wamefanyiwa upasuaji wa tumbo baada ya kutunguliwa kwa risasi na
wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Taarifa hizo zinasema Waziri Karamagi anadaiwa kutoa maamuzi yaliyoipa
umiliki wa mgodi huo wa Epanko kampuni moja binafsi na hivyo kuwaacha
wachimbaji wadogo wakijiona kuwa wamekosa chao.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa mgodi huo ulikuwa kwenye mgogoro wa muda
mrefu baina ya kampuni hiyo inayofanya utafiti wa madini na wachimbaji
wadogo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro inadaiwa amekiri kuwa uamuzi wa wizara ya
Nishati na Madini wa kuwamilikisha kampuni hiyo eneo la mgodi huo
unaleta utata.

Hata Mkuu wa wilaya ya Ulanga Dk. Rajabu Rutengwe naye inasemekana
hakutoa kibali kwa kampuni.

* SOURCE: Alasiri

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages