Kingunge ashangaa kupondwa ziara ya mawaziri

0 views
Skip to first unread message

mcha...@googlemail.com

unread,
Oct 10, 2007, 2:30:55 PM10/10/07
to KULIKONI TANZANIA
Kingunge ashangaa kupondwa ziara ya mawaziri
Posted Date::10/9/2007
Kingunge ashangaa kupondwa ziara ya mawaziri
Na Beatrice Charles
Mwananchi

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Kingunge Ngombale Mwiru amewashangaa
wananchi wanaolalamika kuwa ziara ya mawaziri waliopelekwa na serikali
mikoani kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kufuja fedha
za umma.

Akizungumza jana na baadhi ya viongozi wa kata za Ilala, mkoani Dar es
Salaam, Kingunge alisema tangu Tanzania ipate uhuru mawaziri walikuwa
wanafanya ziara mikoani na kwamba ni sehemu ya kutekeleza wajibu wao.

"Nawashangaa wananchi ambao wanahoji kwamba kwanini mawaziri wanafuja
fedha za serikali kwa kufanya ziara mikoani badala ya kwenda wabunge
husika kwenye mikoa yao," alisema Kingunge bila kufafanua zaidi.

Alisema mawaziri si watu wa kukaa ofisini tu na ndio maana wametumwa
katika mikoa mbalimbali kufafanua kuhusu mjadala wa bajeti uliozua
maswali mengi baada ya bajeti hiyo kutangazwa bungeni Julai mwaka huu
na Waziri Zakia Meghiji.

Kingunge alisema moja ya mipango ambayo yataiwezesha Serikali kuingia
katika mkondo wa maendeleo ni kwenda kwa wananchi kuwaeleza mikakati
ya uwezeshaji ili kila mwananchi aweze kushiriki katika kujenga uchumi
imara wa taifa.

"Ili tujenge msingi wa kiuchumi wa kisasa na maendeleo ya sayansi na
teknolojia inatupasa kushirikiana, yaani wananchi na serikali".
alisema Ngombale Mwiru.

Mbali na hayo, alisema moja ya michakato katika ilani hiyo ni
kuendeleza elimu, huduma ya afya na miundombinu na njia ya kutekeleza
hayo, serikali iliamua kuwapeleka mawaziri mikoani ili kuwaeleza
wananchi mambo yanayotarajiwa kufanyika.

Naye Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza,
alisema kwa upande wa kuboresha elimu, serikali katika bajeti yake ya
2007/08 imetenga Sh1.5 trilioni kwa ajili ya elimu ya awali, msingi,
sekondari na vyuo.

Mahiza alisema wananchi wakipata elimu wataondokana na ujinga na
hatimaye kuweza kufanya kazi za kilimo kwa kuwa sekta hiyo inahitaji
wasomi wa kutosha.

Alifahamsha kuwa serikali ina mikakati ya kujenga shule za sekondari
za kidato cha tano na sita katika kila tarafa ifikapo mwaka 2010.

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages