Created by Edward chacha on Oct 30, 2006
Category: National Affairs
Region: Tanzania
Target: Tanzania citizens
Description/History:
Lengo
letu ni kukusanya sahihi zipatazo milioni moja na kuziwakilisha kwa
Rais Kikwete tukiitaka serikali iwekeze kwenye mradi wa Stieglers
Gorge, uliopo kwenye bonde la mto Rufiji wenye uwezo wa kuzalisha umeme
wa Megawatt 2100 [mwingi wa kutosha na hata mwingine kubaki na kuuzwa
nje ya nchi] ili tuweze kuondokana kabisa na tatizo hili la kukatikiwa
na umeme, tatizo ambalo ni aibu kubwa kwa taifa letu.
Petition:
Stieglers
Gorge ni nini hasa?--Stieglers Gorge ni mpalio mwembaba unaopatikana
kwenye bonde la mto Rufiji, kilomita 374 toka jijini Dar es salaam. Kwa
utafiti uliowahi kufanyika mwishoni mwa miaka ya sabini na mwanzoni mwa
miaka ya themanini [ 1978-1980] kwa ushirikiano wa RUBADA [Rufiji Basin
Development Authority] na M/s Norplan/Hafslund, ilionekana kwamba mradi
wa Stieglers Gorge una uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme mwingi kwa njia
ya maji [Hdro-power] zaidi ya umeme ambao Tanzania ilikuwa ikihitaji
katika miaka hiyo.
Matokeo ya utafiti huo pia yalionyesha kwamba, mpalio wa Stieglers una
uwezo wa kuhimili mitambo mitatu mikubwa ya kuzalisha umeme [3 power
stations]. Mtambo 'A' wenye uwezo wa kuzalisha megawati mia nne (400MW)
ambao ungefungwa upande wa kaskazini mwa bwawa [dam]. Mtambo 'B' wenye
uwezo wa kuzalisha megawati mia nane (800MW) ambao ungefungwa upande wa
chini ya bwawa, na mtambo 'C' wenye uwezo wa kuzalisha megawati mia
tisa (900MW) ambao ungefungwa upande wa kusini mwa bwawa. Jumla
megawati elfu mbili mia moja [2100MW].
http://www.gopetition.com/online/9995.html
The TUPATIENI 'STIEGLERS GORGE' petition to Tanzania citizens was written by
Edward chacha.
The petition is hosted free of charge at www.gopetition.com. There is
no express or implied endorsement of this petition by gopetition.com
pty ltd.
---------------
Subi / nukta77-----------------------