Bastola hiyo ambayo bado inaendelea kusakwa, inadaiwa kupotea wakati wa
purukushani zilizofanyika mara baada ya tukio hilo la kuuawa kwa dereva
wa daladala pale kwenye makutano ya barabara za Bagamoyo na ile ya
kuelekea Kawe.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Dito ameieleza polisi kuwa silaha hiyo
ilipotea muda mfupi baada ya tukio ambapo kundi la watu lilimvamia na
kumfanyia vurugu iliyosababisha upotevu wa bastola hiyo.
Kufuatia kuyeyuka huko kwa bastola, polisi hivi sasa ingali ikiendelea
na msako kabambe wa kuitia mikononi.
"Hivyo napenda kukuarifu kuwa nimekubali ombi lako la kujiuzulu wadhifa
wa Mkuu wa Mkoa. Kwa mara nyingine tena pole kwa yote. Usiache
kumshukuru na kumuomba Mungu."
Hayoni maneno ya Rais Jakaya Kikwete akikubali kujiuzulu kwa Mkuu wa
Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile-Mzuzuri, anayekabiliwa na kesi ya
mauaji ya raia mjini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma
jana usiku, Rais Kikwete amekubali ombi hilo kufuatia barua
aliyoandikiwa na Ditopile Jumapili iliyopita, siku moja kabla ya
kufikishwa mahakamani, akimuomba Rais akubali kujiuzulu kwake.
Rais alieleza: "kuomba kwako kujiuzulu wadhifa wako wa Mkuu wa Mkoa ni
uamuzi wa busara na hekima. Unatoa fursa kwa taratibu stahiki za
kisheria kufanyika bila ya vizuizi visivyokuwa vya lazima. Ni heshima
kwa taifa letu linalozingatia utawala wa sheria.
Wajuzi wa mambo wanadai Braza Dito ilikuwa lazima aachie ngazi tu, hata
kama asingetangaza kujiuzulu kulingana na kosa linalomkabili lazima
angevuliwa cheo hicho.
"serikali leo imetembelea familia ya hayati hassan mbonde dereva wa
daladala aliyepigwa risasi na mshukiwa ditopile mzuzuri, na kutoa pole
kwa wafiwa na ubani wa 500,000/- . hapo ni katibu mkuu kiongozi mh.
philemon luhanjo akikabidhi ubani kwa baba mzazi wa marehemu mh. mzee
mbonde huko kawe. jk pia katuma salamu za rambirambi na inatarajiwa
atakwenda kuhani pindi arudipo safari, meibii jumapili hivi. mh. mzee
mbonde amemwambia mh. luhanjo kwamba hayati hassan ndo lilikuwa tegemeo
la familia, na kuondoka kwake ni pigo kubwa kwao"