Kiwango cha kufaulu chashuka NA Matokeo ya Form Four

102 views
Skip to first unread message

Mariam

unread,
Feb 13, 2006, 3:43:59 PM2/13/06
to Kilimanjaro Forum
Matokeo ya Form Four
www.moec.go.tz/nectaResults/OLEVEL.htm

Kiwango cha kufaulu chashuka
http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2006/02/12/59897.html

12 Feb 2006
By John Ngunge

Baraza la Mitihani la Tanzania limewataja wanafunzi wa kike na kiume 20
bora kitaifa waliofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza kidato cha
nne mwaka jana.

Majina hayo yalitajwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Joyce
Ndalichako jijini Dar es Salaam wakati akitangaza rasmi matokeo ya
mtihani wa kidato cha nne.

Hata hivyo, Dk. Ndalichako alisema kwa ujumla kiwango cha kufaulu cha
wanafunzi kimeporomoka ikilinganishwa na mwaka juzi.

Aliwataja watahiniwa hao kwa kuanzia na wa kike 10 bora kitaifa na
majina ya shule wanazotoka katika mabano kuwa ni msichana Wende Aman
(St. Francis), Rashida Rashid (St. Francis), Dorothea Kahindi
(St. Francis), Happy Mathew (Marian Wasichana), Jacqueline T. Killenga
(St. Francis), Niwaeli Elisante (Agape Seminari), Nellin Njovu (St.
Francis), Falecia Massacky (Marian Wasichana), Alphoncina Kagaigai
(Marian Wasichana) na Caroline Cosmas (Marian Wasichana).

Kwa upande wa wavulana, Dk. Ndalichako aliwataka watahiniwa 10 bora
kitaifa kuwa ni Kado E. Damball (Maua Seminari), Ibrahim Shafi (Tanga
Sekondari), Hussein Hamidu (Tanga Sekondari), Patrick N. Sungura
(Mzumbe), Deodatus O.

Mkongwa (St. Joseph-Kilocha), William Mgisha (Itaga Seminari), Goodluck
Mlwilo (Mzumbe), Abiud K. Thomas (Umbwe), Mustapha Nuru (St. Anthony)
na Divine B.R. Miho (Brooke Bond).

Matokeo ya Baraza la Mitihani la Tanzania yanaonyesha kuwa jumla ya
watahiniwa wote waliofaulu mtihani wa kidato cha nne uliofanywa Oktoba
mwaka jana kwa madaraja ya I-IV ni 102,064 sawa na asilimia 83.84 huku
watahiniwa 19, 670 sawa na asilimia 16.16 wakiwa wameshindwa.

Idadi ya wanafunzi waliofaulu mwaka juzi (2004) madaraja ya 1-1V,
ilikuwa ni 79,838, sawa na asilimia 87.11.

Aidha Baraza hilo limefuta matokeo yote ya mtihani wa kidato cha nne ya
watahiniwa 101 wa shule na watahiniwa 37 wa kujitegemea waliobainika
kufanya udanganyifu katika mtihani huo.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Ndalichako, alisema kuwa idadi ya
watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne wa mwaka jana katika
madaraja ya 1-1V imeshuka kwa asilimia 3.27 ikilinganishwa na ya mwaka
juzi.

Hata hivyo hakueleza sababu za kushuka kwa ufaulu huo ingawa alisema
Baraza lake litafanya utafiti wa kujua sababu hizo hapo baadaye.

Jumla ya wanafunzi 121,734 walifanya mtihani wa taifa wa kumaliza
kidato cha nne Oktoba mwaka jana.

Alisema katika mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2004,
watahiniwa 1,307 wa shule na watahiniwa 237 wa kujitegemea walibainika
kufanya udanganyifu na matokeo yao yote yalifutwa.

Aidha Dk. Ndalichako alisema Baraza lake limesitisha kutoa matokeo ya
mtihani kwa watahiniwa 19 wa kujitegemea ambao hawakukamilisha taratibu
za usajili wa mtihani huo na matokeo hayo yatatolewa mara
watakapokamilisha taratibu husika.

Kwa upande mwingine alisema Baraza lake limesitisha kutoa matokeo ya
mtihani kwa watahiniwa 36 wa shule kutokana na watahiniwa hao kutokuwa
na alamaza maendeleo ya kila siku.
Alisema matokeo yao yatatolewa mara baada ya wakuu wa shule/vyuo
watakapowasilisha alama za maendeleo ya kila siku za wanafunzi husika.

Dk. Ndalichako alizitaja shule 10 bora katika matokeo ya mtihani wa
mwaka jana kuwa ni Sekondari ya Wasichana ya St. Francis (Mbeya),
Sekondari ya Wasichana ya Marian (Pwani), Maua Seminari (Kilimanjaro),
St. Mary Goreti (Kilimanjaro), Mzumbe (Morogoro), St. James Seminari
(Kilimanjaro), Sekondari ya Wasichana ya Visitation (Kilimanjaro),
Sekondari ya Kibaha (Pwani), St. Mary's Juniour (Pwani) na Sekondari
ya Msolwa (Morogoro).

Kwa upande wa shule 10 za mwisho, Dk. Ndalichako alizitaja kuwa ni
Sekondari ya Chemchem (Singida), Sekondari ya Jongwe (Pemba), Sekondari
ya Sahare (Tanga), Sekondari ya Mbaramo (Tanga), Sekondari ya Kitangiri
(Mtwara), Sekondari ya Nyangao (Lindi), Sekondari ya Kange (Tanga),
Sekondari ya Wari (Kilimanjaro), Sekondari ya Nandembo (Ruvuma) na
Sekondari ya Mawaal (Tanga).


* SOURCE: Nipashe

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages