BIASHARA UNAZOWEZA KUANZISHA BILA KUWA NA MTAJI MKUBWA
KUTOKA DILEX BUSINESS SOLUTION
Inaandikwa na Alex Mr motivation
(1) KUANZISHA KAMPUNI ZA USAFI
Usafi ni changamoto kubwa kwa wengi kwa maana hiyo unaweza kuitumia changamoto hii kama fursa. Katika kipengele hiki kuna kampuni tatu au biashara tatu ambazo unaweza kufungua, kwanza ni kampuni ya kufanya usafi majumbani, kampuni ya kufua ‘dry cleaning’ na tatu ni kampuni ya kufanya usafi wa mazingira.
Kufanya usafi wa majumbani ni changamoto kubwa kwa watu ambao wapo makazini, wanaweza kuwa na wafanyakazi wa majumbani lakini hawawezi kufanya kila kitu. Unaweza kuanza kufanya kazi hiyo, hapa nivizuri ukijitambulisha kama brand ya biashara na si mtu binafsi.
Anza kujitangaza hivyo katika mitando ya kijamii na kwa marafiki zako. Onyesha huduma utakzokuwa ukitoa kwa maana ya package nzima ya usafi wa majumbani, Unaweza kuwa ukifanya usafi wa nyumba nzima kwa ujumla kwa maana ya ndani, kufanya usafi wa nguo na kufanya usafi wa nnje, kwa maana ya kuzunguka nyumba.
Yote haya unaweza kufanya mwenyewe au kutafuta vijana ambao unawaamini mkashirikiana nao. Ni biashara ambayo inahitaji mtaji mdogo kwakaua ni ya kutumia nguvu ila mkijipanga vizuri inalipa na inaweza kuwa kampuni kubwa mpaka kukua na kuanza kufanya usafi katika maofisi makubwa.
Kwa maana hiyo basi usijali kwa kuanza kufua nguo za watu au kusafisha nyumba za watu kuwa na malengo ya kumiliki kampuni ya kufanya usafi majumbani na maofisini. Unaweza pia kuomba kufanya usafi katika maofisi madogo madogo au katika vibanda vya biashara.
Njia ya pili ni kufua, hii naamini inatambulika na nirahisi, unaweza kuanza kwa kufua nguo za majirani zako. Watu wengi wanaofanya kazi hasa vijana wakiume na mabinti ambao hawajaolewa huona uvivu wa kujifulia wenyewe. Kama wewe huna ajira kuliko kukaa tu hii ni fursa ya kufungua kampuni ya kufua nguo, anza kwa kufua nguo kwa mikono na mtaji utakaohitaji ni sabuni karai, maji na nguvu zako.
Wengi wanaweza kudhani inadhalilisha lakini lengo likiwa ni kufungua kampuni kubwa kwa kazi hiyo, kumiliki mashine, malengo makubwa yatakuondolea ile hali ya kudhalilika. Lakini unaweza usifue wewe, ukakusanya nguo kisha ukatafuta watu ambao hawana ajira na kuwalipa kidogo, kazi yako ikawa ni kuwasimamia tu, ukawa bosi wao.
Njia ya tatu ya kujiajiri kupitia kufanya usafi ni kwa kufanya usafi wa mazingira hasa mitaani. Ingawa kuna makampuni ya kukusanya uchafu na mengine ya kufanya usafi mijini katika baadhi ya mitaa, lakini bado suala la uchafu ni changamoto. Makampuni haya hayafiki maeneo mengi na hata yakifika hayafanyi kwa kiwango kinachotakiwa.
Unaweza kuanzia hapo, fika sehemu zenye wafanyabishara au nnje ya nyumba za watu, ongea na wamiliki uwe unafanya usafi. Kwa maana kuwa wakati wengine huishia kukusanya takataka tu, basi wewe safisha kabisa, nnje ya maofisi na maeneo ya biashara. Nirahisi watu hawa kukuchangia kidogo kuliko kuishi na uchafu hasa katika kipindi hiki ambacho serikali imelitilia mkazo suala la usafi.
Vifaa hapa ni ufagio na unaweza kutengeneza fursa nyingine kwa kuomba vifaa kwa makampuni makubwa kama ya simu, mabenki na mengine. Kusanya vijana watatu, wanne kama wewe ambao hawana ajira kisha anzeni kufanya usafi nnje ya ofisi moja kubwa, katika maeneo ya biashara kwa kuelewana na wamiliki kuchangia kidogo.
Mkishafanya hivyo baada ya muda mnaweza kujisajili kama kikundi cha mazingira hi vyo kuwa rahisi kuomba msaada wa vifaa vya usafi. Hapa mnafanya hivi mkiwa na lengo la kufungua kampuni ya kufanya usafi. Kampuni za usafi ni moja kati ya makampuni ambayo yanalipa sana kwakuwa uchafu huzalishwa kila siku na nilazima uondolewe.
Mnaweza kufanya kazi ya sample katika maeneo ya watu. Kikundi cha vijana watano mkianza kufanya usafi kwenye sehemu sugu, sehemu ambazo kuna malalamiko mengi, kuna uchafu mwingi, jitoleeni kufanya usafi na watu wakiona matokeo ya kujitolea kwenu ni rahisi kuwaunga mkono na kuwalipa kidogo.
Pigeni picha mkifanya kazi hizo, picha za kabla ya kufanya usafi na baada ya kufanya usafi na zitumieni kujitangaza katika mitandao ya kijamii. Jipeni jina kama kikundi jina ambalo litakuja kubadilika na kuwa jina la kampuni yenu. Nirahisi kufanikiwa kama akili zenu mtazielekeza katika kutoa huduma bora na si kupata fedha za haraka.
Hapa mtakua mmetumia nguvu zenu kujiajiri, fanyeni utafiti juu ya uendeshaji wa makampuni ya usafi, jifunzeni namna ya kukua, changamoto ya usafi ni kubwa kwa wengi, majumbani na mitaani, igeuze hii kuwa fursa ya kuyabadilisha maisha yako na kuondokana na utegemezi, fursa ya kumiliki kampuni ya usafi.
(2) KUANDAA MATUKIO
Wazungu wanaita “Event Management” kuna aina nyingi sana za matukio ambayo unaweza kuandaa, kwa bahati nzuri sasa hivi hakuna mtu ambaye anataka kufanya sherehe yake mwenyewe, kila mtu anataka mtu wa kumsaidia kufanya hivyo. Siku hizi hata misiba inahitaji mtu wa kuiandaa.
Kinachohitajika hapa ni ubunifu tu na kujuana na watu. Unaweza kuanzisha kampuni ya kuanza matukio kwanza kwa kuwa kama dalali, kwa maana ya kutafuta sharehe na kuzitafutia kampuni au watu ambao tayari wanabiashara hizi kuandaa. Kwa maana kuwa ingawa lengo lako ni kumiliki kampuni yako, lakini silazima usubiri mpaka upate mtaji.
Kazi yako ni kukusanya taarifa za matukio na sherehe kisha kuyachukua na kutafuta waandaaji wa kuaminika. Unaweza kuyachukua kama wewe kwa kuwa wakala kwa maana ya kujitambulisha kama sehemu ya kampuni au kuwa na kampuni yako mwenyewe kisha baada ya tenda ukawapelekea wahusika, au ukatafuta tu tenda na kuziuza.
Nibiashara rahisi kama utajuana na watu wa maofisini ambao wanahitaji sherehe na makongamano, ukajuna na ma MC ambao hujuana na watu wanaohitaji kuandaa sherehe, ukajuana na wadada wa kupamba saluni ambao ni rahisi kupata taarifa za sherehe. Tumia fursa hii kujifunza ukiwa na malengo ya kuanzisha kampuni yako.
Lakini pia unaweza kuanza kwa kuandaa matukio yako mwenyewe, silazima iwe sherehe kubwa, harusi, kongamano au tukio kubwa mabalo linajulikana na watu. Hapa kikubwa unachohitaji ni wazo la kufanya biashara hii, kumiliki kampuni ya kuandaa matukio. Kisha itafutie jina zuri na chambua shughuli ambazo kampuni yako itakuwa ikufanya.
Kwa maana kuwa tengeneza kampuni yenye jina hata kama si iliyo sajiliwa kisheria, kisha chambua majukumu yake, kwa mfano kuandaa harusi, vipaimara, makongamano, mikutano na matukio mengine. Unaweza kuanza kazi kwa kuandaa tukio lako mwenyewe na hapa ndipo ubunifu unahitajika.
Watumie rafiki zako au ndugu ambao mpo karibu. Unaweza kutangaza tu kuwa umeandaa get together ya watu mlosoma nao, walosoma chuo fulani, kutoka mkoa fulani na vitu kama hivyo. Chambua tukio litakavyokua, labda chakula cha mchana au jioni, mziki mzuri na makorokocho mengine, kisha tangaza kiingilio.
Hawa ni watu ambao mnafahamiana hivyo nirahisi kukuamini. Tafuta hoteli nzuri kisha mfuate mmiliki na muambie kitu uanchotaka kufanya, muambie ukweli kuwa unataka kuwakutanisha watu fulani pale, hapo nirahisi kukudhamini kwa mfano kukupa ukumbi wakati mkinunua vinjwaji na chakula kwake.
Hilo ni jambo la kawaida na nirahisi kukubali kwani atauza chakula. Kwake itakuwa sawa tu na wateja wakawaida kuja kula pale na kuondoka, kuendelea kubaki baada ya chakula inamaana mtaendelea kutumia vinywaji hivyo ataendelea kutengeneza faida.
Kwakuwa watu watanunua tiketi au kutoa kiingilio kabla ya tukio, basi nirahisi kuandaa tukio kama hili bila kutumia hata senti tano kutoka mfukoni kwako. Anza na watu unaowafahamu kwakuwa ni rahisi kukuamini na rahisi kuwatangazia kwani unaweza kutumia mitandao ya kijamii kuwapa habari na kuhamasisha kuhusu tukio.
Kumbuka hata kama utapata watu watano au wawili kwako ni mafanikio, utakuwa umenza safari ya tukio lako. Siku ya tukio beba Business Cards ambazo unaweza tengeneza kirahisi kujitangaza kwako. Wape zile kadi zikionyesha mawasiliano yako na biashara unayofanya, hawa ndiyo watakusaidia kukutangaza na kukutafutia wateja.
Kuwa na malengo makubwa ya kikampuni lakini anza kidogo, anza hata kwa ndugu kwa kuwaambia mtoke siku moja kubadilishana mawazo. Kwa maana kuwa, silazima kusema kiingilio, mnaweza kuamua kuchangishana tu na kutafuta sehemu mkatoka. Muhimu ni wewe uwe umeandaa tukio na utengeneza faida hata kama ni kidogo.
(3) KUWA MC
Anza kuwa MC katika matukio madogo madogo kama vile kipaimara, ubatizo, sherehe za familia, sherehe za siku za kuzaliwa, sherehe za ofisi na nyingine ndogo ndogo. Hizi zitakusaidia katika kutengeneza kujiamini na kuweza kuongea mbele za watu, ukiweza huko ni rahisi kupanuka na kuanza kujitambulisha kama MC.
Ukishaweza kujijengea kujiamini, kujua nini cha kuongea basi nirahisi kuwa MC, changamoto katika kazi hii ni kupata shughuli za kusherehesha. Anza na marafiki zako wa karibu, watumie hawa kutafuta sherehe, tengeneza urafiki na watu wa saluni za kike, wauza nguo za maharusi, wapambaji, wamiliki wa kumbi za sherehe na watu wengine ambao wanajishughulis
ha na mambo haya.
Tengeneza umaarufu wako katika mitandao ya kijamii, kwa maana kuwa vaa kiheshima, weka picha za kiheshima na anza kupost mambo yanayohusiana na sherehe. Kwa mfano unaweza kuwa unatoa tips za namna ya bibi harusi anavyopaswa kuingia kwenye kumbi, namna ya kufungua shampeni, namna ya MC anavyopaswa kuwa na mambo mengine mengi ya kisherehe.
Hii itawastua watu wako wa karibu kuona unajua sana mambo ya sherehe, tips hizi zinapatikana katika mitandao, google na weka picha za sherehe. Kisha jitambulishe kama MC, unaweza kubadili jina lako katika mitando ya kijamii na kuanza na neno MC ili kuwavuta watu na wakioanisha na kile unachokiandika ni rahisi kukuamini.
Lakini usiishie hapo, unaweza kutengeneza blog kwaajili ya kuchambua mambo hayo ya u MC na sherehe kwa ujumla, weka picha, chambua namna ya kuandaa matukio ya kiofisi. Blog hiyo unaweza kuitumia pia kuweka picha za sherehe ambazo unaalikwa, kwa maana kuwa kila baada ya sherehe, unatangaza kuwapa ofa maharusi ya kutangaza picha zao katika mitandao yako ya kijamii na katika blog yako bure..
Ninaposema MC namaanisha mshereheshaji, si lazima kuwa wa harusi, kitchen party au sherehe kama hizo. Unaweza kuwa pia wa matukio ya kiofisi, mikutano na vitu vingine. Usiifunge akili yako sehemu moja, unaweza kufanya hivyo kwa lengo la kuwa MC tu au baadaye kuja kuanzisha kampuni ya kuandaa matukio.
(4) BIASHARA YA MAZAO
Upo kijijini sehemu ambayo kuna kilimo cha aina yoyote au upo mjini sehmu ambayo mazao ya kilimo ni ngumu sana kupatikana. Hii kwako inaweza kuwa fursa kama utaitumia vizuri kwa kuamua kuwa dalali wa mazao. Unaamua kuwa dalali kwa lengo la kuufanya udalali wa mazao kama kazi yako au kwa lengo la kuja kuwa mfanyabiahsara wa mazao lakini pia kwa lengo la kupata tu mtaji kwaajili ya kufanya kitu kingine..
Kuna wanawake ambao wamelazimika kwenda vijijini kuishi na waume zao ambao wameajiriwa huko, unawakuta wapo tu majumbani wakilalamika hawana mitaji ya kufanya biashara lakini ukichunguza kidogo pale kijijini watu hulima mahindi, mpunga au maharage kwa wingi sana, jambo ambalo husababisha vitu hivi kuuzwa kwa bei rahisi sana.
Lakini mtu huyu alitoka mjini na huko vitu ni bei ghali, kule mjini nako kuna mtu ambaye hana kazi yupo tu. Bila kujali uko wapi unaweza kuamua kuwa dalali wa mazao hasa ya chakula na kuingiza pesa bila kuhitaji kuwa na mtaji wowote ule.
Kwa wale ambao wapo sehemu ambayo mazao huzalishwa unaweza kuchukua muda wako kukusanya mazao, hata si kwa kununua, kwa oda, kwamba kukusanya watu ambao wanamazao na kuwaweka tayari kwa mazao yao kununuliwa. Kazi yako hapa itakuwa ni kuangalia kuhakikisha ubora kisha unaweka rekodi kuwa mhusika ana mazao kiasi gani?
Ukishafanya hivyo basi unaanza kutafuta wateja, wanaweza kuwa mjini, kwa maana kwa kwenda au kuwasiliana na ndugu au rafiki aliyeko huko kukutafutia masoko. Au kwa kusubiri wafanyabishara wakubwa wanapokuja kijijini kutafuta nafaka unawashika mkono na kuwapeleka kwenye watu wako.
Kwa maana kuwa mwanzo unakuwa umeanza kwa kukusanya kwa ahadi ya kuja kununua lakini kadri siku zinavyoenda unaweza kuwa unanunua unahifadhi na kuuza wewe. Lakini pia kwa uliyemjini unaweza kuanza kufanya kazi ya kukusanya wateja, unatembelea wanunuzi na kukusanya oda kisha unatafuta wauzaji na kuwaunganisha.
Kitu cha muhimu hapa ni kujua kuongeza, kuwasiliana na watu vizuri na kubwa kabisa kujua watu sahihi katika biahsara hiyo. Tengeneza mawasiliano na madereva na makondakta wa malori ambao ndiyo hununua mazao vijijini na kuyaleta mjini, hawa watakusaidia kukuunganisha na wakulima pamoja na wafanyabishara wakubwa.
DILEX BUSINESS SOLUTION
Kama una wazo la kufanya biashara hapa Tanzania na ungependa kumiliki kampuni yako au jina la biashara lako,* huduma yetu ni kukusaidia kufaniki
sha usajiri wa biashara yako. Tutumie message yenye neno "KAMPUNI" Whatsapp namnba 0716762015 kupata maelezo zaidi juu ya huduma yetu.
SASA NAHITAJI KUTENGENEZA BUSINESS PROFILE NA KUSAJIRI KAMPANI YANGU,NITAWAPATA WAPI DILEX BUSINESS SOLUTION??
Tumia hayo mawasiliano hapo chini kuwasiliana na Dilex business solution au fika offisini kwetu Tunapatikana, Mwalimu.J.K.Nyerere Trade Fair ground(SABA SABA), PLOT No.436, BLOCK A, Kilwa Road, Dar es salaam, Tanzania
Contact us DILEX BUSINESS SOLUTION
WHATSAPP GROUP : TUCHEKI 0716762015
FACEBOOK PAGE: Dilex business solution
FACEBOOK PAGE: DILEX Inspire
WHATSAPP :0716762015
Instagram: Dilex business solution