Imani

43 views
Skip to first unread message

Honorati Manang

unread,
Aug 3, 2011, 5:33:44 AM8/3/11
to iman...@googlegroups.com
Imani nini? Imeandikwa waebrania 11:1 "Basi imani ni kuwa na hakika ya
mambo yatarajiwayo ni bana ya mambo yasiyoonekana."

Yesu ndiye mwanzo wa imani imeandikwa Luka 17:5 "Mitume wakamwambia
Bwana tuongezee imani." Warumi 10:17 yasema "Basi imani chanzo chake
ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo."

Imani ya haki ni kuamini yote ambayo Yesu ametutendea. imeandikwa
Warumi 5:1 "Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe
na imani kwa Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu kristo."

Imani ni kuwana imani kwa Mungu katika mambo yote. imeandikwa
Waebrania 10:38 "Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani naye
akisita-sita Roho yangu haina furaha naye."

Imani dhaifu yaweza kuwa yenye nguvu Mungu akimsaidia imeandikwa Marko
9:24 "Mara babaye yule kijana akapaza sauti akasema Naamini nisaidie
kutokuamini kwangu."

Honorati Manang

unread,
Aug 4, 2011, 9:09:54 AM8/4/11
to iman...@googlegroups.com
Chanzo cha Imani ni Kujua. Kujua hutokea kwa Kusikia au kuona:

Kuna maadui wakubwa wa imani ambao ni Kukosa maombi na kutosoma Neno
la Mungu: Warumi 10:17 “Imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja
kwa Neno la Kristo” katika Nehemia 8:10 “…….kwa kuwa furaha ya Bwana
ndio nguvu zenu”, nguvu ni imani inayokufanya uone njia pasipokua na
njia yale unayoona hayawezekani kwako yatawezekana. Furaha inanipa
nguvu yakufanya mambo ambayo wengine hawawezi kufanya.
Pasipo furaha huwezi kufanya lolote utakuwa mwenye huzuni. Katika
kufanya maombi na kusoma Neno la Mungu, nitakuwa na furaha ambayo ni
IMANI ya kupokea nisiyostahili. Pia Hofu ni adui wa imani: Hofu ni
siraha kubwa ya shetani. Kile unachowaza kupokea kwa imani mfano
kupata kazi nzuri, mke mwema, uponyaji n.k shetani huleta hofu. Na
hofu huondoa imani yako na yale unayoogopa yasikupate yatakupata maana
umefungua moyo wako kwa shetani, kile unachoumba katika hofu
kitakupata.
Ni vizuri tuwe watu wa maombi na kusoma Neno la Mungu, likae ndani ya
mioyo yetu ili IMANI ifanye kazi zaidi ya tulivyoamini, hofu haitapata
nafasi kwetu bali tutakuwa majasiri.

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages