Ndugu zangu Wana Bunge baada ya kuamka sasa ni wakati wa kupanga mipango katika kufikisha adhima yetu.Ni kweli sote tuliona ile post kwenye Michuzi Blog,mie binafsi nachukulia kama ni changamoto katika kujipanga na kuona jinsi gani tutaisaidia shule yetu.Shule ambayo ilituanzishia safari yetu ya kielimu hapa duniani ukizingatia kwa miaka ile wengi wetu tulijua "kusoma na kuandika katika ngazi ya shule ya msingi. Turudi tulipotoka ndugu zangu na ni haki ya shule ya msingi Bunge kufaidi matunda yake kutoka kwetu. Pendo wazo lako ni zuri sana lakini kabla tujiweke kisheria zaidi na uwezo ndugu yetu Pendo alishawahi kutuma mfano wa Katiba naomba nijitolee kuipitia halafu niilete hapa kwa ajili ya kupata kuchangiwa na nyie wadau. Mwisho naomba nililete kwenu tena na nahitaji ruhusa yenu "NATEGEMEA kukutana na SPIKA wa BUNGE Mheshimiwa Mama Anna Makinda katika masuala yangu ya kichama lakini ningelipenda kuzungumza nae kuhusiana na suala letu la kuwaleta wanabunge pamoja na kumgusia kuhusu umuhimu wa Taasisi yake anayoingoza(BUNGE) na shule yetu. Wako. Lyana Abdullah Zulu, Seven Commando,1996. NB:Naombeni dua zenu ndugu zangu nategemea kuanza harakati zangu za UBUNGE 2015 mwezi huu,mwezi ambao kwangu binafsi una heshima kubwa kwa maana ya kuwa ni mwezi ambao NIMEZALIWA,naombeni dua zenu,baraka zenu hata changamoto pia nazipokea......NAOMBA kuwasilisha.
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
Date: Thu, 1 Aug 2013 16:06:41 +0000