HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBIL
UFAFANUZI KUHUSU MATIBABU YA WAGONJWA WA SELIMUNDU (SICKLE CELL)
Gazeti la Mtanzania toleo Na. 8162 la Aprili 22, 2016 limechapisha taarifa kwenye ukurasa wake wa mbele yenye kichwa cha habari “Wagonjwa
wa sickle cell hatarini Muhimbili”. Aidha vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo televisheni pamoja na radio na mitandao ya kijamii imezungumzia suala hili.
Kutokana na taarifa hiyo, Hospitali ya Taifa Muhimbili inapenda kutoa ufafanuzi wa jambo hili kama ifuatavyo;
-
Tunapenda umma uelewe kuwa huduma hii haijasitishwa na wala Hospitali haitasitisha utoaji wa huduma hiyo. Watu wanaoeneza uvumi kuwa huduma hii imesitishwa wana maslahi yao binafsi kuhusu tiba ya wagonjwa hawa.
-
Ni kweli kwamba takribani miaka kumi kulikuwa na mradi uliokuwa ukifadhili matibabu pamoja na utafiti wa wagonjwa wa selimundu ambao muda wake umeisha tarehe 31 Machi 2016. Mradi huu kwa sababu ya utafiti ulihitaji
wagonjwa wote wa selimundu kuja Muhimbili kwa ajili ya utafiti na tiba. Hivyo basi hali hii ilisababisha wagonjwa wengi wanaohitaji huduma ya selimundu kuja Hospitalini hapa licha ya kwamba mahitaji yao hayakuhitaji watalaamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
-
Tunaomba jamii ikumbuke kwamba hata kabla ya mradi huo, Hospitali ilikuwa inatibu wagonjwa wa selimundu waliokuwa wanapata rufaa kuja hapa kutokana na matatizo yaliyokuwa yanajitokeza ya ugonjwa huu.
-
Hivyo baada ya mradi huo kuisha muda wake Hospitali ya Taifa Muhimbili imewaingiza wagonjwa wa selimundu katika mfumo wa kawaida wa matibabu kama wagonjwa wengine. Hii ina maana kwamba wagonjwa wenye selimundu wasiohitaji
huduma ya watalaam wetu wataendelea na huduma katika hospitali zilizopo karibu nao na wagonjwa watakao onwa Muhimbili ni wale watakaopata rufaa kufuatana kutokana na matatizo wanayopata.
-
Naomba ieleweke kwamba wagonjwa wa selimundu wanaohitaji huduma yetu watatibiwa kama wagonjwa wengine wote wanaotibiwa Hospitalini hapa kwa mjibu taratibu na kanuni zilizopo bila ubaguzi wowote.
Imetolewa;
![]()
Aminiel Aligaesha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma
Aprili 22, 2016
Aminiel Buberwa Aligaesha,
Head of Public Communication and Customer Care Unit,
Muhimbili National Hospital,
P.O. Box 65000,
DAR ES SALAAM.
Mobile: +255-755/715 648636