Novenakutoka neno la Kiitalia "novena" lenye asili katika Kilatini: novem, "tisa") ni mfululizo wa sala au ibada ambazo zinazunguka maombi maalumu ambayo kwa kawaida yanafanywa na Wakristo kwa siku tisa mfululizo[1].
Ingawa kuna aina mbalimbali za novena, lengo lake kuu ni kukuza imani, kujitolea, na kuomba msaada wa kutoka mbinguni katika shida au kwa maombi maalumu kama vile toba na msamaha au kwa ajili ya amani[2][3][4] .
Asili ya desturi hiyo ni siku tisa za sala zilizoshikwa na wafuasi wa Yesu huko Yerusalemu kati ya kupaa kwake mbinguni(siku ya 40 baada ya Pasaka) na Pentekoste (siku ya 50) kama walivyoagizwa naye ili wajiandae kujazwa Roho Mtakatifu waweze kumshuhudia ulimwenguni kote[5][6].
Katika Kanisa Katoliki[7], novena mara nyingi hufanywa kwa heshima ya nafsi mojawapo ya Mungu, Bikira Maria, malaika au mtakatifu fulani[8], lakini maarufu sana ni novena ya Huruma ya Mungu ambayo inaanzia Ijumaa Kuu, yaani siku tisa kabla ya Sikukuu ya Huruma ya Mungu, inayofanyika Jumapili ya Pili ya Pasaka. Wakatoliki wengi hushiriki katika novena hiyo kwa kufanya sala maalumu kila siku kwa siku hizo tisa, wakilenga kukuza huruma na upendo wa Mungu kwa njia ya maombezi ya Bikira Maria.
3a8082e126