Ndugu waheshimiwa, Marafiki zangu na wasomi wenzangu;
Nawasalim nyote katika jina la Bwana. Mwaka unaisha wengi hatujaonana ila naamini kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja nanyi, na mnaendelea vizuri. Nami sijambo.
Nipende kutumia nafasi hii kuwapongeza kwa mafanikio yote ambayo mmeyapata mwaka huu wa 2013. Mkumbuke kumshukuru Mungu sana. Pia pale kulipokuwepokuwepo changamoto/vikwazo, niwatie moyo kuwa Mungu anayo makusudi nanyi ndo mana mpo hai ili mshuhudie ukuu wake katika mwaka mwingine.
Natambua kuwa wapo wenzetu ambao hawajapata kazi rasmi kama matarajio yalivyo. Napenda kuwatia moyo kuwa msikate tamaa. Mungu hakutupatia ujuzi ambao hauwezi kutusaidia katika kuji kwamua na hali ngumu ya maisha. Kwa hiyo usijidharau, lakini kuwa na ujasiri katika kuthibitisha
kile unacho kijua, ninaamini muda si mrefu kila mmoja wetu atakuwa mahali fulani. Kwa wale ambao tumefanikiwa kuwa na kazi katika shirika fulani binafsi au la umma, tusiite kujishikiza, hata kama ni kwa muda( of coz tupo kwa muda mana hakuna aliyefunga ndoa na kazi hiyo) nashauri tufanye kazi kwa moyo, na umahiri, tusidhalilishe taaluma zetu. Pia tusiwe mafisadi; kukubali mapato yoyote yasiyo ya halali kuwa katika account zetu. Ni bora account isome "negative" (-ve) kuliko kuwa na fedha isiyo ya halali, hii ni pamoja matumizi ya fedha hizo. Kwakadiri tutakavyofanya kazi kwa uaminifu, Mungu atatupandisha kutoka hapo tulipo na kutuwezesha kuwa mahali tutakapoweza kuwasaidia wengine.
Ushauri wangu kuhusu swala la kazi; Kila mmoja wetu, walio ajiriwa na hata wasio ajiriwa, tuwe na mtazamo wa kujiajiri, tuajiri na sio kuajiriwa. Silazima tuanze na biashara kubwa. Biashara zote kubwa sasa zilikuwa ndogo wakati
fulani. Matajiri wote wakubwa sasa wengi wao huenda walikuwa masikini wakubwa miongo kadhaa iliyo pita, lakini walitumia fursa ndogo walizozibaini na wakaweza kufanya mambo yaliyowawezesha kufika walipo sasa. Wote wenye mishahara mikubwa sasa, ndio waliokua na mishahara modogo miaka kadhaa iliyopita; kwanini mimi ning'ang'ane kuanza na mshahara mkubwa sasa. Swali la kizushi "Hivi mshahara mkubwa au mdogo, ni shilingi ngapi!!, lini nitapata mtaji wa kuanzisha mradi flani endapo nasubiri mshahara mkubwa, kama sina uzoefu kigezo wanachokihitaji waajiri wengi binafsi, na wala si taaluma kubwa!"
Wote tunatambua kuwa wasomi wamekua wengi kuliko nafasi za ajira zilizopo. Tubuni miradi ambayo itatuwezesha kuajiri hata wale wasomi walioko nyumbani kwetu/kwenu ambao aidha wanaendelea na ngazi nyingine ya masomo, au wameshakua wana ujuzi wa kuajiriwa lakini hawajapata kazi rasmi (mf. wa darasa la saba, form IV, VI, na
hata vyuo). Hata ule wakati wanapokua likizo, wanaweza kutumika wakachangia kuingiza kipato kitakacho wasaidia kupata nauli na gharama zingine za matumizi yao madogo madogo hata makubwa. Ukweli ni kwamba hata mimi sijaanzisha mradi wowote, lakini nina mpango hayo. Wapo wenzetu wengi ambao mnanayo miradi tayari (huenda ni wewe) nawaombea kufanikiwa sana mtupe hamasa, pia mtutie moyo kwa ushauri ili nasi tuinuke.
Napenda kuwajulisha pia kua mie nishaoa hivi juzi (tar 9/12/2013) tarehe ya kumbukumbu ya uhuru wa taifa letu la Tanzania. Mke wangu anaitwa Rebecca. Nimeambatanisha picha baadhi za ndoa na harusi kuthibitisha hili. Tunawakaribisha nyumbani kwetu mkipata fursa ya kufika Morogoro.
Mungu awabariki sana, pia nawatakia mwisho mwema wa mwaka 2013, na mwanzo mzuri wa mwaka mwingine wa 2014, uwe wa mafanikio. Nawatakia pia sikukuu njema wapendwa.
"Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, Na Ushirika
wa Roho Mtakatifu Viandamane nasi sote Sasa na Hatamilele" Amen.