Miaka miwili au mitatu baadaye, bosi wangu alinikabidhi madaraka ya kusimamia eneo la ujenzi, kwa hivyo nilitia bidii zangu zote kazini na nikacha kuhudhuria mikutano mara kwa mara kama ilivyokuwa. Baadaye nilitambulishwa na rafiki kwa Bw. Li, mfadhili wa biashara, na tukaanzisha kampuni ya ujenzi pamoja. Nilifurahi sana, na niliazimia kuanza kufanya kazi kwa bidii kabisa. Kisha niliingia kabisa katika hekaheka za pesa na nikaacha kabisa kwenda kanisani kwenye mikutano. Nilitaka miradi ifanyike vizuri ili nipate sifa za wengine kwa ustadi wangu, kwa hivyo nilidai mengi zaidi kutoka kwa wafanyakazi. Niliwakemea kila nilipoona kuwa walikuwa wamefanya kitu ambacho hakikuwa sahihi au hakikufikia matakwa yangu. Kiongozi wa timu mara nyingi alibubujikwa na machozi kwa sababu ya tabia yangu mbaya. Wafanyakazi waliogopa kila waliponiona na hata walijificha. Hata watu ambao walikuwa marafiki wazuri hawakuwa wema kwangu na hawakutaka kuwa na imani kwangu tena. Kuona jambo hili kulihuzunisha sana. Bwana Yesu hutufunza tuwasamehe wengine sabini mara saba, na tumpende jirani yetu kama tunavyojipenda. Hata hivyo, sikuwa nimetia hayo katika vitendo hata kidogo, hata mara moja. Kwa hivyo huko kulikuwaje kuwa Mkristo? Nilijua kuwa nilikuwa nikitenda dhambi na mara nyingi nilimwomba Bwana, nikikiri na kutubu. Niliamua kubadilika. Lakini kila wakati jambo lilipotokea, bila kujijali bado nilitenda dhambi. Nilichukizwa sana.
Kama hupitii kazi ya Mungu kamwe hutaweza kufanywa mkamilifu. Katika uzoefu wako, lazima pia uingie katika maelezo. Kwa mfano, ni vitu vipi hukuongoza kukuza dhana na nia nyingi sana, na ni aina gani za matendo yanayofaa uliyo nayo kushughulikia haya? Kama unaweza kupitia kazi ya Mungu, hii ina maana kwamba una kimo. Kama unaonekana tu kuwa na nguvu, hiki si kimo halisi na wewe huwezi kuchukua msimamo kabisa. Ni wakati tu mnaweza kupata uzoefu wa kazi ya Mungu na kutafakari kazi ya Mungu wakati wowote, mahali popote, mnaweza kumwacha mchungaji, muishi peke yenu kwa kumtegemea Mungu, na mnaweza kuona matendo halisi ya Mungu, ni hapo tu ndipo mapenzi ya Mungu yatatimizwa. Sasa hivi, watu wengi hawajui jinsi ya kulipitia. Wanapokumbana na suala hawajui jinsi ya kulishughulikia, hawawezi kuipitia kazi ya Mungu, na hawezi kuishi maisha ya kiroho. Lazima uchukue maneno ya Mungu na kuyafanya ndani ya maisha yako ya utendaji.
Mungu Mwenyewe ni maisha, na kweli, na uzima Wake na ukweli hutawala. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli kamwe hawatapata uzima. Bila mwongozo, msaada, na utoaji wa kweli, nanyi tu mtapata barua, mafundisho, na zaidi sana, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachoonyeshwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na njia Yake ya sasa ya kufanya kazi. Kama wewe utatumia rekodi ya maneno yaliyosemwa na Mungu wakati wa enzi zilizopita leo, basi wewe ni mtafutaji wa mambo ya kale, na njia bora ya kukueleza wewe ni mtaalamu wa urithi wa kihistoria. Kwa sababu wewe daima unaamini katika athari ya kazi ambayo Mungu alifanya katika nyakati zilizopita, amini tu katika kivuli cha Mungu alichowacha awali Alipokuwa Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, na kuamini tu kwa njia ambayo Mungu aliwapa wafuasi wake katika nyakati za zamani. Huamini katika mwelekeo wa kazi ya Mungu leo, huamini katika uso wa utukufu wa Mungu leo, na huamini katika njia ya sasa ya kweli iliyotolewa na Mungu. Na hivyo wewe ni mwotaji wa mchana ambaye hana ufahamu kamwe na hali ya mambo ya sasa. Kama sasa bado wewe unafuata maneno yasiyokuwa na uwezo wa kuleta maisha kwa binadamu, basi wewe ni kipande cha ukuni uliokauka kisicho na matumaini[a], kwa maana wewe ni mwenye kushikilia ukale mno, asiyeweza kutiishwa kwa urahisi, huwezi kusikiza wosia!
df19127ead