Tangazo la Kazi: Nafasi ya Mtunza Mazingira

79 views
Skip to first unread message

Tanzania Mailing

unread,
Jun 28, 2024, 3:47:55 AM (2 days ago) Jun 28
to arusha...@googlegroups.com

 

Tangazo la Kazi: Nafasi ya Mtunza Mazingira

 

 

Kuhusu Shule

Shule ya St Jude ni shule inayotoa elimu ya hisani ndani ya Tanzania. St Jude’s inafadhiliwa na wafuasi wa ukarimu kutoka kote ulimwenguni ambao hufanya dhamira yetu ya kuwapa wanafunzi wa Kitanzania mahiri na wanaotoka kwenye mazingira ya kimaskini elimu bure na yenye ubora.

 

Shule ya St.Jude inayofuraha kutangaza nafasi ya kazi ya mfanya usafi kwa watanzania wenye sifa stahiki.

 

Kazi na Majukumu

-       Kukata majani, fensi na kuchongea maua vizuri na katika mpangilio mzuri kwa kutumia mashine za kukata majani na mkasi.

-       Kuondoa mabaki ya chakula jikoni na nje ya bwalo kila siku asubuhi.

-       Kuondoa uchafu kwenye vyombo vya kukusanyia uchafu vilivyopo kwenye nyumba ya wageni.

-       Kukata majani na kutunza bustani kwenye nyumba ya wageni.

-       Kuzibua na kusafisha mifereji mikubwa mfano: pembeni na uwanja wa Campbell, karibu na jingo la utawala na nyuma ya jiko.

-       Kunyeshea viwanja wakati wa kiangazi kwa kutumia spirinkila na mpira wa maji.

-       Kuhamisha vitu toka sehemu moja hadi nyingine uhitajiwapo.

-       Kupunguza matawi ya miti.

-       Kunyunyuzia dawa ya kuulia wadudu kwenye maua.

-       Kutunza vifaa vya bustani mf: mashine za kukata majani, mikasi, bomba la kupulizia dawa.

-       Kuotesha maua kwenye maeneo yanapohitajika.

-       Kuhakikisha kwamba mazingira ya shule ni mazuri naya kuvutia wakati wote.

-       Kuhakikisha toka zote zinachomwa kwenye Tanuru la taka (incinerator).

-       Kupunguza matawi ya miti kwa kuwasiliana na ofisi ya Matengenezo katika kila kampasi.

-       Wajibu wa kuangalia miti na matawi yake ambayo ni hatarishi katika shule na kutoa ripoti katika Ofisi ya Matengenezo kwaajili ya kukata na kupunguza sawa sawa na Utaratibu wa Kukata na Kupunguza Miti.

 

Sifa za Mwombaji

-          Mwombaji awe na uwezo wa kutunza Mazingira vizuri ikiwa ni pamoja na kutumia mashine za Kukata majani

-          Mwombaji awe na uzoefu wa kutunza mazingira (Bustani, Maua pamoja na ukusanyaji na kutenganisha taka)

-          Mwombaji awe anaishi mazingira ya karibu na shule ya St Jude

-          Mwombaji awe Mtanzania mwenye Umri usio pungua miaka 28

Mwombaji awe na ujuzi wa kuwakarimu  watu na kufwata taratibu za kazi.

Vigezo na Masharti

Mwombaji anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo kikamilifu:

-          Aambatanishe barua ya maombi na Maelezo binafsi (CV)

-          Maombi yawasilishwe katika Shule ya St. Jude Moshono Kampusi kabla au mnamo Jumatatu, tarehe 1 Julai 2024. Maombi yatakayowasilishwa baada ya tarehe na muda uliopangwa hayatafanyiwa kazi.

-          TUTAWASILIANA NA WALE WATAKAOKIDHI VIGEZO NA SIFA KWA AJILI YA MAHOJIANO!

 

 

ANGALIZO:

TAFADHALI KUWA MAKINI NA MATENDO YA UDANGANYIFU KATIKA MATANGAZO YA KAZI NA MCHAKATO WA AJIRA. SHULE YA ST JUDE HAIOMBI MALIPO KATIKA HATUA YOYOTE YA MCHAKATO WA KUAJIRI. MAOMBI YOYOTE YA MALIPO YAKATALIWE NA KURIPOTIWA KWA MAMLAKA YA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA MITAA KWA HATUA STAHIKI.

 

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages