Tangazo la Kazi: Nafasi ya Mfanya Usafi

78 views
Skip to first unread message

Tanzania Mailing

unread,
Jun 28, 2024, 3:45:54 AM (2 days ago) Jun 28
to arusha...@googlegroups.com

 

Tangazo la Kazi: Nafasi ya Mfanya Usafi

 

 

Kuhusu Shule

Shule ya St Jude ni shule inayotoa elimu ya hisani ndani ya Tanzania. St Jude’s inafadhiliwa na wafuasi wa ukarimu kutoka kote ulimwenguni ambao hufanya dhamira yetu ya kuwapa wanafunzi wa Kitanzania mahiri na wanaotoka kwenye mazingira ya kimaskini elimu bure na yenye ubora.

 

Shule ya St.Jude inayofuraha kutangaza nafasi ya kazi ya mfanya usafi kwa watanzania wenye sifa stahiki.

 

Kazi na Majukumu

-       Fanya usafi wa samani (fanicha) vifaa, vyumba na maeneo ya jumuiya kama kumbi na mabwalo

-       Safisha na hakikisha unamwaga dawa ya kuuwa vijidudu maliwato na jikoni

-       Dumisha usafi wa vifaa na viwe katika hali nzuri.

-       Fanya kazi nyingine kama utakavyo agizwa na Mwajiri au mwakilishi wa  Mwajiri

-       Na kazi nyingine yoyote utatakayo pangiwa na kiongozi wako wa wa kazi kwa muda wowote

-       Kuhakikisha kwamba Vyombo vya Chakula havizagai ovyo hovyo

-       Kuweka kumbukumbu ya Vifaa vya Usafi vinavyotumika ili kusaidia kupnga Bajeti

-       Kuandaa chakula cha wanafunzi

-        

Sifa za Mwombaji

-          Mwombaji awe na uwezo wa kufanya usafi kwa ufasaha kwa kufuata ratiba

-          Mwombaji awe na uzoefu wa kufanya usafi kwenye shule, kampuni au taasisi.

-          Mwombaji awe anaishi mazingira ya karibu na shule ya St Jude.

-          Mwombaji awe Mtanzania mwenye Umri usio pungua miaka 25

-          Mwombaji awe na ujuzi wa kuwakarimu watu na kufuata Kanuni za Ajira

 

Vigezo na Masharti

Mwombaji anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo kikamilifu

-          Aambatanishe barua ya maombi na Maelezo binafsi (CV)

-          Maombi yawasilishwe katika Shule ya St. Jude Moshono Kampusi kabla au mnamo Jumatatu, tarehe 1 Julai 2024. Maombi yatakayowasilishwa baada ya tarehe na muda uliopangwa hayatafanyiwa kazi.

-          TUTAWASILIANA NA WALE WATAKAOKIDHI VIGEZO NA SIFA KWA AJILI YA MAHOJIANO!

 

 

ANGALIZO:

TAFADHALI KUWA MAKINI NA MATENDO YA UDANGANYIFU KATIKA MATANGAZO YA KAZI NA MCHAKATO WA AJIRA. SHULE YA ST JUDE HAIOMBI MALIPO KATIKA HATUA YOYOTE YA MCHAKATO WA KUAJIRI. MAOMBI YOYOTE YA MALIPO YAKATALIWE NA KURIPOTIWA KWA MAMLAKA YA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA MITAA KWA HATUA STAHIKI.

 

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages