NENO LA LEO 28.03.2012 WEWE NI WA THAMANI

19 views
Skip to first unread message

Eliezer Mwangosi

unread,
Mar 27, 2012, 10:12:36 PM3/27/12
to

Salaam,

 

Ujumbe  unatoka:  1Petro 1:18-19

Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa Damu ya THAMANI, kama ya mwana kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.

tAFAKARI:

Marafiki zangu leo nina habari njema kwenu, bila kujali hali uliyo nayo, jinsi unavyojiona na kujisikia, jinsi watu wengine wanavyokuona, neno la Mungu linasema wewe ni wa Thamani kubwa mbele zake. Sikiliza hata jamii ikudharau, eidha kwa umaskini au kwa maisha ya Dhambi, Mungu bado anakuona ni wa thamani. Kumbuka kuna Yesu Kristo alitoa uhai kwa ajili ya wanadamu wote, wakiwa bado katika Dhambi.


Mara nyingi Shetani anapenda kuwadanganya watu kwa tamaa za mwili, halafu anawaacha wakiwa na hali mbaya, kuna wengi hata wanakosa ujasiri kutokana na maisha ya aibu ya dhambi waliyoyapitia hapo nyuma, lakini pia kuna watu wananyanyasika kutokana na hali zao za sasa, huenda ni uchumi au hali duni za maisha, habari njema ni hii; hata wote wakuache na kukudharau, Upendo wa Yesu utazidi kuwepo kwako ukikuzingira Daima.


Wakati mwingine wanaume wanajifanya Mabwana wa kunyenyekewa na wanawake, hasa siku hizi utasikia wanasema “Ukilinga nitakuacha na kuchukuwa mwingine” na wakati mwingine anakata mawasiliano makusudi ili aone unavyohangaika.  Wapendwa mbele za Mungu wote ni wa Thamani, tusitumie nafasi tulizonazo vibaya, akina mama na mabinti, nyie ni wa thamani sana, sio vyombo vya kutumiwa na kuachwa hovyo, acheni tabia za kujirahisi au kujiona watu duni, mtegemeeni Mungu naye atawakweza.

 

Ni nini kinakuletea majuto moyoni? Huzuni hizo zinatoka wapi? Nani anakudharau na kukuona hufai? Ni nani anakuonea na anataka kukuendesha kama gari bovu? Kwa Damu ya Yesu wewe ni wa Thamani kubwa, Ukiwa ndani ya Yesu wewe si Duni tena, amini hivyo na ndivyo ulivyo.   

 

MAFURIKO YA BARAKA YAKAWE JUU YENU WOTE SASA NA HATA MILELE – NAWATAKIA SIKU NJEMA

 

Ev:  Eliezer Mwangosi.

Kwa masomo zaidi fungua mitandao ifuatayo: http://emwangosi.blogspot.com/ (Vijana) http://kayanafamilia.blogspot.com/ (Ndoa) http://matengenezo.blogspot.com/ (Ujumbe wa Matengenezo)

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages