Tanagzo la Semina maalum

42 views
Skip to first unread message

Daniel Mwakitalima

unread,
Jul 29, 2015, 4:32:36 AM7/29/15
to arusha...@googlegroups.com

        

  

 

                                         

 

 

                                                                                                                                                                                                                        Date:  29/07/2015

 

                                                               TANGAZO LA SEMINA MAALUM

                                                                        YA

KUWAJENGEA WAMILIKI WA BIASHARA UWEZO WAKIUFUNDI WA KUANDAA NA KURATIBU NA KUSIMAMIA MPANGO WA BIASHARA ZAO

 

Kampuni ya Ushauri katika masuala ya Uongozi na uendeshaji wa Biashara iitwayo The Big Picture Consulting iliyopo hapa jijini Arusha, hivi karibuni ilifanya utafiti wa kina kuangalia jinsi huduma kwa wateja inavyotolewa katika sehemu mbalimbali za biashara hapa jijini Arusha.

Matokeo ya utafiti huo ni kwamba pamoja na bishara nyingi kuwa na mazingira mazuri na ya kuchangamka kijasiriamali lakini kwa upande wa utoaji huduma kwa wateja kasoro nyingi zilionekana wazi wazi. Aidha, biashara nyingi hazina ‘Mpango wa Biashara’ (Business Plan) wala ‘Mpango wa Urithishwaji’ katika Biashara (Business Succession Plan). Kasoro hizi zote zimechangia sana biashara nyingi aidha kutokuwa endelevu na kufa kabisa ama kujisahau hasa katika suala la Ubunifu na Mabadiliko’ na kushindwa kuchangamkia fursa zinazojitokeza kila kukicha katika ushindani wa biashara!

Kwa kutambua mapungufu haya yote na mengineyo, na umuhimu wa biashara yako kuendelea kutoa huduma iliyotukuka zaidi hapa Mkoani na kwingineko, Kampuni ya the Big Picture Consulting Ltd imeandaa semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kitaalamu wa jinsi ya kuandaa na kusimamia mpango wa biashara mbalimbali. Pia, tutasikiliza kero na changamoto zinginezo zinazoambatana na biashara yako yoyote ile na kuweza kukutengenezea uwezo na namna ya kukabiliana nazo barabara.

Tafadhali onyesha utayari wako wa kuungana nasi kwa kulipia gharama ya shilingi elfu 25,000 tu za kitanzania katika ofisi yetu tajwa hapo juu au nenda ofisi ya Gola Foundation iliyopo katika jengo la CCM Sanawari karibu na Mataa ya traffic/Naura Spring hotel kabla ya siku ya mafunzo.  Pia, ukipenda kulipia kwa njia ya M-pesa, tafadhali wasiliana nasi ili tukupe maelekezo zaidi. Mafunzo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumapili, tarehe 9/8/2015, saa saba mchana pale jengo la CCM/Naura Spring-Sanawari. Cheti kitatolewa baada ya mafunzo. Tafadhali zingatia muda

Mambo muhimu yatakayofundishwa kwa undani katika suala zima la Mpango wa Biashara ni haya yafuatayo:-

      Maana ya  mpango wa biashara

Sababu za kuwa na mpango wa biashara

Waandaaji  na watumiaji wa mpango wa biashara ( ni kina nani na kwanini wanautaka? )

Namna ya kuandika mpango wa biashara

ü        Jinsi ya kutumia mpango wa biashara/ujasiriamali

ü       Changamoto na makosa katika biashara/ujasiriamali na ufumbuzi wake

 

Walengwa/wahusika katika semina hii ni wafanyabiashara wa ngazi zote, wajasiriamali wa ngazi zote, watu binafsi walioajiriwa na wasioajiriwa, wanafunzi wa vyuo n.k.Semina hii itaendeshwa kwa lugha yetu ya kiswahili

Tafadhani hudhuria semina hii muhimu sana kwa maendeleo ya biashara yako ili kwenda sambamba na mabadiliko yanayotokea hapa nchini na duniani kote. Tafadhani usikubali kubaki nyuma.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa kutumia mawasiliano hapa chini



Serengeti Road adjacent Barclays Bank

+255 755 819611, 713 232772

P.O Box 14456,Arusha,

Tanzania- East Africa

Email: dakit...@gmail.com

dalam...@yahoo.com

 

 








--
Daniel Lazarus Mwakitalima
Chief Executive Officer
The Big Picture Consulting Co. Ltd
P.O.Box 14456
Arusha 
Tanzania-East Africa 
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages