Wapendwa watumishi wenzangu,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(WAMJW) kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP), imeandaa mikutano kuwakutanisha wadau wote
wa mfumo wa Ugavi wa Dawa na
Vitendanishi vya UKIMWI na kujadili
kuhusu, Mafanikio na changamoto zinazoukabili mfumo wa ugavi wa Dawa na
Vitendanishi vya UKIMWI nchini ili kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa hizi kwa wakati na
zikiwa na ubora sahihi.
Hivyo basi mkiwa wadau muhimu mnaalikwa kuhudhuria
Mkutano wa wadau utakaofanyika kanda ya Mwanza,kuanzia tarehe
27 mpaka 28 Oktoba 2016 katika ukumbi wa NYAKAHOJA kuanzia
saa tatu kamili asubuhi.(Tunaombwa kuzingatia mabadiliko ya ukumbi siyo VETA kama ilivyoandikwa katika barua ya mwaliko iliyoambatanishwa).
Barua ya mwaliko kupata ruhusa ikiwa na orodha ya waalikwa imeambatanishwa pamoja na barua pepe hii.
Gharama
za usafiri na posho za kujikimu zitalipwa kwenye akaunti ya mtumishi husika kwa
mujibu wa taratibu za serikali. Washiriki wanatakiwa watumie usafiri wa gharama
nafuu na watarejeshewa nauli zao baada ya kutoa stakabadhi halali za safari.
Washiriki wanapaswa kuja na nakala ya malipo ya mshahara (salary slip),
kitambulisho cha kazi na akaunti number .
Tafadhali mnaombwa kuwajulisha waalikwa wote ambao hawajapata barua pepe hii.
Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano mzuri kwa manufaa ya umma.
Saulo Lucas Sarungi
Mfamasia
Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI
0767 173 975