watendaji wa halmashauri wanapowakimbia AZAKi

0 views
Skip to first unread message

Bernard Komba

unread,
Nov 10, 2009, 11:24:49 AM11/10/09
to reginad mengi, kristo yesu, W I, KITU CHEUPE UKWELI, YESU YESU, SANAWA CHANGAMOTO, a b, gazeti la kenya, habari fms, look tazama, daima freemedia, katoliki kanisa, tumaini tuma, first last, RAIA RAIA, MATUKIO GOOGLE
Ben Komba/Pwani/11/10/2009 4:44 PM

Watendaji wa halmashauri ya Mji wa Kibaha kwa kile kilichoonekana kwa wengi kama kukwepa kwa makusudi kikao kati yake na AZAKi zilizopo Mjini hapa kushindwa kutokea.

Mpaka inatimu saa sita kamili mchana kulikuwa hakuna hata mtumishi mmoja kutoka Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha aliyeonekana katika ukumbi wa mikutano.
Hali ambayo iliwaacha na butwaa waalikwa wengine na wawakilishi kutoka AZAKi mbalimbali, ikiwa pamoja na mwakilishi wa POLICY FORUM, kikao hicho kilikuwa ni mwendelezo wa kikao cha awali kilichofanyika April 23 mwaka huu.

Ambapo AZAKi baada ya kukamilisha utafiti wa matumizi ya bajeti ya halmashauri ya mji wa Kibaha na kuziwakilisha katika kikao hicho na wakuu wa Idara kuzikanusha na kuomba yaishe ili wakajipange kujibu hoja hizo za msingi katika kujenga utawala bora.

Lakini kinyume chake wakuu hao wa idara wa halmashauri ya mji wa Kibaha wakakubaliana kwa kauli moja kutohudhuria kikao hicho walichokuwa wakikifahamu fika zaidi mwananchi BW.GEORGE SEMWAIKO mtaalam wa masuala ya maboresho ya serikali za mitaa.

Amebainisha majibu rahisi waliyotoa halmashauri ya Mji wa Kibaha yanayotokana na maswali magumu ambayo yaliwakimbiza katika kikao cha kwanza na kudai kuwa wanaenda kujipanga upya ni majibu ya kejeli kwa wananchi wenye taaluma mbalimbali kwa kuwachukulia kama MAMBUMBU, MZUNGU WA RELI.

Amewasisitizia waalikwa na wawakilishi wa AZAKi kuendelea na ufuatiliaji wa matumizi bora ya fedha za bajeti ya halmashauri ya mji ili kutoa mwanya kwa mabadiliko ya kiutendaji kwa wakuu wa idara wa halmashauri hiyo ambao wengi wao wameonekana kujisahau.

Kumekuwa na mwamko mkubwa miongoni mwa wananchi kuhusu ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma, mafanikio hayo ni pamoja na kuzingatiwa kwa sauti za wananchi katika mipango mbalimbali ya maendeleo yao.
Mmoja wa wawakilishi wa AZAKi, BI.AICHI NGURE amelaani ya baadhi ya viongozi kuchukulia kero zinazohojiwa na wananchi kama kero badala ya kuwashukuru kwa kuwakumbusha wajibu wao kutokana na wao mara nyingi kuwa na kazi nyingi.

BI.NGURE ameongeza pamoja na serikali kutaka wananchi waibue miradi ya maendeleo katika mitaa yao, Lakini inapofikia hatua ya kutoa zabuni halmashauri inapora jukumu hilo na kumleta mkandarasi wanayejua wao ambao mara nyingi, hufanya kazi chini ya kiwango.

Naye SHEIKH KILANGA mwakilishi kutoka BAKWATA kwa upande wake amesema ushirikishwaji wa wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo bado ni mdogo kunakotokana na wakuu wa Idara katika halmashauri kuhofia wananchi kujua kila kitu na kuziba fursa ya wao kufanya ubadhirifu.

Mbali ya kutoshirikishwa kwa wananchi hata baadhi ya miradi kama vikwazo,fursa katika maendeleo, mpango ambao ulinuia kutambua mahitaji ya jamii kikamilifu, mradi huo ambao kwa mara ya mwisho kutekelezwa mjini Kibaha ni mwaka 2002, toka hapo mradi huo umebaki katika makabrasha,mpango huo wa fursa na vikwazo katika maendeleo maarufu kama O&OD.

Katika hatua nyingine wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa walijitambulisha rasmi mbele ya mkutano huo na kuahidi kuwatumikia wananchi waliowachagua kwa uaminifu mkubwa ikiwa pamoja na kuhakikisha miradi wanayoiibua inatekelezwa kikamilifu.

Halmashauri ya Mji wa Kibaha ina mitaa 53, kwa kutumia nafasi zao wameahidi kwenda kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kuhusu kuzinduka kutoka usingizi mzito wa kuwaamini viongozi wetu kupita kiasi wakati wenyewe wameshatusaliti na kutuchukulia sisi kama matutusa.

Naye mwakilishi wa POLICY FORUM katika kikao hicho kilichohusisha AZAKi na wakuu wa Idara ya halmashauri ya Mji wa Kibaha, BW.MARCOSSY ALBANIE amezungumzia kitendo cha kutojitokeza kwa watendaji hao, kunaonyesha jinsi gani utafiti wao ulivyokuwa makini kiasi cha kuwafanya kukosa hoja.

Mmoja wa wajumbe mpya wa Serikali ya mtaa wa Mailimoja mjini Kibaha, BW.ATTIK MOHAMED alitumia fursa hiyo kama wenzake kwa kwenda mbali zaidi kwa kuwahakikishia wananchi kuwa ana lengo la kuongeza kasi na nguvu ya utekelezaji wa sera ya maendeleo ya wananchi.

Maoni hayo na mengine mengi yaliyozungumzwa nwa wananchi katika kikao hicho kilichosusiwa na halmashauri ya mji wa Kibaha, ni vyema serikali ikayatupia macho, kwani baadhi ya miradi iliyotekelezwa kwa shinikizo ilifanywa kwa kulipuliwa ili mradi waseme fedha zimetumika.

Kwa hali hiyo juhudi zote za serikali kutaka kufanya mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kisiasa zimekuwa zikipata kizingiti cha awali cha utekelezaji wake, yaani katika halmashauri ambayo inawajibikaji kusaidia miradi iliyoibuliwa na wananchi wenyewe katika ngazi ya awali kabisa ya mtaa, na mwanzo wa nchi ni mitaa na vijiji, kupuuzia maendeleo ya mitaa ni kupitwa na wakati kifikra.
END.


Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages